Tumeanza mwezi,mwezi ambao kwetu sisi waislamu una maana kubwa sana kwa haraka haraka tu huu ndio mwezi ambao quraan tukufu ndio ilishushwa mwezi huu na kwa uchache zaidi ndio mwezi ambao mwenyezi mungu anatusamehe dhambi zetu tulizonazo na tutakazokuwa nazo,ni mwezi ambao sio ombi bali ni lazima kwa kila aliyejaaliwa kufunga maana yake ni kwamba kama huna tatizo lolote kiafya litakalokufanya ushindwe kufunga ni lazima kufunga..
Mwezi huu unatukumbusha kuacha yale yote ambayo mwenyezi mungu ametukataza kama kuzini,kusengenya,kuongopa,kuiba,nk pia tunakumbushwa kwa nguvu zote kufanya yale tunayostahili kufanya kwa imani zetu kama kuswali,kutoa sadaka na kwenda hija kwa walio na uwezo..
Tunafundishwa kufunga na kuswali,kufunga bila ya kuswali sawa na hakuna funga..
Kuna mengi ya kufanya ili funga zetu zikubalike ijapokuwa vijana wana misemo yao kuwa swaumu za mjini zina kazi ila ukitia nia unafunga bila wasi na kumuachia mungu ndiye mwenye kujua umefunga ukiwa sahihi ama lakini kwa kuzingatia misingi yote ya funga.
Ugumu wa vijana wengi katika mwezi huu ni kutamani,sio kula laa kwakuwa katika maisha ya kawaida ya watanzania wengi ni swaumu,ila linawashinda la kuatamani kufanya ngono.
Kuona ndoa nyiingi inapofikia kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu ni jibu tosha la nini ambacho namaanisha,sasa kwa ninyi msiooa ama kuolewa swaumu kwenu zikoje!!???
Zaidi ya yote funga njema wapendwa mkumbuke kuswali na kutoa swadaka!
1 Unasemaje..??:
Nawe pia mkuu ubarikiwe sana kwa kazi nzuri unayofanya
Post a Comment