Call / WhatsApp +255673378129

May 16, 2011

UNAILINDA VIPI DISH YAKO NA MVUA..??

 Ni jambo la kawaida mtu kulinda chake ili kidumu milele,hapa tunaweza kuona jambo ambalo watu wengi ambao wanamiliki madish wanapenda kulifanya kwa kuzuia mvua.....!!
Je wewe unalindaje dish lako...??




Share:

TUHESHIMIANE JAMANI....!!!

 Ni kawaida ya kuwa mtu ukifunga dish lazima nyumba iwe na hadhi fulani hivi ila kwa hapa tutaenda sawa tu ukiambiwa uishi upendavyo huku machannel ya kitu cha Dish yakipatikana kama hivyooo uonavyo....!!
 

Share:

May 14, 2011

Hakuna kinachoshindikana...!!

Share:

May 11, 2011

Mwanaume anasifiwa kazi...!!

Matembezi kwetu ni kama kawaida,hapa tumerejea tena kwa mdada mmoja hivi yupo maeneo ya Mbezi sala sala n mambo yakawa mswano,kana kwamba tunabomoa kumbe ndivyo twatengeneza...!!

Hii ni twin KU lnb kwa ajili ya channel za Gospel.


 Hii ni twin KU na twin C BAND,maana yake utapata channel za Local na Gospel na hiyo dish ndogo ni kwa ajili ya DSTV.

Share:

May 10, 2011

Nyumbani kwangu pia...!!

Icje ikawa ikawa kama fundi nanii yeye anatengenezea wenzie vitanda hali ya kuwa yeye analala chini...!!


Hii ni dish ya DSTV na hapa ni nyumbani kwangu ambapo napata usingizi,hivyo nami maisha yanaendelea kama ambao nawafungia hayo madish..!!
Share:

May 8, 2011

WEEK END KWETU HAINA TOFAUTI NA MONDAY..!!









Week end kwetu ni kama Monday vile maana mbio ndizo zilezile,7bu tupo kwa ajili ya kuwafurahisha wengine,huku yetu yakituendea vema...!!
Hapa ni katika J2 ya leo maeneo ya kulasini nishauza hapo na sasa naelekea sehemu moja wanapaita Tabata pale maeneo ya swiz pub...!!
Share:

May 7, 2011

WENYE KUMBI ZA KUONYESHA MPIRA KUPITIA DSTV IMEKULA KWAO...!!!


 Ni kilio cha watanzania wengi pande mbili kwa wakati mmoja,namaanisha kwa wale wapenzi wa mpira ligi za nje na wale wamiliki kumbi hizo...!!
MULTICHOICE TANZANIA ( DSTV ) kwa sasa ipo katika operations ya kuwafungia wale wote ambao walinunua DSTV kwa matumizi binafsi matokeo yake wakaenda kufanyia biashara kwa kutoza watu kiingilio na kufanya idadi ya wamiliki kumbi za kuonyesha mpira kuongezeka kila kukicha,huku idadi ya wateja wa kawaida kupungua kutokana na wengi kuangalia kupitia kumbi za mpira hizo....!!
Wapo ambao lishawakumba hili na kama wewe bado yakupasa ujiandae kwani wapo njiani,labda itangua ngumu kwa wale wenzangu namie walio ndani ndani,huku mafundi wao wakiwalinda maana ndo watoa taarifa wa kwanza...!!
Je hii ni kweli itaongeza wateja maana hakutakuwa na kumbi za mpira na kuwalazimu wapenzi wa mpira kufunga DSTV majumbani mwao...!!
Share:

May 6, 2011

NIPO KWENYE RESEACH ZAIDI....!!!

 
Kila kukicha yanazaliwa mapya nami naumiza kichwa kwenda sawa katika ukanda wangu huu....!!
Mfano leo Tanzania yetu imekuwa na mfumuko wa ving'amuzi na kufanya pia ufungaji wa madish kupunua ila mwisho wa siku bado dish linskuwa dish na king'amuzi kinabaki kuwa king'amuzi....!!
Ambacho wengi hawajui hata hayo makampuni yenye kuuza vinga'amuzi wanatumia Satellite Dish kukamata hizo channel zote zinazoonekana kwenye ving'amuzi vyenu..!!!
Hii inathibitisha ya kuwa still Dish itakuwa juu na ving'amuzi kufuata..!!
Ila kwa upande wangu nipo kwenye reseach ya kutaka kujua channel zote zilizopo kwenye Satellite ulimwenguni ambazo zinapatikana Africa pia zile zinazotumika na makampuni na kufungwa na kuwa za kulipia....!!
Lengo ni kupanua uwezo wangu katika fani hii na nashukuru mungu nimepata speed ambapo nimefanikiwa kwa kiasi fulani....!!
Share:

May 5, 2011

EWTN yanayoendelea Vatican city...!!


Hii ni Channel inapatikana kwenye C BAND ila sijaifanyia utafiti kama kwenye KU BAND kama inapatikana pia,ni ya dini ya wakristo na kwasasa kuna mambo yanaendelea kule Vatican city kuapishwa nadhani kwa viongozi wao...!!
Jana nilikuwa Bagamoyo pale maeneo ya Zinga kwenye kituo cha masister mahitaji yao ilikuwa ni channel ya EWTN pekee ili waone hayo yanayoendelea huko Vatican city..!!
Awali walikuwa tayari wana Dish ya c band ambayo walikuwa wanaona Local channel na za Gospel,hivyo nikawaongezea LNB ya c band na kusababisha Vatican city kuhamia Bagamoyo kwenye kituo cha masister...!!
  Kwangu ikawa mwazo mzuri kuinstall EWTN pekee kwani mpaka sasa nimepokea order zaidi ya nne kuhusu channel hiyo ambapo week end ntakuwa mzigoni kusababisha EWTN kuhamia majumbani mwa mwatu...!!
Share:

May 3, 2011

HOTEL INSTALLATIONS INAKUWA ILIVYOKUWA...!!

Hii inaitwa Multiswitch na mara nyingi hutumika mahotelini ama kwenye Apartment au hata kwenye nyumba binafsi,ila kazi yake ni kugawa Receiver zaidi ya moja kama uonavyo hapo,hizo cable zote zimeingia kwenye receiver....!!
Share:

Hapa hakuna kinachoonekana kamwe....!!

Satellite Dish ya aina yeyote ukiiona imezibwa hivi jua ya kuwa hakuna kinachoonekana kwenye TV,kwa sababu tunaposet huwa tunalenga kwenye Satellite husika hivyo lazima kuwe na mawasiliano baina ya Dish na Satellite kwa mtindo wa kulenga,hivyo ikizibwa maana yake ni kukata mawasiliano baina ya Dish na Satellite,labda niwape faida wenye madish woote kama ukiona Dish lako halionyeshi la kwanza kufanya ni kuliangalia Dish lako je halijazibwa..?? pili angalia cable haijachomoka..?? vyote vikiwa sawa ndo unapaswa kumwita fundi kwani zaidi ya hapo kutakuwa na issue ya kiufundi zaidi..!!
Share:

May 1, 2011

KOTA ZA BANDARI ILIKUWA BWAAA...!!

 
Ufundi banaa huzidiana yaani kama ubabe...!!
Mbabe wako ndo mnyonge wangu n hilo halina ubishi na ndivyo ilivyotokea hapa..!!
Jamaa alipewa issue ya kuhamisha Dish toka maeneo ya K'koo na kuhamishia Kulasini katika kota za Bandari,Dish ilikuwa ni ya c band zile kuuubwa wenyewe walikuwa wanaangalia Local channel...!!
Ilimchukua siku tatu kucheza nayo lakini wapi wazungu walikataa,ikamlazi jamaa kunitafuta baada ya kukubali matokeo ya kuwa usipokubali kushindwa c mshindani,nami tena kama nimezaliwa nayo hayo madude nikafika eneo la tukio nikasababisha watu wachekecheke na TV yao kisha nikachukua kila kilicho changu bila kusahau nimetumwa pesa kisha nikachapa mwendo...!!
Share:

HOUSE'S TOO CHEAP FOR SALE AT MBEZI LUIS..!!

NYUMBA INAUZWA MBEZI LUIS KWA FUNGO MIL.45
 

Muonekano kwa nje.





   Kwa uwani ndani ya uzio.                                                Kwa nje kupitia getini.   











                   Kwa uwani ndani ya uzio.


 Kwa uwani ndani ya uzio.

Ipo maeneo ya Mbezi luis kwa fungo,unaingia ndani kidogo toka Morogoro rd.Nyumba ni self-3 bed rooms,kitchen,toilet,store,sitting room na ina vyumba vya uwani v3,choo cha nje,pia inauwanja mkubwa wa kujenga nyumba kubwa uliozungushiwa ukuta na parking ya magari ndani ya gate.
Umeme ni LUKU.
Bei ya kuuza ni mil 45.Mazungumzo yapo hapo tutakapokutana na mnunuzi.
 Kwa maelezo zaidi piga simu no.+255659937711/+255763973797 au tuwasiliane  kwa
email: mustaphamadish@gmail.com
                      
                                                                                                                                                     

PLOT FOR SALE AT BAGAMOYO MJINI MIL.3 
Kiwanja kinauzwa kipo maeneo ya Bagamoyo maeneo ya nia njema karibu na shule ya msingi nia njema.Ukubwa wa kiwanja ni robo heka.Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa no. +255659937711

                                                                                                                                                      
  
PLOT FOR SALE AT BAGAMOYO MJINI MIL.3
Kiwanja kinauzwa kipo maeneo ya Bagamoyo kidongo chekundu.Ukubwa wa kiwanja ni robo heka.Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa no.+255659937711

                                                                                                                                                       

HOUSE FOR SALE AT MAGOMENI MAPIPA MIL.250.
Nyumba inauzwa ipo maeneo ya Magomeni mapipa mtaa Idrisa ni muundo wa National housing,ina vyumba 6 ndani,vyumba vitatu vya uwani,jiko,choo na store.Kwa maelezo zaidi piga simu no.+255659937711
Share:

Nawatakia sikukuu njema wajenga nchi wenzangu !

Leo ni tarehere 1 mwezi wa 5,kila tarehe hii imekuwa tunasherehekea sikukuu ya wafanyakazi,lengo na madhumuni ni kuthamini uwepo wa wafanyakazi na kukutana pamoja kuonyesha na kuzunguza ambayo yanaweza yakatupa changamoto wafanyakazi wa kila idara,huu ni mtazamo wangu kwa upeo wangu mdogo nilionao juu ya siku hii ya leo,pengine wewe unajua zaidi ya hii...!!
Hivyo popote mlipo nawatakia sikukuu njema watanzania wenzangu na msio watanzania pia maana lengo ni kujenga nchi huku mkono ukienda kinywani na maisha yakiendelea.
Kwa mwaka huu imefanyika kitaifa Morogoro mgeni rasmi akiwa mkuu wa nchi,binafsi napenda kuchukua nafasi hii kuwahusia vijana wenzangu kufanya kazi kwa bidii huku tukikumbuka ya kuwa "CHEZA NA MSHAHARA NA SI KUCHEZA NA KAZI" maisha mazuri hayaji kiurahisi yatupasa kufanyakazi kwa bidii sana na mliopo shule msome kweli maana kadri siku zinavyozidi kwenda maisha yanazidi kuwa magumu.
Ni hayo tu kwa leo wajameni....!!!
Share:

Apr 9, 2011

CARs FOR SALE....!!!

 Starlet Mil.4,500,000

 Noah Mil.13,500,000

 Vitz Mil.6,500,000

 Spacio Mil.8,600,000

GX110 Mil.13,500,000

For more informations call us +255659937711,mustaphamadish@gmailcom.
Pia tuna gari aina mbali mbali.
Share:

Mar 15, 2011

DISH INAPOTUMIKA NA WAJENZI....!!

Hilo hapo chini ni Dish Antenna aina ya c band,unaweza ukasema pengine anashughulika ili watu waone picha but c kama udhaniavyo...!!




Mimi niliishia hapa ila kilichoendelea nadhani hata wewe mwenyewe unapata picha...!!
Share:

Feb 3, 2011

AJALI WAJAMENI...!!

Kilichotokea hapa hakuna anayejua,hii nimeipata katika pita pita zangu mtandaoni lakini dah..!!
hapa inavyoonyesha jamaa hakuweza hata kutumia kama paa matokeo yake alienda kupima kule kwenye vyuma chakavu..!! 
Share:

Jan 20, 2011

Poleni sana wadau....!!

Baada ya mbio za mbali na nyumbani sasa nimerejea kama kawaida...!!
Huku nikiwa nimeona na kujifunza meengi,kiukweli nimeongeza vitu vingi kwa muda mchache ambapo awali nilikuwa sina mawazo hayo,naomba niishie hapa najipanga ili tuweze kushea kile ambacho nimepata.....!!!
Zaidi ya yote samahani wale wote waliokuwa wanapata usumbufu jinsi ya kunipata ila email ni nyingi sana lakini zote nitazijibu wala msijali...!!
Share:

Jan 10, 2011

nimewamiss sana wajameni...!!

ebwana dah....!!
Kitambo kidogo sipatikani hewani kwa no.za tz huku wengi nikiwapa shida jinsi ya kunipata na lawama zikiwa zimejaa gunia..!!
Nipo sehemu ambayo ni nadra sana kukutana na mtu mwenye ngozi kama yangu nyeusi,pia kiswahili ndicho hakisikiki kabisaaa...!!
Ila ni mbio tu i wish nitakuwa home soon banaa....!!
Share:

Dec 29, 2010

Mbio za funga mwaka ndani ya bwaga moyo.....!!

Tunahesabu siku tu kuelekea mwaka mupya mupya kabisa 2011,huku tukiumalizia malizia mwaka huu 2010,ukiniacha na kumbukumbu nzuri ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa namba za kipekee ambazo kamwe hazitajirejea 10.10.10 maana nilizaliwa miaka kadhaa nyuma ikiwa ni tarehe 10 mwezi wa 10.
Tukiyaacha hayo leo nipo bwagamoyo na nadhani nitakuwepo huku mpaka kesho ama kesho kutwa na hakuna kilichonileta huku zaidi ya kazi na na7bisha kama kawa yangu.....!!
Share:

Dec 28, 2010

Kuelekea 2011 yapi mazuri na ya kupongeza 2010....!!

Kwa kuanza tu naweza nikasema kwa mwaka huu 2010 ni mwaka mgumu sana hasa kwa vijana,yananitoka haya kutokana na mazungumzo yao pale unapokaa nao,maana wenyewe wanakwambia hakuna njia kama milango inazidi kufungwa ili watu wasitoke,hivyo kipindi wao wanasema hivyo sijui wewe unasema aje kuhusu mwaka huu unaoishia.....!!
Upande wa kazi banaa jua halikuwa kali saana maana ushindani ulikuwepo ila si mkali sana ni wa kawaida tu,ilizaliwa kampuni inayojulikana kama star times ambayo kuna mkono wa TBC na wachina,ambao wamekuja tofauti kidogo,badala ya kutumia dish wao walitumia Antenna na decoder,ni kitu kizuri na watanzania wamekipokea ila si kama ambavyo walidhani hasa baada kufa GTV na kusemekana inakuja kampuni ambayo itakuwa inafanana na GTV ili kuleta ushindani na DSTV katika swala la mpira kuhusu malipo ya mwezi,sitaki kuelezea sana ila tukaitambua star time na utofauti wa kutumia antenna ila yenyewe si ya kwanza ilitangulia EASY TV ambayo mpaka sasa bado ipo na inafanya vizuri pia.
Pia ATN nao wametoa ving'amuzi vyao ikiwa hawana tofauti na star time ila wao wapo kidini zaidi na channel zao,hii ina maana kwamba kwa mwaka ujao 2011 kutakuwa na mapokezi ya vingamuzi vyengine toka kwa wamiliki wa makampuni ya habari Tanzania,ugomvi wa kibiashara ndio sababu ya kuwaumiza watanzania kwa kuwalazimisha kujaza decoder majumbani kwao.......!!
Star times ilitosha kabisa kukidhi mahitaji ya watanzania ijapokuwa Easy tv nao walikidhi ila sijui sababu ni nini mpaka wakatolewa maana na TBC kuamua kuanzisha ya kwao ambayo channel zote za Mengi hazipo,ikisemekana hawataungana maana wana ugomvi wa kibiashara,huku easy tv ikiwa na channel zote za local mpaka TVZ.....!!
Ni meengi sana kipindi tunaendelea kukumbuka lichukue hili...!!
Share:

Dec 26, 2010

Boxing day nime7babisha like this......!!!

Ikiwa ni siku 1 baada ya kusherehekea sikukuu ya x-mass,kilichofuata ni kupeana zawadi kwa kwenda mbele nami nina wangu wa kuwapa banaa...!!
Unadhani zawadi kwangu itakuwa ni nini kama si ku7bisha ili wengine wafurahie na familia zao na maisha yaweze kusonga mbele kama ilivyo ada ili kuutengeneza mchana na usiku,leo ni jumapili saafi kabisa nami nipo nafanya haya ambayo nimejaaliwa kufanya siku hii ya leo...!!
Unajua watu wanashindwa kuelewa kuna watu duniani wamezaliwa kwa ajili ya kuja kufurahisha watu wengine tu duniani nami nikiwa mmojawapo na kama hukulijua hilo ichukue hii na utembee nayo,ili siku ukipata bahati ya kukutana na mimi nawe uweze kufurahishwa pia....!!
Hii ni nyumba ya mtu,ambaye ana tv mbili sitting room na bed room na alitaka kuona picha clear kote kwa kutumia Satellite Dish Antenna na kila mtu kuangalia channel aipendayo kwa wakati mmoja bila kumuudhi mwengine,nami nika install FTA channel za Local na Gospel,Dish 1 ila Receiver 2,pia nikafanya Extra view upande wa DSTV na boxing day kwangu ikaishia hivii....!!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita