Call / WhatsApp +255673378129

Oct 7, 2010

TOFAUTI YA RECEIVER NA DECODER

Decoder ni kifaa kinachopokea Channel ambazo zipo fixed kwa mfano DSTV,ni lazima ziwe zinalipiwa na kampuni husika,hii inamaana huwezi kupata bure labda wenyewe waamue hivyo ama upite wizi.
 Receiver ni kifaa kinachopokea channel zote zilizopo kwenye satellite,haijarishi kama ni fixed ama zipo zipo tu,ila hii inategemea na muelekeo na setting husika ikizingatiwa freequence.Haina maana kwamba hata zile za kulipia utazipata bure,zipo ambazo utazipata kutokana na ukubwa wa dish na muelekeo na huwa sio zote.
Pia kuna Receiver zinazotumia smart card hivyo unaweza ukapata channel zote za kulipia mf: channel za DSTV unaweza ukapata bila kutumia decoder zao,kitakachokulazimu ni kununua smart card yao.
Share:

Baada kufa GTV...!!

Ni wazi kwamba ni watanzania wengi wameathirika na uyeyukaji wa GTV wamejikuta wamebakia na Decoder wasijue wazifanyie nini huku wengine wakijipa imani ya kuwa ipo siku watarejea....!!
Decoder ya GTV unaweza ukaitumia kwa kutumia dish lake lile lile unaweza ukaona channel zipatazo 13 FREE,ambazo ndani yake kuna kama MBC1,2,3 ambazo zinonyesha movie sometimes mpira ambao unakuwa live ila si mechi zote,wala ligi maalumu inakuwa wenyewe tu wakijisikia kufanya hivyo wanafanya.Ukiacha njia hiyo kuna jamaa yangu mmoja ambaye nakili kusema ya kuwa amenizidi ung'amuzi kiasi kwamba amefanikiwa kuflash GTV decoder na ikawa receiver ambayo inapokea channel yeyote kutokana na matakwa yako...!!
Dish la GTV pia unaweza ukatumia kwa DSTV ama channel za Gospel ama nyengine kwa sababu Dish haichagui Receiver ama Decoder ni ufundi wa fundi tu.
Share:

JUA USICHOKIJUA..........!!!

Kwa channel za nyumbani Tanzania si zote ambazo zinapatikana kwenye Satellite Dish Antenna,kwa sababu TV station nyengine wanatumia Transmeter kurusha matangazo yao hivyo channel yeyote ambayo inatumia Transmeter haipatikani kwenye Dish,nikiwa na maana ya kuwa itakulazimu utumie Antenna ya kawaida.
Zijue channel ambazo zinapatikana kwenye Satellite Dish Antenna:-
*ITV,EATV,CAPITAL
*STAR TV
*ATN
*TBC
*CHANNEL 10
NB:Hii ni kuanzia Satellite Dish Antenna inayoanzia futi 6 na kuendelea na LNB itumikayo ni C band.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita