Kiukweli kila kukicha tunapoteza wakongwe katika fani,inasikitisha ila mwisho wa yote inakuwa hatuna jinsi kwa7bu tumezaliwa ni lazima tutakufa isipokuwa tunachogopa ni kutangulia tu....!!
Kifo cha DR REMMY kamwe hakitasahaulika na hakuna wa kuziba pengo lake,kila mtu atakumbuka kwa style yake ila kwangu mimi ni zaidi ya ambavyo wengi wanadhani...!!
Mimi ni kati ya wale watanzania wachache waliopata bahati ya kuzaliwa mjini tena ni maeneo ya sinza pale nyuma ya shule ya Mashujaa kiasi kwamba ukitoka tu nje unakutana na kanisa....!!
Hivyo nikisema hivyo wale ambao wanakumbukumbu nzuri watakumbuka enzi hizo yaani nyumba za hapo kulikuwa na muingilianowa watoto sana yaani hakukuwa na mipaka kwa jinsi tulivyoishi enzi hizo so watoto wa DR REMMY walikuwa home hawapungui nasi kwao kama kawa...!!
Ila tulikuja kuhama sinza mwaka 1993 ambapo ndo ukawepo umbali,kiukweli nimesikitishwa sana poleni sana wana wa familia ya DR REMMY na wapenzi wote wa mkongwe huyu ambaye alikuwa JEMBE.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,Ameen.