Call / WhatsApp +255673378129

Dec 31, 2017

LNB NI NINI...??

Kwenye Technology kuna vifaa ambavyo kuvitafutia lugha ya kiswahili moja kwa moja hakuna ila nitakachojitahidi kufanya ni kukupa urahisi ili uelewe pasi kutoka nje ya maana yenyewe.



LNB ni nini?
LNB ama kwa kirefu chake ni Low Noise Block downconverter, ni kidubwana,kifaa kidogo kinachokaa kwenye dish ambacho kinapokea signal toka kwenye satellite na kupeleka kwenye satellite receiver ( King'amuzi kinachotumia dish ). Pia huitwa low-noise converter (LNC), au low-noise downconverter (LND), hiki kifaa wakati mwengine kinaitwa low-noise amplifier (LNA).

LNB ni mchanganyiko wa low-noise amplifier, frequency mixer, local oscillator na intermediate frequency (IF) amplifier. Inapokea microwave signal kutoka kwenye satellite iliyokusanywa na Dish, inaimarisha, na inachagua mzunguko wa mzunguko kwenye upeo wa chini wa mzunguko wa kati (IF). Hii downconversion inaruhusu signal kuletwa ndani kwenye Satellite receiver kwa kutumia Coaxial cable. ikiwa Signal ilibaki katika asili yake microwave frequency ingehitaji gharama kubwa na impractical waveguide line.

LNB kwa kawaida ni kisanduku kidogo kinachofungwa mbele ya uso wa dish kwa kutumia mfano wa fimbo ( kibomba/ vibomba ). Microwave signal kutoka kwenye dish inachukuliwa na  feedhorn kwenye LNB na hutolewa kwa sehemu ya waveguide.

LNB hufanyakazi kwa kutumia umeme ambao utatokea kwenye Satellite receiver kwa kutumia coaxial cable na huchomekwa sehemu iliyoandikwa LNB IN ikiwa imetumika pin katika kufanya coaxial cable kufunga kwenye Receiver na kwenye LNB pia.

AINA ZA LNB
  • Ku band 
  • Ka band
  • C band
Post hii itaendelea...
+255789476655
Whatsapp +255784378129

Share:

Dec 21, 2017

KUTUMIA KING'AMUZI KIMOJA KWA TV ZAIDI YA 1


Ving'amuzi vyote unavyovijua wewe iwe vya bure ama vya kulipia, nikiwa na maana vyenye kulipia malipo ya mwezi na visivyo na malipo ya mwezi, unaweza kutumia king'amuzi kimoja kwa tv zaidi ya moja, kwa kutumia king'amuzi kimoja unaweza kugawa picha kwa tv hata zikiwa 100.
Hii inawezekanaje!? kwanza unapaswa kujua ni king'amuzi gani ambacho unataka kugawa picha kwa tv zaidi ya moja,  chagua kwenye orodha hapo chini:-
NB:Nitaweka link kwa kila king'amuzi ambayo itakupeleka mpaka kwenye post ambayo itakuwa na maelezo yote kwa kina.
Kwa Maelezo zaidi hii hapa +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Dec 15, 2017

TELEVISION AU RUNINGA NI NINI!?

 Tv ya kijerumani ya mwaka 1956

Neno "televisheni" linatokana na maneno mawili: tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na visio (kutoka Kilatini: mwono; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza television lililotoholewa katika Kiswahili televisheni.
Televisheni - TV au runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.
Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.
Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita).
Baada ya Vita Kuu ya II, mfumo bora wa utangazaji wa televisheni Black n White ulikuwa maarufu nchini Marekani na Uingereza, na seti za televisheni zilikuwa za kawaida katika nyumba, biashara na taasisi.Katika miaka ya 1950, televisheni ilikuwa katikati ya msingi kwa kushawishi maoni ya umma.  Katikati ya miaka ya 1960, utangazaji wa rangi uliletwa nchini Marekani na nchi nyingi zilizoendelea.. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (widescreen).
Tangu mwaka 2010, kwa uvumbuzi wa smart television, internet television imeongeza upatikanaji wa programu za televisheni na sinema kupitia mtandao kupitia huduma za video za Streaming kama vile Netflix, Amazon Video, iPlayer, Hulu, Roku na Chromecast.
Aina za tv

