Call / WhatsApp +255673378129

Jun 20, 2011

TUSIUCHUKULIE POA UKIMWI..!!


 Kwa mtazamo wangu kutokana na research ndogo niliyoifanya inaonyesha kwa sasa swala la gonjwa la ukimwi si kama ilivyokuwa kama miaka ya nyuma na kadri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kuchukulia poa na kuona kama  mtu kuugua mafua na maisha kuendelea kama kawa..!!
Nimetumia neno kuchukulia poa kwasababu katika watu ambao nawakusudia zaidi ni vijana ijapokuwa wote nataka twende sawa ila kwa vijana ni too much..!!
Leo hii NGONO imekuwa ndio inawatumikisha sana watu,utakuta watu wapo bize sana kwa ajili ya kufanya NGONO.wanatafuta pesa,wanaongopa,wanatumia muda mwingi sana na kufanya kila linalowezekana ili tu mwisho wa siku wafanikishe kufanya NGONO.
Siku hizi idadi ya walio wengi wanapenda sana ngono na upendo wa dhati unakuja baada ya kufanya ngono na hii inasababisha idadi ya wanaooa/kuolewa hupungua kila kukicha maana inakuwa ngumu kudumu kwa kutokupata kile ambacho either alikitegemea kabla ama alitaka tu kuona kiundani inakuwa aje..?
Mapenzi yanadumu miezi kadhaa tu then wanaachana ama mtu mmoja anakuwa na zaidi ya mpenzi mmoja na ndo pabaya sana hapa..
Unayemuamini ana wapenzi wawili nawe ukiwa wa tatu,hapo hapo nawe unakiacha unayemuamini unao wengine wa kuzugia pengine watatu,inaweza ikawa mpenzi wako unayemuamini hayuko poa kifedha hivyo kuna wa kukununulia vocha na matumizi mengine huku ukiwalipa kwa penzi lako lakini huna future nao,uliye na future nae ndiye huyo mwenye wapenzi wawili wewe ukiwa wa tatu na yaweza kuwa mmoja tu kati ya hao ndo unatumia kinga tena pia pengine siku za mwanzo mwanzo tu na mkishazoeana inakuwa mpango....!!
Hapa UKIMWI utatukosa ??
Kama ulikuwa hujui automatically kama utamsaliti mpenzi wako jua ya kuwa nawe atakusaliti ama anakusaliti...!!
Jamani,jamani UKIMWI upo tusijisahaulishe kama vipi tuwe na mmoja na yakishindikana hayo TUVAE..!!
Ni hayo tu kwa leo toka kwangu kuja kwenu.
Mustapha E. Hanya
Share:

Jun 17, 2011

CHANNEL ZINAZOPATIKANA EASY TV..!!

Ntawaletea idadi ya channel zote zinazopatikana kwenye ving'amuzi kutokana na maombi yenu ili muweze kuelewa na kufanya maamuzi yaliyo sahihi na leo hii naanza na EASY TV.
EASY TV ina jumla ya channels 32 ila zinazoonyesha ni 30 tu.
Movie 1
Movie 2
Movie3
Movie Arabic
Aljazeerah
CNN
BBC
CCTV4
UBC
Citizen
TBC 1
Star TV
Channel 10
Capital
EATV
TVZ
ITV
Clouds TV
EWTN/TV Tumaini
Mliman TV
Emmanuel TV
Peace TV
Channel V
Xing kong
Ph'x China
JSC document
JSC sport
MTV
Child
Ila kiukweli mfumo wa ving'amuzi wanaujua wenyewe maana channel wanazouza nyingi ni za FREE TO AIR hivyo satellite husika wakihama channel inapotea,hivyo mpaka baada muda ndipo wanairejesha na pengine isilejee tena..!!
Pia wanaweza kuongeza channel pale wanapoona channel ipo ipo tu na inafaa kutazamwa na watanzania wanaibandika..!!
Kwenye easy tv nimemalizia hapa next time ntahamia kwenye STAR TIMES na ntamalizia na TING ni hayo tu kwa leo n nawatakia week end njema wadau..!!

Share:

Jun 6, 2011

Transit Motel Airport

 Baada ya kusababisha Transit Motel ya ukonga kazi ikahamia Transi Motel ya air port na kazi ikawa ni moja tu kufanya TV zionyeshe kwa uzuri ili mteja aweze kidhi haja yake kwa kile anachotaka kukiona..!!

Nikaanza ingia chumba mpaka chumba na hiki ni chumba kimojawapo kati ya vyote vizuri vilivyopo..!!

 Mpaka hapa nikapita,wanapaita RECEPTION kwa niliowaacha ni mapokezi huwezi ingia mpaka upitia hapa


Hapo tayari kwa matumizi ya wageni kama si wenyeji ili maisha yaendelee huku ukiangalia TV ikiwa clear kabisa,ukipuliziwa na AC na pia ukitaka chakula ama kinywaji chochote unapiga tu simu unaletewa chumbani kama hautahitaji kutoka nje..!!
Nami nikachukua kila kilichochangu mwendo nikachapa..!!



Share:

May 31, 2011

TRANSIT MOTEL Ukonga kama kawa kama dawa...!!


 Ilinichukua siku mbili kufanya nilichofanya na kuacha TV za vyumba vyote zikiwa clear kabisa..!!
Inaitwa TRANSIT MOTEL hii ipo ukonga pale njia panda ya kwenda segerea..!!
 Hiki ni chumba kimojawapo kati ya vyote nilivyopita pita na kuacha TV za vyumba vyote vikiwa clear kabisa


Hapa ndipo mapokezi ukifika hapa lugha ambayo utakutana nayo ukiambiwa vyumba vimejaa utajilaumu sana,maana ni mapokezi mazuri na ukarimu ndani yake..!!
Napo kuna TV hivyo nayo pia nikaiweka clear kabisa..!!


 Mito ipo miwili inamaana ukiwa na mwenzako ndo mpango zaidi ila hata ukila alone TV yako itakuburudisha na kukufanya ukajisia uko home..!!

 Hapa ndipo kwenye mlango wa kuingilia...!!!
Imetulia kimuonekano na hata huduma zao na kila chumba kina AC,TV,SIMU vyumba vyote ni self na kama unausafiri utapark ndani ya geti zaidi ya yote bei zao ni kama buree..!!
Tarehe 31 yangu ya leo nimeimalizia hukooo...!!
Share:

May 29, 2011

TUNAUZA | TUNAFUNGA | TUNATOA USHAURI | VING'AMUZI

DISH NA VING'AMUZI AINA ZOTE.
PIGA:+255714973797
Share:

FLAT SCREEN NA TV BRACKET..!!

Mwezi huu tunaumalizia huku kukujuza umuhimu wa flat screen na tv bracket,pengine waweza ikawa wewe ni mmojawapo kati ya wale wanaoshangaa inakuwaje tv inaganda ukutani..!!
Tv inafungwa ukutani kwa kutumia tv bracket,tv bracket inakamata ukuta kwa kudrill na tv husika kwa kufunga na bolt,hii inakuwa salama kwa wezi,watoto ama hata nafasi haichukui nafasi kubwa na inaleta muonekano mzuri..!!
Hapa imeshafungwa ukutani.

Pia waweza kufunga kwenye sehemu kama hii.

Inategemea na utakavyo.


Pia unaweza kuigeuza kwa jinsi unavyotaka.
Hii inaitwa tv bracket.

 Hapa imeshafungwa ukutani bado kupachika tv.

Kiukweli ni nzuri na ya kupendeza iwe nyumbani,ofisini,hotelini na popote pale,zaidi ya yote ni kwa usalama pia..!!
Share:

May 28, 2011

BAHARI LODGE nimesababisha..!!



Ilikuwa Alihamisi na Ijumaa nilikuwa pale maeneo ya Bahari beach,wenyewe wanapaita njia panda ya kwenda bahari beach hotel dar es salaam,hapa kuna lodge moja ya kisasa safi sana inaitwa BAHARI LODGE..!!
Issue ilikuwa Local hazionyeshi kwa TV zote nami nilihitajika kusababisha hilo ili mmiliki na wateja waendelee kula bata kwa furaha kwa kupata walichokihitaji..!!

 Hii ni mojawapo ya room za hapa Bahari Lodge..!!
Ikawa zinapatikana Local channels zifuatazo:-
ITV
EATV
CAPITAL
TBC
TV TUMAINI
AGAPE
STAR TV
CHANNEL TEN
C2C.
Pia na DSTV kama ambavyo niliikuta,nami nikachukua kila kilicho changu na kushaa...!!


Share:

May 26, 2011

ARABISAT..!!

Jana nilikuwa maeneo fulani hivi wanapaita mwinyimkuu magomeni,hapa nilisababisha channels za kiarabu kama zijulikanazo ARABISAT kwenye dish ya c band ft6 na mzee alizipata channels hizi zifuatazo maana ndo mahitaji yake:-
JSC
Syrian TV
Southern Sudan
AD Alouta
Oman TV
Kuwait TV
Saudi TV
Qatar TV
Sharjah TV
Saud-Quran
Sudan TV
Saud-Sunnah
TVE-Internacional
Baada ya hpo nikamfungia na Antenna ya EUROMIND ili aweze kutumia king'amuzi na channels za Local kwenye TV bila kutumia king'amuzi.
Kisha tukasign out na crew yangu..!!
Share:

May 19, 2011

MWENDO NI ULE ULE...!!

 Wa nyumba hadi nyumba jengo hadi jengo ilihali dunia tunaileta nyumbani kwako ukiwa TV yako hata kama black n white utaifurahia...!!


Hapa ni maeneo ya sinza hapa nimeacha channel za gospel zikiendelea kama kawa ila usitishike na hiyo lebo ya DSTV ni dish tu,kutokana na ukweli kwamba dish zinaingiliana..!!

Share:

May 16, 2011

UNAILINDA VIPI DISH YAKO NA MVUA..??

 Ni jambo la kawaida mtu kulinda chake ili kidumu milele,hapa tunaweza kuona jambo ambalo watu wengi ambao wanamiliki madish wanapenda kulifanya kwa kuzuia mvua.....!!
Je wewe unalindaje dish lako...??




Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita