Kwa mtazamo wangu kutokana na research ndogo niliyoifanya inaonyesha kwa sasa swala la gonjwa la ukimwi si kama ilivyokuwa kama miaka ya nyuma na kadri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kuchukulia poa na kuona kama mtu kuugua mafua na maisha kuendelea kama kawa..!!
Nimetumia neno kuchukulia poa kwasababu katika watu ambao nawakusudia zaidi ni vijana ijapokuwa wote nataka twende sawa ila kwa vijana ni too much..!!
Leo hii NGONO imekuwa ndio inawatumikisha sana watu,utakuta watu wapo bize sana kwa ajili ya kufanya NGONO.wanatafuta pesa,wanaongopa,wanatumia muda mwingi sana na kufanya kila linalowezekana ili tu mwisho wa siku wafanikishe kufanya NGONO.
Siku hizi idadi ya walio wengi wanapenda sana ngono na upendo wa dhati unakuja baada ya kufanya ngono na hii inasababisha idadi ya wanaooa/kuolewa hupungua kila kukicha maana inakuwa ngumu kudumu kwa kutokupata kile ambacho either alikitegemea kabla ama alitaka tu kuona kiundani inakuwa aje..?
Mapenzi yanadumu miezi kadhaa tu then wanaachana ama mtu mmoja anakuwa na zaidi ya mpenzi mmoja na ndo pabaya sana hapa..
Unayemuamini ana wapenzi wawili nawe ukiwa wa tatu,hapo hapo nawe unakiacha unayemuamini unao wengine wa kuzugia pengine watatu,inaweza ikawa mpenzi wako unayemuamini hayuko poa kifedha hivyo kuna wa kukununulia vocha na matumizi mengine huku ukiwalipa kwa penzi lako lakini huna future nao,uliye na future nae ndiye huyo mwenye wapenzi wawili wewe ukiwa wa tatu na yaweza kuwa mmoja tu kati ya hao ndo unatumia kinga tena pia pengine siku za mwanzo mwanzo tu na mkishazoeana inakuwa mpango....!!
Hapa UKIMWI utatukosa ??
Kama ulikuwa hujui automatically kama utamsaliti mpenzi wako jua ya kuwa nawe atakusaliti ama anakusaliti...!!
Jamani,jamani UKIMWI upo tusijisahaulishe kama vipi tuwe na mmoja na yakishindikana hayo TUVAE..!!
Ni hayo tu kwa leo toka kwangu kuja kwenu.
Mustapha E. Hanya
Mustapha E. Hanya