Siku za usoni nitakuja kuzungumzia kwa kina kuhusu yaliyo hapa chini:
Broadcast Systems 
  • Terrestrial Television
  • Cable Television
  • Satellite Television
  • Internet Television
Display Technologies
  • Disk
  • CRT
  • DLP
  • Plasma
  • LCD
  • OLED
  • LDTV
  • SDTV
  • HDTV
  • UHDTV
 Imeandikwa na Mustapha Hanya
Whatsapp+255784378129
Share:

Dec 14, 2017

UTAJUAJE KAMA TV YAKO INA KING'AMUZI NDANI?


Swali la wengi kwasasa ni hili kutokana na ukweli kwamba uondoshwaji wa local channels kwa baadhi ya Visimbuzi imekuwa kama janga hivi.. Sasa niwape namna ya kujua jinsi gani ya kupata local channels kupitia tv ikiwa ina kisimbuzi ndani, inaweza ukatumia Antenna ama Dish inategemea na uwezo wa tv:-
Utajuaje kama tv yako ina kisimbuzi ndani?
  • Ingia kwenye INPUTs inategemea na brand, zipo ambazo zinatumia SOURCE, INPUT n.k unabonyeza na itakuletea orodha ya input zote mfano:-
AV
HDMI1
VGA
USB
ATV
DTV
Ukiona ina DTV ujue ina kisimbuzi.
  • Njia nyengine unachukua remote yako unabonyesha kwenye SETTING unaenda kwenye SEARCH hii nayo inategemea na tv, tv nyengine hutumia tune n.k hapa unaweza ukaweka AUTO SEARCH itakuletea Analogue tv na Digital tv ikikuletea hizo chaguo ujue tv yako ina kisimbuzi ila kama itakuletea Analogue tv pekee ujue haina kisimuzi..
 Ikiwa tv yako ina DTV maana yake inapokea matangazo ya Digital hivyo unapaswa kutafuta Antenna na kuchomeka muelekea wa Startimes/Ting ama Continental na kufanya search kama kila kitu kikiwa sawa channels zitaingia..
Kuna DVB T1/ T2 hii ni kwa ajili ya antenna.
Kuna DVB S1/ S2 hii kwa ajili ya dish.

Insta @mustaphamadish
Whatsapp+255784378129

Share:

Dec 13, 2017

UNALIPIA LAKINI INAKATA KABLA MWEZI KUISHA


Hii inaweza kutokea kwenye ving'amuzi vyote na hutokea makosa ya mtandao ama kama kifurushi ulichopo sio sahihi hivyo hakiwezi kufika mwezi kwa baadhi ya ving'amuzi! Mara chache mno hutokea kwa ving'amuzi kama cha Azam tv,DStv,Zuku, n.k. na huwa mara zote ni kufail kwa system tu na unachopaswa kufanya ni kutoa taarifa ili uweze kusaidiwa kwa kurudishiwa huduma. Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa upande waking'amuzi cha Startimes na huwa tofauti na ving'amuzi vyengine ili kujua zaidi Bofya hapa
Whatsapp+255784378129

Follow Insta @mustaphamadish
Share:

Dec 2, 2017

KING'AMUZI KISICHO NA MALIPO YA MWEZI


Awali tulikuwa na ving'amuzi viwili ambavyo havikuwa na malipo ya mwezi, kulikuwa na Digitek na Continental, baadae Continental wakaanza mfumo wa kulipia na kuwa na Vifurushi pia kutaka kujua zaidi kuhusu Continental decoder bofya hapa, tukabaki na Digitek ambapo ni king'amuzi pekee ambacho hakina malipo ya mwezi. Kwa kutokuwa na malipo ya mwezi kwenye king'amuzi cha Digitek kumefanya kwenye zile Tv ambazo zinauwezo wa kupokea matangazo ya Digital pasi kutumia king'amuzi kuwezesha kupata channels za Tanzania bila malipo yeyote na bila kutumia king'amuzi cha nje kwakuwa ndani ya tv kwa lugha nyepesi tunasema ina king'amuzi.

Kwa maelezo zaidi +255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita