Call / WhatsApp +255673378129

Dec 19, 2010

EURO MIND Antenna

Si wanainchi wote ambao wana uwezo wa kufunga Dish ama king'amuzi kutokana na hali ya maisha jinsi ilivyo na kwa upande wa pili pia si channel zote za nyumbani zinazopatikana kwenye Satellite Dish ama hata penye king'amuzi pia,hivyo swala la Antenna linabaki pale pale kwamba ni la muhimu si uwezo ijapokuwa linahusika pia.
Kwa wapatao tabu kuhusu Antenna ipi inaweza ikawasaidia kuona picha clear kutokana na eneo waishilo,jibu ni moja tu EURO MIND Antenna na ikitokea haishiki basi ujue eneo lako halistahili Antenna.
Kwa wale wenzangu na mimi wa uswazi kuna zile tube ambazo unazifanyia mambo na kuwa bonge la Antenna.
Share:

KU na minara dam dam....!!

 Lau ingelikuwa nainstall C band hakika ningekesha bila kuwa na single solution cable kwa kuwa kungekuwa na kitu kinaitwa interference maana uwapo mnara either wa simu ama mitambo mitambo Satellite Dish hasa C band linakuwa kama linakingwa hivi ama kupungua uwezo wake wa kukamata sawia satellite husika,baada ya wataalamu kulijua hilo wakatutengenezea kifaa ambacho kinaweza kuimili mikiki hiyo nayo ni SINGLE SOLUTION CABLE hii ni kwa Dish kubwa tu...!!
Kwa dish ndogo ni nadra sana kutokea interference hata kama kuna mnara mbele kama nilivyoinstall hiyo DSTV maeneo ya Afri center na mambo yakawa swaafiii...!!!
Ukienda mbali zaidi zipo lnb za dish ndogo ambazo nazo kazi yake ni kukabiliana na interference....!!
Share:

DSTV OFFER IMEFANYA USIKU KUWA MCHANA...!!

Hapa ni maeneo ya sinza karibu na shule ya msingi GRACE,nyumbani kwa mdada mmoja hivi anafanyia kazi pale tigo mliman city,kutokana na ratiba kuwa ngumu katika kipindi cha offer ikatufanya tufike saa 12 jioni na kutulazimu tusababishe ili watu waone walicholipia na usiku ukatukutia hapo.......!!
Lakini pamoja na hayo mpaka kwenye saa mbili kasoro ikawa wanaume tunachapa mwendo na siku ikawa bulubulu kama zege halikulala maana ingeharibu ratiba ya kesho.....!! 

 Kutoboa matundu na drill ili kufunga stend ya Dish ya DSTV

 Hapa kutafuta signal ya DSTV

 Stend imekaa inavyotakiwa

 
 Hapa signal ya kutosha picha inaonekana


Finder inafanya kazi nyakati zote kutokana na mazingira nikiwa na maana ya kuwa hata usiku pasipokutumia taa yenyewe ina taa ambayo inaweza kujiteemea hata kwenye giza totoloo....!!
Share:

Dec 18, 2010

AV selector

Kuna TV nyingi ambazo zina AV moja ama mbili na mtumiaji akawa ana vya kuchomeka zaidi ya viwili.
Mf: ana DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na Game labda,hapo hapo TV yako ina AV moja ama mbili hivyo itakuwa inakulazimu kuchomoa na kuchomeka kila muda ambao unataka kuangalia kimojawapo kati ya hivyo,ambapo itakuwa usumbufu licha ya hivyo pia ile kuchomoa chomoa kila wakati AV cable ni rahisi kukatika.
Napenda kukujuza ambacho labda ulikuwa hukijui....!!
kuna kitu kinaitwa AV selector kazi yake ni kuunganisha vyote kwa wakati mmoja,nikiwa na maana ya kuwa kama ni DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na hata Game na vyote ukaona bila kuchomoa chomoa...!!


Kazi yako itakuwa ni kubadili kwa kubonyeza AV selector yenyewe kwa namba husika kwani katika kuchomeka kwako kutakuwa na namba kwa kila ambacho utachomeka kama DVD no.1,Receiver no.2 na vilivyobakia kwa mtindo huo huo hivyo itakuwa ukibonyeza namba 1 itaonyesha DVD,namba 2 Receiver na vyote kulingana na jinsi utakavyobadili.
Kuna AV selector ambazo zinatumia remote na zisizotumia,kuna za umeme na zisizotumia umeme,kuna kuanzia njia tatu na kuendelea.

Share:

Segerea ilikuwa pangu pa kavu....!!

Offer bado inaendelea nami nazidi kusababisha watu wafurahie maisha,nilikuwa maeneo maeneo wanapaita segerea ambapo nyuma ya nyumba hizi ndipo ilipo gereza la segerea.....!!
Hapa tatizo kubwa lilikuwa ni pa kufunga dish maana nyumba ilikuwa imejengwa kiaina yake,kwa kawaida ili dish likae kwa uzuri na usimwite fundi kila baada ya muda ni lazima tudrill ukutani lakini sometimes inakuwa haina jinsi kama ilivyo hapa na ndio tukaamua tufunge kwenye mbao ili tu mwenye yake aweze kuona kama yalivyo matakwa yake......!!
 Tumeangalia ubora wa mbao kama kweli unaweza kubeba dish na ndipo tukafunga maana unaweza ukafunga ile unaondoka tu unapigiwa simu ya kwamba dish lipo chini....!!









Share:

Dec 17, 2010

IZUNGUKE DUNIA UKIWA NA TV YAKO NYUMBANI.......!!

Unaweza kuona channel ya taifa lolote ambayo ipo katika satellite katika ukanda huu wa Africa mashariki,tunakuwezesha kupata kujua na kuona kila kinachoendelea up to date kana kwamba upo nchi husika,tunakufanya usiichoke TV yako zaidi ya yote utamani kuibeba ba kutembea nayo popote uendapo...!!
Kuwa wa kwanza kupata habari kwa kuangalia vituo vya kimataifa vya habari na utaweza kuburudika na kujifunza zaidi kwa channel za ndani na za nje clear bila chenga....!!


Share:

Dec 13, 2010

Buriani DR REMMY..........!!!

Kiukweli kila kukicha tunapoteza wakongwe katika fani,inasikitisha ila mwisho wa yote inakuwa hatuna jinsi kwa7bu tumezaliwa ni lazima tutakufa isipokuwa tunachogopa ni kutangulia tu....!!
Kifo cha DR REMMY kamwe hakitasahaulika na hakuna wa kuziba pengo lake,kila mtu atakumbuka kwa style yake ila kwangu mimi ni zaidi ya ambavyo wengi wanadhani...!!
Mimi ni kati ya wale watanzania wachache waliopata bahati ya kuzaliwa mjini tena ni maeneo ya sinza pale nyuma ya shule ya Mashujaa kiasi kwamba ukitoka tu nje unakutana na kanisa....!!
Hivyo nikisema hivyo wale ambao wanakumbukumbu nzuri watakumbuka enzi hizo yaani nyumba za hapo kulikuwa na muingilianowa watoto sana yaani hakukuwa na mipaka kwa jinsi tulivyoishi enzi hizo so watoto wa DR REMMY walikuwa home hawapungui nasi kwao kama kawa...!!
Ila tulikuja kuhama sinza mwaka 1993 ambapo ndo ukawepo umbali,kiukweli nimesikitishwa sana poleni sana wana wa familia ya DR REMMY na wapenzi wote wa mkongwe huyu ambaye alikuwa JEMBE.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,Ameen.
Share:

Dec 12, 2010

c channel zote zinazopatikana kwenye Dish

Swali ambalo daily nakutana nalo kwa kila ninapoinstall Dish hasa kwenye makazi ya watu....!!
Unafunga dish ndogo channel za Emanuel gospel mtu anaulizia local zinapatikana ngapi...??
Unafunga futi sita local mtu asipoiona C2C anahoji kunani...??
Hivyo ni vema ukajua unachotaka na utakachopata kabla hujahudumiwa....!!
Nimegundua ya kuwa wateja design hii ni wale ambao wameenda nyumba ya fulani kaona channel fulani nae wakati anataka huduma anataja ile channel aliyoipenda na kuiona bila hata kujua zimefungwa dish ngapi nje,na ndo maana tunaamua kutoa darasa kabla ya kumuhudumia mteja nawe kuwa huru kuuliza...!!
Share:

Week end ndo inaishia hivyo...!!

Muda huu ndo week end inaishia kwangu mimi ila najua kwa wengine ndo kwanza wanaamka sasa na kutafuta pa kwenda,ila kiukweli kila mtu na starehe yake............!!!
Leo nilikuwa sehemu 1 wanapaita mbezi salasala nika7babisha watu waone DSTV then nikajirejesha home na ndo nipo mpaka sasa natuma post hii....
maana yake sina mpango wa kutoka tena kwenda popote najiandaa kuianza Monday.....!!

Share:

Dec 10, 2010

ROYAL PUB....!!

Kiukweli mimi sio mpenzi wa mpira ila afanyae vizuri stahili zake pongezi,leo nilikuwa hapa Royal pub ambapo nilifunga DSTV pamoja na projecter si leo ni muda sasa ila leo nilikuwa hapa kuhakikisha mpira wa leo unaonekana vema pasipo kutokea tatizo lolote na ndicho kilichotokea watanzania wameangalia vema jinsi time ya Tanzania iilivyoichakaza Uganda....!!
Bao lilopatikana kwa njia ya penati,ambapo Juma kaseja ameweza kudaka penati 1 huku kipa wa timu ya uganda kutoambulia hata penati 1...
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita