Call / WhatsApp +255673378129

Jan 10, 2012

LOCAL CHANNELS ZATULIA KWENYE FUTI 6!!


Baada ya kusumbua muda mrefu hatimae Channels za Tanzania zote zilizopo kwenye Satellite zatulia!
Tatizo ilikuwa kama zinatulia za V za H zitasumbua na Zikitulia za H za V zitasumbua,tatizo hili huwa linatokea mara kwa mara na wala sitaki kuamimni kama ndio limeshakuwa limefika kikomo kwa ushauri tu ikiwa unataka Local channels kupitia Dish ukinunua la futi 8 itakuwa unapata uhakika wa kile ukitakacho kwasababu hata zikiwa zinasumbua kwenye futi 8 unaendelea kula raha!!
Hata channels ambazo awali zilipotea nazo zimerejea kama Mozambique n.k kwa LNB c band hiyo hiyo ya Local channels.
Pia unaweza ukapata za kenya kama KBC n.k. kwa kutumia KU lbn!!
Share:

Jan 3, 2012

FREE CHANNELS





Kwenye Dish ndogo kuna channels nyingi za bure,inategemea na wewe unahitaji channels za vipi!!
Lakini kwenye Dish ndogo hupati channels hata moja ya Tanzania.
Kwa maelezo zaidi usisite kuuliza!!
Share:

Oct 18, 2011

Dish thamani yake itabaki pale pale!!

Popote ulipo na popote utakapo unafunga.


Uzuri wa Satellite Dish Antenna ni popote ulipo ama utakapoamua kuweka makazi ukilifunga utakacho kuona utaona ikiwa clear bila chenga,Dish inakaa popote na Signal inaingia lakini lisikingwe ili kupata Satellite husika hii inamaana Dish huwezi kufunga chumbani!!
Kwa kuongeze ukifunga Dish huwezi muona mwanao wakati anaenda shule maana kuna maswali mengi tunakumbana nayo,huko mitaani watu wanadanganyana ya kuwa ukifunga Dish kama nyumba ya pili choo chao vile vya uswazi unaweza ukamuona!!

Jamani jamani sio kweli hiyo ni kazi ya CCTV Camera!!!
Share:

Aug 31, 2011

Savvanah Bar & Restaurant

In Quality centre Dar es salaam....!!!
Mpaka sasa najivunia kuwa na watu ambao wanaheshimu uwepo wangu,wanathamini mchango wangu na mengineyo mazuri kama hayo,hii imepelekea leo kupewa shavu palee kwenye jengo jipya kabisa la Quality centre lililop pugu road,hapa ndani pana kitu kipya pia kinaitwa Nivvanah bar & restaurant...!!
Hapa tenda ilikuwa ya wenzangu ambao walikuwa wanafunzi wangu na wao ndo waliosababisha mimi kuhitajika hapo kwenda kutoa ambacho nilistahili kukitoa na mwisho wa yoote ikawa kama ambavyo utapata fursa kutembelea na kujionea..!!
Kuna channels za Local na DSTV zaidi ya yote kumepambwa na flat screen ni hayo tu kwa leooo...!!!
Share:

Aug 8, 2011

DSTV offer imeisha..!!

Ilikuwa kama utani na kuacha watu wakajiuliza hee DSTV kunani tena ama ndo wameishiwa,ama wameteteleka kwa sababu ya STAR TIMES...!!!??
Baada ya kutoa bonge la offer kwa 89000/= uliweza kupata full installations..!!
Watu wakajisahau na wengine wakiamini wataendelea kushuka ndipo wao watakapofunga ila mambo yakawa ndivyo sivyo,offer imeisha na wengine wakiitamani hata ile bei ya 89000/= ambayo muda wake umeshaisha..!!
Jamani labda kama itakuwa mmepoteza umakini ni kwamba Multichoice ni kampuni kubwa na ipo serious na kazi zaidi ya yote wanajua wakifanyacho na hata burudani zao za ukweli na ndio maana hata wateja zao ni watu makini na ambao wapo up to date..!!

Share:

Aug 4, 2011

CHANNELS ZA TANZANIA KWENYE DISH..!!




 Swali ambalo nakumbana nalo kila kukicha ya kuwa channel gani na ngapi za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish na kwanini nyengine hazipatikani? huku wengine wakidhani channels zote za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish..!!
Zaidi ya yote kuna ambao mpaka leo hii wanaamini ya kuwa ukifunga S.Dish Antenna hata zile channel ambazo zinatumia Antenna zitakuwa hazina chenga kwa sababu karibu na Antenna hiyo kuna Dish...!!
Channels za Tanzania ambazo zinapatikana kwenye Dish ni zile tu zinazotumia Satellite kurusha matangazo yao mfano:-ITV,CAPITAL,EATV,AGAPE,CHANNEL 10,STAR TV na TBC1.
Pia hakuna ufundi wa kufanya nyengine zionekane kwenye Dish mpaka wahusika watakapoamua kujiunga na Satellite.
Uzuri wa kutumia Dish ni kwamba hata nje ya nchi channel husika inaonekana kwa kutumia dish lakini kama utatumia Transmetter kurusha matangazo itakuwa ni Tanzania tu tena wala si nchi nzima sehemu chache tu za nchi..!!
Hivyo kuna ulazima wa channel zote za Tanzania kujiunga na Satellite kurusha matangazo yao,hii ni kwa faida yao katika kujitangaza zaidi maana itakuwa inaonwa na watu wengi zaidi..!!
C2C,DTV,CTN,TV TUMAINI,CLOUDS.
Hizi hazipo kwenye Satellite hivyo hazipatikani kwenye Dish.
Share:

Jul 14, 2011

MAPIPA COMMISSION AGENCY

Pesa si mbaya ila matumizi ndio ambayo mabaya na hii ndio 1 kati ya matumizi mazuri ya pesa,japo yale mabaya hata wakati unafanya unaamini ni mazuri kwako..!!
Nilikuwa sehemu 1 wanapaita Magomeni Mapipa kuna yard mpya ya kuuza magari imefunguliwa inaitwa MAPIPA COMMISION AGENCY jamaa hawa wanauza gari aina zote mzigo unatoka moja kwa moja toka Japan na bei zao pia ni za kawaida sana..!!
Hapa bana nikawafungia dish mbili za KU (ndogo) lengo ni kuona DSTV na Channels za bure za MBC na lengo likatimia na mambo yakawa kama ambavyo pesa ilitumika kutaka mazuri ndivyo walivyoyapata..!!
Zamani banaa ndo ilikuwa mtaani ama nyumba ikifungwa dish wao wanaume lakini si sasa kwani bei ni za kawaida tu isipokuwa ilikuwa imani za watu tu,kama vipi tugongee nawe uzunguke dunia kama ambavyo wenzio wanavyozunguka wakiwa na TV zao majumbani..!
Share:

Jul 8, 2011

Somewhere in Tabata..!!

Haya ndio kati ya mambo yanayotufanya tuwe bize na heshima iwepo katika jamii na maisha yaweze kwenda mbele..!!
Hii ni sehemu moja wanapaita Tabata jijini Dar es salaam,kilichofanyika ni kuinstall DSTV katika vyumba vyote nyuma nzima pamoja na Local channels,zilizo kwenye Dish na zilizo kwenye Antenna kisha tukachukua vilivyo vyetu mwendo kijumba kinachofuata..!!
Share:

Jul 3, 2011

Tupo pamoja ila Email ni nyingi sana na zote nitazijibu..!!

C kwamba nimewapotezea wadau wangu laa hasha,ila kazi ni nyingi na utulivu unakuwa mdogo sana,yote ni ninyi mnaonifanya mimi niwe bize hivyo nathamini sana uwepo wenu hivyo wote mtapata kile mnachotaka ijapokuwa inaweza ikawa si kwa muda ule utakao ila ukiwa mvumilivu tatizo lako hapa ndipo kwenye solution.
Pamoja sana.
Mustapha MaDish.
Share:

Jun 20, 2011

TUSIUCHUKULIE POA UKIMWI..!!


 Kwa mtazamo wangu kutokana na research ndogo niliyoifanya inaonyesha kwa sasa swala la gonjwa la ukimwi si kama ilivyokuwa kama miaka ya nyuma na kadri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kuchukulia poa na kuona kama  mtu kuugua mafua na maisha kuendelea kama kawa..!!
Nimetumia neno kuchukulia poa kwasababu katika watu ambao nawakusudia zaidi ni vijana ijapokuwa wote nataka twende sawa ila kwa vijana ni too much..!!
Leo hii NGONO imekuwa ndio inawatumikisha sana watu,utakuta watu wapo bize sana kwa ajili ya kufanya NGONO.wanatafuta pesa,wanaongopa,wanatumia muda mwingi sana na kufanya kila linalowezekana ili tu mwisho wa siku wafanikishe kufanya NGONO.
Siku hizi idadi ya walio wengi wanapenda sana ngono na upendo wa dhati unakuja baada ya kufanya ngono na hii inasababisha idadi ya wanaooa/kuolewa hupungua kila kukicha maana inakuwa ngumu kudumu kwa kutokupata kile ambacho either alikitegemea kabla ama alitaka tu kuona kiundani inakuwa aje..?
Mapenzi yanadumu miezi kadhaa tu then wanaachana ama mtu mmoja anakuwa na zaidi ya mpenzi mmoja na ndo pabaya sana hapa..
Unayemuamini ana wapenzi wawili nawe ukiwa wa tatu,hapo hapo nawe unakiacha unayemuamini unao wengine wa kuzugia pengine watatu,inaweza ikawa mpenzi wako unayemuamini hayuko poa kifedha hivyo kuna wa kukununulia vocha na matumizi mengine huku ukiwalipa kwa penzi lako lakini huna future nao,uliye na future nae ndiye huyo mwenye wapenzi wawili wewe ukiwa wa tatu na yaweza kuwa mmoja tu kati ya hao ndo unatumia kinga tena pia pengine siku za mwanzo mwanzo tu na mkishazoeana inakuwa mpango....!!
Hapa UKIMWI utatukosa ??
Kama ulikuwa hujui automatically kama utamsaliti mpenzi wako jua ya kuwa nawe atakusaliti ama anakusaliti...!!
Jamani,jamani UKIMWI upo tusijisahaulishe kama vipi tuwe na mmoja na yakishindikana hayo TUVAE..!!
Ni hayo tu kwa leo toka kwangu kuja kwenu.
Mustapha E. Hanya
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita