Call / WhatsApp +255673378129

Dec 19, 2010

DSTV OFFER IMEFANYA USIKU KUWA MCHANA...!!

Hapa ni maeneo ya sinza karibu na shule ya msingi GRACE,nyumbani kwa mdada mmoja hivi anafanyia kazi pale tigo mliman city,kutokana na ratiba kuwa ngumu katika kipindi cha offer ikatufanya tufike saa 12 jioni na kutulazimu tusababishe ili watu waone walicholipia na usiku ukatukutia hapo.......!!
Lakini pamoja na hayo mpaka kwenye saa mbili kasoro ikawa wanaume tunachapa mwendo na siku ikawa bulubulu kama zege halikulala maana ingeharibu ratiba ya kesho.....!! 

 Kutoboa matundu na drill ili kufunga stend ya Dish ya DSTV

 Hapa kutafuta signal ya DSTV

 Stend imekaa inavyotakiwa

 
 Hapa signal ya kutosha picha inaonekana


Finder inafanya kazi nyakati zote kutokana na mazingira nikiwa na maana ya kuwa hata usiku pasipokutumia taa yenyewe ina taa ambayo inaweza kujiteemea hata kwenye giza totoloo....!!
Share:

Dec 18, 2010

AV selector

Kuna TV nyingi ambazo zina AV moja ama mbili na mtumiaji akawa ana vya kuchomeka zaidi ya viwili.
Mf: ana DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na Game labda,hapo hapo TV yako ina AV moja ama mbili hivyo itakuwa inakulazimu kuchomoa na kuchomeka kila muda ambao unataka kuangalia kimojawapo kati ya hivyo,ambapo itakuwa usumbufu licha ya hivyo pia ile kuchomoa chomoa kila wakati AV cable ni rahisi kukatika.
Napenda kukujuza ambacho labda ulikuwa hukijui....!!
kuna kitu kinaitwa AV selector kazi yake ni kuunganisha vyote kwa wakati mmoja,nikiwa na maana ya kuwa kama ni DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na hata Game na vyote ukaona bila kuchomoa chomoa...!!


Kazi yako itakuwa ni kubadili kwa kubonyeza AV selector yenyewe kwa namba husika kwani katika kuchomeka kwako kutakuwa na namba kwa kila ambacho utachomeka kama DVD no.1,Receiver no.2 na vilivyobakia kwa mtindo huo huo hivyo itakuwa ukibonyeza namba 1 itaonyesha DVD,namba 2 Receiver na vyote kulingana na jinsi utakavyobadili.
Kuna AV selector ambazo zinatumia remote na zisizotumia,kuna za umeme na zisizotumia umeme,kuna kuanzia njia tatu na kuendelea.

Share:

Segerea ilikuwa pangu pa kavu....!!

Offer bado inaendelea nami nazidi kusababisha watu wafurahie maisha,nilikuwa maeneo maeneo wanapaita segerea ambapo nyuma ya nyumba hizi ndipo ilipo gereza la segerea.....!!
Hapa tatizo kubwa lilikuwa ni pa kufunga dish maana nyumba ilikuwa imejengwa kiaina yake,kwa kawaida ili dish likae kwa uzuri na usimwite fundi kila baada ya muda ni lazima tudrill ukutani lakini sometimes inakuwa haina jinsi kama ilivyo hapa na ndio tukaamua tufunge kwenye mbao ili tu mwenye yake aweze kuona kama yalivyo matakwa yake......!!
 Tumeangalia ubora wa mbao kama kweli unaweza kubeba dish na ndipo tukafunga maana unaweza ukafunga ile unaondoka tu unapigiwa simu ya kwamba dish lipo chini....!!









Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita