Call / WhatsApp +255673378129

Oct 15, 2017

CABLE SNAKE BUNNINGS


Hiki ni kifaa maalum ambacho kinatumika katika kuvuta wire unaopita kwenye Conduit, hutumika pale inapotokea ugumu katika kupitisha cable ili uweze kufika kwenye point husika..
Cable Snake mara nyingi hutumika pale tunapofanya Installation kwenye Apartment, Hotel, n.k

Naseer - Zao la Mustapha MaDish akifanya yake na Cable Snake

Technical Director akizungumza na mjomba Cable Snake

Karibu kwa Ushauri, Huduma na Yote yanayohusu burudani ya TV.
Whatsapp+255784378129
+255789476655
Share:

Oct 14, 2017

TUNAKUFANYIA KILICHO BORA KWA KIPATO ULICHONACHO!

Niliwahi kusikia na watu wengi huamini hivyo ya kuwa ili upate kilicho bora ni lazima uwe na salio la kutosha imani ambayo sisi #MaDishTechnology tunapingana nayo na tunakuhakikishia wewe mdau wetu ya kuwa hata kwa kipato chako kidogo unaweza kupata kitu kilicho bora!

 Ubunifu wa Technical Director - Mustapha MaDish

Tunazingati usafi, Ubora, Tunathamini kile ulichonacho nasi kazi yetu kukipandisha thamani!
Hapa kuna mapungufu ya vifaa ambavyo vilihitajika lakini kutokana na kipato cha mteja wetu tumefanya kilichowezekana.. Najua unajua kwa muonekano huu hata ingelikuwa wewe ungependa tu pasi hivyo vilivyokosekana kuwepo!!
Msamila - 1 kati ya walionufaika na Mustapha MaDish

Tutafute sasa unufaike na huduma zetu zilizo bora
Kama unahitaji tukubadilishie mandhari ya eneo lako iwe:-
  • > Nyumbani
  • > Apartment
  • > Lodge
  • > Hotel
  • > Club / Bar
  • > Office 
Na popote pale ambapo wewe ungependa sisi tukupendezeshee!
Mustapha MaDish : +255789476655 | Whatsapp+255784378129

Share:

Oct 11, 2017

DISH 1 YA DSTV DECODER 91 ROOM 168

 

APARTMENT INSTALLATION:

Jengo la Apatment husika

 Mustapha MaDish

 Kinachofanyika hapa kinawezekana hata kwenye nyumba yako ya kawaida ambayo ina room 3 ama zaidi, Hostel n.k. Inawezekanaje !?
Hii ni Apartment ina jumla ya nyumba 91 na ina vyumba ambavyo vinahitaji tv zaidi ya 168 hapa inahitajika DStv tu kwa sasa isipokuwa tunachokifanya tunaacha mwanya wa King'amuzi chochote kuunganishwa katika muunganiko huu! Hii ndio kazi ya MADISH TECHNOLOGY.
      > Tv System Installation:-
  • HOTEL INSTALLATION
  • OFFICE INSTALLATION
  • APARTMENT INSTALLATION
  • HOSTEL INSTALLATION
  • LODGE/GUEST INSTALLATION
  • CLUB/BAR INSTALLATION 
 Mustapha MaDish
Kwa maelezo zaidi piga 0789476655 / Whatsapp+255784378129




Share:

Oct 3, 2017

OFFER YA AZAM TV 2017 KUELEKEA 2018

King'amuzi ambacho ni mpinzani pekee wa DStv kwa Tanzania na ni kweli kinafanya vizuri sana hasa bila kumung'unya maneno..!
Siku za usoni nitakuja kuwajuza sababu ya king'amuzi cha azam tv kufanya vizuri na kuchuana na mkongwe wa Digital Tanzania DStv ili wanaowasindikiza wengine wapate kujifunza!
Bei ya Azam tv ni kama ifatavyo:-
  • Vifaa Tsh 135,000/=
  • Ufundi ( Kufungiwa ) Tsh 30,000/=
  • Vifurushi kwa wiki kuna Tsh 5,000/= na Tsh 7,000/=
  • Vifurushi vya mwezi Bofya Hapa
Kwa mchakato huu Azam tv hawana offer ya kumalizia mwaka na kama itatokea tutapeana taarifa! 
Kwa Maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Oct 2, 2017

OFFER YA DSTV 2017 KUELEKEA 2018


FUNGA MWAKA NA DSTV
Offer hii inakupa unafuu kama ifatavyo:- 
  • Kwa Tsh 79,000/= Unapata Vifaa pamoja na kifurushi cha mwezi mmoja ( Bomba Tsh 19,000 )
  • Ufundi Tsh 30,000/=
  • Vifurushi vya DStv Bofya Hapa
DStv ni king'amuzi ambacho naweza nikasema kwa offer kinaongoza na licha tu ya mara kwa mara kutoa offer hata sokoni pia ina base kubwa sana ya watumiaji, ukiachilia mbali yote hayo kwa ukongwe hiki ndicho king'amuzi kikongwe

Kwa Maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Sep 7, 2017

PENDA UNACHOFANYA..


ILI UFANIKIWE...  NIMEJIFUNZA KUZINGATIA MOJA KATI YA VITU MUHIMU.. NI KUPENDA UNACHOFANYA..
..... Hapa siangalii sana napata bei gani ingawaje pesa ndio ambayo hasa tunaitafuta.. Nna mengi ya kuzungumza hapa ila leo somo liwe moja tu kwa Vijana wenzangu na wote ambao mnataka kupata mafanikio katika kile mkifanyacho... Mpende mnachokifanya.. Ukipenda unachokifanya utakifanya kwa juhudi zako zote na wala hautaangalia wanaokukwamisha wanazidi kila kukicha.. Nilipoanza ilikuwa kama utani isipokuwa kwakuwa nilikuwa na mapenzi ya dhati na kazi yangu hivyo wala sikukata tamaa.. nilisimamia ninachokiamini na kujifunza zaidi.. mpaka leo hii idadi ya wanafunzi nilionao wala hakuna ulazima wa mimi kwenda site tena kufunga hata kadishi kamoja.. ningewatuma na bado kupitia wao ningeingiza pesa... Lakini katika vitu nisivyovipenda ni kukaa ofisini... mimi napenda muda wote kuwa site na ndo sababu mpaka leo hii utakapopata wasaa wa kutembelea office yetu ni mara chache sana kunikuta kwa Office nimekaa!
Share:

Sep 3, 2017

BEI & VIFURUSHI VIPYA AZAM TV

 

AZAM LITE
Tsh 10,000/=
Channels 55+
Kujua Channel zilizopo Bofya Hapa

AZAM PURE
Tsh 18,000/=
Channels 60+
Kujua channel zilizopo Bofya Hapa

AZAM PLUS
Tsh 23,000/=
Channels 90+
Kujua channel zilizopo Bofya Hapa

AZAM PLAY
Tsh 28,000
Channels 105+
Kujua channels zilizopo Bofya Hapa

Kwa Maelezo zaidi
Insta @mustaphamadish
+255789476655
Whatsapp +255784378129
Share:

Aug 29, 2017

DSTV YASHUSHA BEI ZAIDI | VIFURUSHI 2018


Habari njema kwa wadau wa kabumbu na wateja wote wa DStv kiujumla! Hii ni bei ilianza tarehe 1 mwezi wa 9 mwaka 2017 bei ambayo ni kama ifatavyo kwa Vifurushi vyote vya DStv:-
1.Premium kutoka 184000 mpaka 169000/= tu!
2.Compact Plus kutoka 122500/= mpaka 109000/= tu!
3.Compact kutoka 82,500/= mpaka 69,000/= tu!
4. Family kutoka 42,900/= mpaka 39,000/= tu!
5.Bomba kutoka 19,975/= mpaka 19,000/= tu!
Kwa Maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp +255784378129
Share:

UZIO WA UMEME KWA ULINZI


Tukikuhudumia unapata faida gani!?
  • Jengo na mali zako kiujumla kuwa salama
  • Bei nafuu ambayo mtanzania ni rahisi kuimudu
  • Tunakupa ushauri kabla ya kukuuzia huduma 
  • Tunafanya kazi ndani ya muda
  • Miezi 12 ( mwaka mmoja ) unapata repairing bure
  • Tunapita kufanya check up kila baada ya miezi mitatu
  • Tupo karibu na wewe saa 24.
  • Ni rahisi kutufikia
Tupigie kwa namba +255789476655 ama Whatsapp+255784378129
Tupo Dar es salaam
Popote Tanzania tunafika!
Share:

Aug 26, 2017

KWANINI USILIPIE MAPEMA | KING'AMUZI CHAKO!?


Nimejaribu kufatilia kwa ukaribu sana utaratibu wa kufanya malipo ya king'amuzi kati ya watumiaji wageni nikimaanisha wenzetu rangi nyeupe na sisi ngozi nyeusi ijapokuwa si wote isipokuwa wengi wetu tuna utaratibu mmbovu sana wa kufanya malipo ya ving'amuzi tunavyotumia...!!
Mfano ukute mzungu/ama muhindi utaratibu wake wa kulipia, mfano amelipia king'amuzi anachotumia tarehe 10 mwezi wa 11, atalipia tena siku mbili ama tatu nyuma kwa mwezi unaofata, anaweza akalipia terehe 7 ama 8 ama 9 mwezi wa 12 ambapo hukuti anapata usumbufu kuhusu malipo na uzuri zaidi ving'amuzi karibu vyote vina utaratibu wa kukutumia ujumbe tena kwenye king'amuzi chako ya kwamba kifurushi chako karibu kinaisha hivyo ufanye malipo mapema!
Wengi wetu sie kina ngozi nyeusi kama nimelipia tarehe 10 mwezi wa 11, sitafanya malipo mpaka kifurushi kitakapokata kabisa matokeo yake unatokea usumbufu wa hali ya juu.. wakati mwengine inaweza ikawa kipato hilo ni sawa siwezi lipinga ila hupaswi kungoja mpaka siku ya mpira ndipo ufanye malipo kwa maana mara zote siku za mipira sio Azam sio DStv huwa system zao zina elemewa na matokeo yake unapata maudhi usiyoyategema ambapo ungelipia siku moja ama mbili kabla ya mpira unaotaka kuangalia usingepata usumbufu hata kidogo!
Tujitahidi kubadilika wadau wa ulimwengu huu wa Digital tv... Kwa hili naomba niwe mkweli  ikiwa utalipia siku ya mpira na ukatafuta msaada umekosa hata mimi na managment yangu hatutakuwa na msaada ila kama utalipia siku 2 ama 1 kabla ya mpira msaada utaupata toka kwetu kwa king'amuzi chochote kile.
Kwa maelezo zaidi.....
 +255789476655 
Whatsapp+255784378129
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita