NI BAADA YA JOPO LA
MADAKTARI MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI MPENDWA WETU S.KANUMBA.
MSANII nyota wa
filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa
ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu
zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani,
zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa
tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku
kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini
alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa
mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00
asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na
mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo.
Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo
wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa
ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua
kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma,
husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili
wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji
ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku
mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo
dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa
ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na
ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine
aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema
ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na
hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya
machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo
kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.
Baba mzazi azungumza Baba
mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa
za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada
wa marehemu, Sara Kanumba. “Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao
Kanumba?’ Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo
hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka,
amekorofishana na mpenzi wake.” alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe
nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… “Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa
simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu
amefariki.”
Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na
tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe
Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. “Nilikuwa nimepanga
apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake
kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi
ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka
nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam,”
alisema.
Pia alikanusha uvumi kuwa hajafika msibani kwa kuwa walikuwa na
ugomvi na marehemu akisema walishamaliza tofauti zao. Alisema anatarajia kufika
leo usiku tayari kushiriki mazishi hayo.
Wabunge kilio Jana, baadhi ya
wabunge waliofika nyumbani kwa marehemu Kanumba waliangua vilio wakati walipotoa
salamu zao za rambirambi.
Mbunge wa
Viti Maalumu, Martha Mlata hakuzungumza na badala yake aliimba kipande cha wimbo
uliozungumzia kifo na maneno ya wimbo huo yalionekana kuwagusa wafiwa na
kusababisha vilio kuanza upya huku baadhi wakipoteza fahamu.
Mbunge mwingine, Neema Mwinyimgaya aliongeza majonzi
masibani hapo alipounganisha msiba huo na wa mama yake… “Mama yangu amefariki
miezi mitatu iliyopita, huko uliko mama, nakuomba umpokee kijana mwenzetu,”
alisema mbunge huyo na kushindwa kuendelea.
Wabunge wengine waliohudhuria
msiba huo ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Aboud Juma (Kibaha Vijijini),
Mussa Azan Zungu (Ilala), Abbas Mtemvu (Temeke), Peter Serukamba (Kigoma Mjini)
na Ritha Kabati (Viti Maalumu).
Kova na mchango wa Kanumba Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema anakumbuka mchango wa
Kanumba katika kuzuia uhalifu jijini.
“Tulishirikiana naye pamoja na
wasanii wengine kuandaa bonanza maalumu ambalo lilidhamiria kukabiliana na
uhalifu hapa jijini na kwa kweli mchakato ule ulifanikiwa kwani uhalifu
ulipungua kwa kiasi kikubwa” alisema Kova.
“Kifo chake kimekuwa cha ghafla
mno na nafikiri kujiweka tayari (kiimani) ni jambo ambalo kila mmoja anatakiwa
kuwa makini nalo katika maisha yake,” alisema Kova.
Ratiba ya
mazishi
2:30 - Msafara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Barabara
ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club.
3:30
- Misa ya kumuombea na salamu mbalimbali.
6:00 – Kuaga
9:00 - Kuelekea
Makaburi ya Kinondoni kupitia Barabara ya Tunisia
0 Unasemaje..??:
Post a Comment