Call / WhatsApp +255755949413

Nov 18, 2010

IPS hostel chanika.....!!

Hapa ni Hostel za IPS college,chuo hiki kipo maeneo ya chanika na hapa ni katika hall lao ambapo ndipo wanapofanya maevent yao ila kikubwa ambacho kime7bisha mimi nifike hapa huwa wanaangalia TV kupitia ukumbi huu so wanamiss kitu kinachoitwa mpira ulio live bila chenga...!!






















Nilichofanya hapa na kuacha watu wakiangaza macho na kusababisha stori na vicheko toka kwenye TV ni DSTV EXTRA VIEW ambapo wanaweza kuona channel mbili kwa wakati mmoja kwa kutumia a/c moja.
Nimetumia Dish moja ila lnb ni twine ila Decoder ni mbili kama kawaida,ila napo pa kufunga ilikuwa tatizo maana miti ilikuwa mingi sana mwisho wa yote nikafanikiwa kudrill ukutani kwa kuizidisha stend kama inavyoonekana hapo juu....!!
Share:

Nov 17, 2010

Mwananyamala tena.......!!

Mahitaji ilikuwa zinatakiwa channel za bure ambazo ni nzuri,Dish nilizikuta ila ambacho mimi nilisaidia ni LNB tu.
Nikasababisha watu waangalie channel za Local,Asia pamoja na zile za MBC.
Ilikuwa hivi:-
Satellite Dish Antenna zilikuwa mbili KU na Cband
nam nikatumia ufundi wangu kusababaisha.
Share:

Some where in Mwananyamala....!!

Huyu jamaa nilimfungia kitaambo maeneo ya sinza pale,ila leo akataka kuhama hivyo nami nikamuhamisha na DSTV yake kama uonavyo,hii ni maeneo ya Mwananyamala A ndipo alipohamia sasa na mambo yalikuwa 
as usually:-
 









Picha hizi zote ni baada ya kumaliza kuinstall na ku7bisha wazungu kuonekana.

Share:

Nyumbani kwa mbunge wa bunge la A.Mashariki....!!

 Ni maeneo ya Chanika wanaita kwa Masantula,hapa bana ndo maeneo aishiyo mh.Didas Masabuli mbunge wa bunge la A.Mashariki,hata mwezi bado toka niende kurekebisha FTA ilikuwa inasumbua na hii ni toka nifunge karibu mwaka mmoja uliopita....!!!
 Ilikuwa hivi......:-
Hapa ni katika setting za kuweka c band LNB ya Local na Asia channels,zote zikiwa ni za bure.
Hapa tayari kwa kuuangalia signal zimeingia,zikiwa LNB zote mbili kama zinavyoonekana hapo.
Share:

Somewhere in Masaki.....!!!

Tupo kwenye mbio za OFFER ya DSTV hivyo tunayasababisha haya daily leo nipo maeneo ya Masaki kwa wakishua,huku nimesababisha DSTV na channel za GOSPEL ambazo ni za bure...!!














Hapa nishauza na tayari kwa kuchapa mwendo....!!
 
Share:

Some where in Mbagala.........!!!!

Actually kazi yangu imeweza kunitembeza sehemu nyingi sana kiasi kwamba hata se
hemu nyengine sikudhani kama kunawatu wanaishi huko ama ni nchi yetu hii hii Tanzania...!!!!Dah...!! mfano juzi nilikuwa sehemu 1 wanaita Mbagala,ila mbagala hii ipo ndani ndani sana,unaingilia zakiem kwenda kushoto.
Macho yangu yamethibitisha kwamba kuna maeneo ukifunga Dish wewe kidume,ndo kama huko Dish za kuhesabu na zote nilizoziona ni FTA ila DSTV ni hii tu niliyeenda kufunga mimi,hii inamaanisha ya kwamba jamaa kajiwekea alama ya kutosha hata kwa anaoishi nao karibu yaani inakuwa "ulizia palipofungwa Dish la DSTV na nyumba yetu inatazamana nayo".
Kazi ilikuwa kama ifuatavyo:-












Share:

Nov 12, 2010

OFFER Tsh 90,000/= DSTV INSTALLATIONS................!!

Hii ni ngumu kuamini ila ni kweli Multi choice Tanzania DSTV wametoa offer kwa wale wote watakao kujiunga.
Full installations ni Tsh 90,000/= ( utapata dish,decoder iliyo na LNB,cable mt 20 pamoja na kufungiwa )
Then itakulazimu ulipie air time ili uweze kuona.
Share:

Nov 2, 2010

OUR SERVICE'S MORE THAN YOUR PAYMENTS....!!

Tunakuhakikishia ubora na ndo maana tunathubutu kusema huduma zetu ni zaidi ya malipo yako....!!
Share:

Popote ulipo tunakuja na popote utakapo tunafunga.

Haijarishi wapi ulipo ila ukituhitaji tunakuja na kukufungia ama kukurekebisha,....!!
usiogope kama nyumba yako ni ya udongo tunazo njia za kukufanya nawe ukaenjoy kama upo masaki katika fukwe za bahari...!!
Share:

FLAT SCREEN INSTALLATIONS

Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA WHATSAPP +255755949413

Post zilizokupita