Wengi wanapenda kufunga DSTV huku local na channel nyengine zikiachwa kwa wapangaji wenyewe kama wanahitaji kutokana na ukweli kwamba wapangaji wengi wa Apartment si wenyeji wa Tanzania hivyo hawaoni umuhimu wa kuangalia channel za nyumbani wakiamini TBC inawatosha ambayo inapatikana kwenye DSTV.Ambacho kinafanyika tunainstall Dish 1 ama 2 mbili kwa apartment nzima,nikimaanisha nyumba zote za wapangaji wa humo kutakuwa na connection ya DSTV ambacho yeye anafanya ni kukunua DSTV decoder tu ambayo hata akihama anaweza kuhama nayo.Hii pia inafanya mazingira ya apartment husika kuwa nadhifu na muonekano mzuri kwa kupunguza wingi wa madish,njia hii inawezekana kwa channel za local ama nyengine pia inategemea na wapangaji husika ama mmiliki wa apartment.
Oct 7, 2010
C BAND SINGLE SOLUTION CABLE
Hiki ni kifaa ambacho kinauwezo wa kukabiliana na interfierence sehemu zilizo na minara mitambo mitambo nk.Pia kuna channel ambazo hazipatikani mpaka utumie Single solution cable c band LNB haijarishi kama kuna interfierence ama laa.
TOFAUTI YA RECEIVER NA DECODER
Decoder ni kifaa kinachopokea Channel ambazo zipo fixed kwa mfano DSTV,ni lazima ziwe zinalipiwa na kampuni husika,hii inamaana huwezi kupata bure labda wenyewe waamue hivyo ama upite wizi.
Receiver ni kifaa kinachopokea channel zote zilizopo kwenye satellite,haijarishi kama ni fixed ama zipo zipo tu,ila hii inategemea na muelekeo na setting husika ikizingatiwa freequence.Haina maana kwamba hata zile za kulipia utazipata bure,zipo ambazo utazipata kutokana na ukubwa wa dish na muelekeo na huwa sio zote.
Pia kuna Receiver zinazotumia smart card hivyo unaweza ukapata channel zote za kulipia mf: channel za DSTV unaweza ukapata bila kutumia decoder zao,kitakachokulazimu ni kununua smart card yao.