Call / WhatsApp +255673378129

Dec 29, 2010

Mbio za funga mwaka ndani ya bwaga moyo.....!!

Tunahesabu siku tu kuelekea mwaka mupya mupya kabisa 2011,huku tukiumalizia malizia mwaka huu 2010,ukiniacha na kumbukumbu nzuri ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa namba za kipekee ambazo kamwe hazitajirejea 10.10.10 maana nilizaliwa miaka kadhaa nyuma ikiwa ni tarehe 10 mwezi wa 10.
Tukiyaacha hayo leo nipo bwagamoyo na nadhani nitakuwepo huku mpaka kesho ama kesho kutwa na hakuna kilichonileta huku zaidi ya kazi na na7bisha kama kawa yangu.....!!
Share:

Dec 28, 2010

Kuelekea 2011 yapi mazuri na ya kupongeza 2010....!!

Kwa kuanza tu naweza nikasema kwa mwaka huu 2010 ni mwaka mgumu sana hasa kwa vijana,yananitoka haya kutokana na mazungumzo yao pale unapokaa nao,maana wenyewe wanakwambia hakuna njia kama milango inazidi kufungwa ili watu wasitoke,hivyo kipindi wao wanasema hivyo sijui wewe unasema aje kuhusu mwaka huu unaoishia.....!!
Upande wa kazi banaa jua halikuwa kali saana maana ushindani ulikuwepo ila si mkali sana ni wa kawaida tu,ilizaliwa kampuni inayojulikana kama star times ambayo kuna mkono wa TBC na wachina,ambao wamekuja tofauti kidogo,badala ya kutumia dish wao walitumia Antenna na decoder,ni kitu kizuri na watanzania wamekipokea ila si kama ambavyo walidhani hasa baada kufa GTV na kusemekana inakuja kampuni ambayo itakuwa inafanana na GTV ili kuleta ushindani na DSTV katika swala la mpira kuhusu malipo ya mwezi,sitaki kuelezea sana ila tukaitambua star time na utofauti wa kutumia antenna ila yenyewe si ya kwanza ilitangulia EASY TV ambayo mpaka sasa bado ipo na inafanya vizuri pia.
Pia ATN nao wametoa ving'amuzi vyao ikiwa hawana tofauti na star time ila wao wapo kidini zaidi na channel zao,hii ina maana kwamba kwa mwaka ujao 2011 kutakuwa na mapokezi ya vingamuzi vyengine toka kwa wamiliki wa makampuni ya habari Tanzania,ugomvi wa kibiashara ndio sababu ya kuwaumiza watanzania kwa kuwalazimisha kujaza decoder majumbani kwao.......!!
Star times ilitosha kabisa kukidhi mahitaji ya watanzania ijapokuwa Easy tv nao walikidhi ila sijui sababu ni nini mpaka wakatolewa maana na TBC kuamua kuanzisha ya kwao ambayo channel zote za Mengi hazipo,ikisemekana hawataungana maana wana ugomvi wa kibiashara,huku easy tv ikiwa na channel zote za local mpaka TVZ.....!!
Ni meengi sana kipindi tunaendelea kukumbuka lichukue hili...!!
Share:

Dec 26, 2010

Boxing day nime7babisha like this......!!!

Ikiwa ni siku 1 baada ya kusherehekea sikukuu ya x-mass,kilichofuata ni kupeana zawadi kwa kwenda mbele nami nina wangu wa kuwapa banaa...!!
Unadhani zawadi kwangu itakuwa ni nini kama si ku7bisha ili wengine wafurahie na familia zao na maisha yaweze kusonga mbele kama ilivyo ada ili kuutengeneza mchana na usiku,leo ni jumapili saafi kabisa nami nipo nafanya haya ambayo nimejaaliwa kufanya siku hii ya leo...!!
Unajua watu wanashindwa kuelewa kuna watu duniani wamezaliwa kwa ajili ya kuja kufurahisha watu wengine tu duniani nami nikiwa mmojawapo na kama hukulijua hilo ichukue hii na utembee nayo,ili siku ukipata bahati ya kukutana na mimi nawe uweze kufurahishwa pia....!!
Hii ni nyumba ya mtu,ambaye ana tv mbili sitting room na bed room na alitaka kuona picha clear kote kwa kutumia Satellite Dish Antenna na kila mtu kuangalia channel aipendayo kwa wakati mmoja bila kumuudhi mwengine,nami nika install FTA channel za Local na Gospel,Dish 1 ila Receiver 2,pia nikafanya Extra view upande wa DSTV na boxing day kwangu ikaishia hivii....!!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita