Call / WhatsApp +255673378129

Oct 31, 2017

TUMEFUNGA TV 15 | DISH 1 | MUHIMBILI HOSPITAL

Ilikuwa ni kazi ya siku moja ama 2 ila kutokana na mazingira yalivyo imetuchukua wiki 2 ama 3.. hii ni sehemu ambayo haitakiwi kelele na inapotokea idadi ya wagonjwa ni kubwa hakuna nafasi ya kina sie kufanya tulichokifanya hivyo ikawa tunachagua siku maalumu katika wiki ili kulitimiza hili tulilolifanya..
Huu ni mfumo ambao umetumia Dish 1 Decoder 1 lakini picha imeenda kwenye tv 15 na zote zikiwa saaaafi huku tukiacha wagonjwa wakipata alau taarifa ya habari...!


Tupigie +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Oct 30, 2017

STARTIMES UNALIPIA KIFURUSHI HAKIFIKI MWEZI!?

Jinsi inavyokuwa:- Kuna aina tofauti ya vifurushi kwa king'amuzi cha Antenna na Dish pia
Watumiaji wengi wa king'amuzi cha StarTimes hulipia pengine 9,000 ama 6,000 na kutegemea kifurushi alicholipia kiishi kwa muda wa mwezi mmoja,matokeo yake kinaenda wiki moja ama hata wakati mwengine hakifiki wiki malipo yanaisha na mtumiaji kutakiwa kulipia tena,hapa ndipo wateja wengi hutamani kukibeba king'amuzi na kukipiga chini!!!
Usichokijua ni kwamba:- Kifurushi ulichopo ni cha juu,yawezekana upo kwenye kifurushi cha Tsh 24,000 ama cha Tsh 36,000 hivyo inapotokea umelipia Tsh 9,000 ama Tsh 6,000 itahesabu siku hivyo haitafika mwezi channel zitakata!
Unachopaswa kufanya:- Ikiwa hujua upo kifurushi gani ni bora kufanya jambo moja la msingi upige simu kabla ama baada tu ya kulipia ili uhamishiwe katika kifurushi unachokitaka kikuwezeshe kufika mwezi mzima!
Kwa Maelezo zaidi!
+255789476655
Whatsapp +255784378129



Share:

Oct 29, 2017

KWENYE NYUMBA 1 | TUMIA DISH 1 KWA WAPANGAJI WOTE


Imezoeleka kufanyika kwenye Aparment kubwa,ambapo gharama na hata mfumo wake huwa expensive ila leo nikupe siri, mfumo huu unaweza kuwa rahisi na bora kwako hata wewe ambaye unamiliki nyumba ambayo sio apartment kuubwa, hata nyumba ya kawaida ambayo ina wapangaji ama mnaishi wenyewe tu familia na mngependa kutumia Dish moja ama Antenna moja kwa tv zote zilizopo kwenye nyumba yako na kila tv ikiwa na king'amuzi chake, kinachotumika kwa wote ni Dish ama Antenna isipokuwa king'amuzi kila mtu anakuwa na chake na analipia vile apendavyo! tumeifanya rahisi kwako ambapo kwa gharama ndogo itakuwezesha kumudu. Hii ni kwa wamiliki wa nyumba ambao mmekusudia ziwe za biashara kwa maana kupangisha,tumeona msuguano uliopo hivi sasa kwenye majumba mengi pale ambapo tumepata kazi ya kwenda kufunga madish,kuna upishani kati ya mwenye nyumba na mpangaji na mara nyengine hutokea upishani kati ya fundi na mteja wake ambaye ni mpangaji wa hiyo nyumba,upishani hutokea pale ambapo mmoja anapopendekeza dish ifungwe mahali fulani huku fundi akitaka ifungwe mahali fulani mwisho wa ubishani huu mara zote fundi huwa mshindi kwakuwa dish haifungwi tu kama inavyofungwa Antenna ya kawaida,dish inamuelekeo wake maalumu na ni lazima ufatwe.



Technology ambayo inatumika imewarahisishia wenye nyumba na pia,nikupe faida kiuchache:-wapangaji
Faida kubwa anayopata mwenye nyumba ni kuepuka uharibifu wa nyumba yake. Faida nyengine ni jengo ama nyumba kuwa safi ( Muonekano mzuri )
Faida anazopata mpangaji ni kupunguza gharama za kufunga na kurepair king'amuzi.

 Dish ambazo zina wateja wengi.

Antenna.

INAFANYAJE KAZI:-
  • Inafungwa Dish moja ama mbili zile zinazopendwa kutokana na eneo ulilopo ama utapata ushauri toka kwetu.
  • Unaweza ukafunga na Antenna 1 kama kutakuwa na ulazima huo.
  • Inaenda Cable kwa kila Point ya Tv kwa nyumba ama jengo lote husika.
  • Kila mpangaji/Mkazi wa hiyo nyumba/jengo atakachopaswa kuhamia nacho/kununua ni king'amuzi tu na kuchomeka pasipo kufunga tena Dish/Antenna.
  • Kila kwenye tv ( King'amuzi ) ataweza kufurahia matangazo pasipo kumuingilia mwengine.
  • Ikitokea kuna repair wahusika wote watahusishwa ama watahusika kwakuwa Dish/Antenna ni moja.

 INAWEZEKANAJE?
     Tupigie  +255789476655  
Whatsapp+255784378129
Email:mustaphamadish@gmail.com
Popote Tanzania ukituhitaji tunafika kwa kazi zifatazo:-
  • Kufunga mfumo wa TV kwenye Hotel
  • Kufunga mfumo wa TV kwenye Apartment
  • Kufunga mfumo wa TV kwenye Nyumba binafsi
  • Kufunga mfumo wa TV kwenye Office
  • Kufunga mfumo wa TV kweny Lodge/Bar n.k
  • Kufunga CCTV Cameras kwenye Hotel/Apartment/Office n.k
  • Kufunga Electric Fence kwenye Yard/Apartment/Office n.k
Share:

Oct 15, 2017

CABLE SNAKE BUNNINGS


Hiki ni kifaa maalum ambacho kinatumika katika kuvuta wire unaopita kwenye Conduit, hutumika pale inapotokea ugumu katika kupitisha cable ili uweze kufika kwenye point husika..
Cable Snake mara nyingi hutumika pale tunapofanya Installation kwenye Apartment, Hotel, n.k

Naseer - Zao la Mustapha MaDish akifanya yake na Cable Snake

Technical Director akizungumza na mjomba Cable Snake

Karibu kwa Ushauri, Huduma na Yote yanayohusu burudani ya TV.
Whatsapp+255784378129
+255789476655
Share:

Oct 14, 2017

TUNAKUFANYIA KILICHO BORA KWA KIPATO ULICHONACHO!

Niliwahi kusikia na watu wengi huamini hivyo ya kuwa ili upate kilicho bora ni lazima uwe na salio la kutosha imani ambayo sisi #MaDishTechnology tunapingana nayo na tunakuhakikishia wewe mdau wetu ya kuwa hata kwa kipato chako kidogo unaweza kupata kitu kilicho bora!

 Ubunifu wa Technical Director - Mustapha MaDish

Tunazingati usafi, Ubora, Tunathamini kile ulichonacho nasi kazi yetu kukipandisha thamani!
Hapa kuna mapungufu ya vifaa ambavyo vilihitajika lakini kutokana na kipato cha mteja wetu tumefanya kilichowezekana.. Najua unajua kwa muonekano huu hata ingelikuwa wewe ungependa tu pasi hivyo vilivyokosekana kuwepo!!
Msamila - 1 kati ya walionufaika na Mustapha MaDish

Tutafute sasa unufaike na huduma zetu zilizo bora
Kama unahitaji tukubadilishie mandhari ya eneo lako iwe:-
  • > Nyumbani
  • > Apartment
  • > Lodge
  • > Hotel
  • > Club / Bar
  • > Office 
Na popote pale ambapo wewe ungependa sisi tukupendezeshee!
Mustapha MaDish : +255789476655 | Whatsapp+255784378129

Share:

Oct 11, 2017

DISH 1 YA DSTV DECODER 91 ROOM 168

 

APARTMENT INSTALLATION:

Jengo la Apatment husika

 Mustapha MaDish

 Kinachofanyika hapa kinawezekana hata kwenye nyumba yako ya kawaida ambayo ina room 3 ama zaidi, Hostel n.k. Inawezekanaje !?
Hii ni Apartment ina jumla ya nyumba 91 na ina vyumba ambavyo vinahitaji tv zaidi ya 168 hapa inahitajika DStv tu kwa sasa isipokuwa tunachokifanya tunaacha mwanya wa King'amuzi chochote kuunganishwa katika muunganiko huu! Hii ndio kazi ya MADISH TECHNOLOGY.
      > Tv System Installation:-
  • HOTEL INSTALLATION
  • OFFICE INSTALLATION
  • APARTMENT INSTALLATION
  • HOSTEL INSTALLATION
  • LODGE/GUEST INSTALLATION
  • CLUB/BAR INSTALLATION 
 Mustapha MaDish
Kwa maelezo zaidi piga 0789476655 / Whatsapp+255784378129




Share:

Oct 3, 2017

OFFER YA AZAM TV 2017 KUELEKEA 2018

King'amuzi ambacho ni mpinzani pekee wa DStv kwa Tanzania na ni kweli kinafanya vizuri sana hasa bila kumung'unya maneno..!
Siku za usoni nitakuja kuwajuza sababu ya king'amuzi cha azam tv kufanya vizuri na kuchuana na mkongwe wa Digital Tanzania DStv ili wanaowasindikiza wengine wapate kujifunza!
Bei ya Azam tv ni kama ifatavyo:-
  • Vifaa Tsh 135,000/=
  • Ufundi ( Kufungiwa ) Tsh 30,000/=
  • Vifurushi kwa wiki kuna Tsh 5,000/= na Tsh 7,000/=
  • Vifurushi vya mwezi Bofya Hapa
Kwa mchakato huu Azam tv hawana offer ya kumalizia mwaka na kama itatokea tutapeana taarifa! 
Kwa Maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Oct 2, 2017

OFFER YA DSTV 2017 KUELEKEA 2018


FUNGA MWAKA NA DSTV
Offer hii inakupa unafuu kama ifatavyo:- 
  • Kwa Tsh 79,000/= Unapata Vifaa pamoja na kifurushi cha mwezi mmoja ( Bomba Tsh 19,000 )
  • Ufundi Tsh 30,000/=
  • Vifurushi vya DStv Bofya Hapa
DStv ni king'amuzi ambacho naweza nikasema kwa offer kinaongoza na licha tu ya mara kwa mara kutoa offer hata sokoni pia ina base kubwa sana ya watumiaji, ukiachilia mbali yote hayo kwa ukongwe hiki ndicho king'amuzi kikongwe

Kwa Maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita