Niliwahi kupata swali kama hili na nilishawahi kuona matangazo sehemu kadhaa mitandaoni ya kuwa kama unatumia king'amuzi cha Startimes tunaingiza channel za Azam tv na DStv na tangazo lengine kama unatumia king'amuzi cha azam tv unaingiziwa channel za DStv na Startimes pia....
Matangazo ni ya wengine lakini huwa nafatwa mimi ili kuthibitisha hili kwakuwa najua uthibitisho wangu ni msaada wa watanzania na wasio watanzania wengi sana..
Licha ya kuwa matangazo wanatoa wengine na namba zao ni nyengine tofauti na namba zangu, wanaotaka kuwahudumia wakiwabana zaidi kwa maswali ama ikitokea tofauti yeyote wanawaelekeza wapitie blog hii kwakuwa ndiye muhusika huyo huyo..
Huko nyuma niliwahi kulalamikiwa hili kwa wahusika kunihusisha na jambo hili ila kuna issue ilikuwa imenibana sana hivyo nikakosa muda wa kuandaa post na mwishowe nikawa kama nimekaa kimya ila nashukuru hivi karibuni kuna jamaa mmoja ambaye ni Fundi MaDish yeye anapatikana kawe, mambo ya ufundi kuzidiana ni jambo la kawaida sana na yeye alijua amezidiwa hivyo akataka kupata kitu ambacho yeye hakifahamu lakini katika kumbana bana ndipo jamaa akamuelekeza apitia kwenye blog hii ili apate ufafanuzi zaidi kwakuwa ndiye yeye maana yake ndiye mimi...
Kwa bahati baada ya kupitia humu akaona kuna utofauti mmoja wapo ni namba ya simu ndipo alipoona bora kunipigia kuendeleza yale maongezi lakini ikawa kama tunaanza upya hivi... ndipo akanieleza yoote..
UKWELI NI:- Sihusiki na chochote kuhusu huduma hii ya kuingiza channel za Azam tv na DStv kwenye king'amuzi cha Startimes wala kuingiza channel za king'amuzi DStv kwenye Azam tv..
Hakuna huduma hii kama ambavyo wanatoa matangazo wahusika, asilimia 100 unaibiwa, ukituma pesa
UMEIBIWA.
Wizi - Ikitokea imegundulika na DStv, Azam tv ama StarTimes unakamatwa wewe uliyewekewa ama unataka kuwekewa na yule muwekaji wa hizo channel. Wahusika wanaojitangaza wanatoa huduma hizi wanajua na ndo maana hawasemi wanapatikana wapi badala yake wanajifanya kumaliza kila kitu kwenye simu..
+255789476655
Insta @mustaphamadish