Call / WhatsApp +255673378129

Apr 7, 2012

TOKA MOYONI IMENIUMA SANA!!

Sometimes unaweza ukakufuru na kutamani afe mtu fulani na aliyekufa akabaki,kutokana na mapenzi yako kwake ila aliyeumba ndiye kila kitu anaamua amchukue nani na muda gani,ukiangalia sana wale wazuri mara nyingi wanakuwa na uhai mdogo ila wale pasua wanaishi miaka miiingi ila siri anaijua Allah!

 Kiukweli nimeumizwa sana na kifo cha Kanumba,sababu ya mapenzi yangu kwake ila sina la kusema zaidi ya kumuombea alale mahala pema peponi!!
 Amefanya mengi mazuri na kusaidia wengi,mimi kwa Tanzania nilikuwa na wasanii wangu wawili tu wa kiume wasanii hasa JB na marehemu KANUMBA na ilikuwa nawaangalia wao maana huwa hawaharibu na sanaa kwao ipo kwenye damu yaani kama kipaji kipaji hasa!!
 Hakuna ama akitokea hawezi kuwa kama yeye!!
 Pumzika kwa amani mpendwa!!

 Alikweza kuwainua watoto wengi na huyu mmojawapo!!
Atazikwa jumanne katika makaburi ya kinondoni!!
Share:

Mar 26, 2012

WADAU SAMAHANI...

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu na umuhimu wa hii kitu kwenu tumeshindwa kuimaliza kurekebisha hii blog on time hivyo chochote ambacho mtakiona kipo tofauti na hii blog ni katika jitihada za kuboresha na soon itakuwa vizuri zaidi katika muonekano mpya na bora zaidi.
Unaweza kushiriki nasi kwa chochote ambacho unadhani tunaweza kufanya pamoja kupitia hii blog na mengineyo pia kama unahitaji huduma  yeyote katika kipindi hiki waweza wasiliana na muhusika kama si wahusika kwa njia zifuatazo: Kwa no.+255 659161111
Kwa email:mustaphamadish@gmail.com
Popote ulipo tupo nawe.
Ahsante n Karibu sana.
Share:

Mar 21, 2012

PATA KILICHO BORA!!

Wengi wanashida ya kupata Installer wenye uwezo na huduma bora!!
Hii ndo solution yenu!!
Kama wewe ni mmiliki wa Hotel ama unataka kujenga Hotel ama zile nyumba za wenyeji na hujui wapi utapata mafundi wenye uzoefu na kutoa ushauri kabla ya kufungiwa Channel unazotaka na kwa wakati!!
Huku bei ikiwa nafuu ambayo utaimudu kulipa huku huduma ikiwa ni ya kiwango cha kimataifa!!
Tunatoa huduma kisasa na kwa wakati tukizingatia ubora na matakwa ya mteja!!
Kwa maelezo zaidi unaweza wasiliana nasi kwa:
+255 732 575 718/716 899 155
mminstallers@ymail.com
Share:

Mar 17, 2012

FUFUA DISH LAKO LEO!!!

Aliyebahatika kufufua Dish lake!!
Nimegudua kuna Dish nyingi katika nyumba nyingi ambazo hazifanyi kazi zimekaa tu kama uchafu ama urembo!!
yanini kukaa na kitu kisicho na manufaa!!??

Share:

Jan 10, 2012

LOCAL CHANNELS ZATULIA KWENYE FUTI 6!!


Baada ya kusumbua muda mrefu hatimae Channels za Tanzania zote zilizopo kwenye Satellite zatulia!
Tatizo ilikuwa kama zinatulia za V za H zitasumbua na Zikitulia za H za V zitasumbua,tatizo hili huwa linatokea mara kwa mara na wala sitaki kuamimni kama ndio limeshakuwa limefika kikomo kwa ushauri tu ikiwa unataka Local channels kupitia Dish ukinunua la futi 8 itakuwa unapata uhakika wa kile ukitakacho kwasababu hata zikiwa zinasumbua kwenye futi 8 unaendelea kula raha!!
Hata channels ambazo awali zilipotea nazo zimerejea kama Mozambique n.k kwa LNB c band hiyo hiyo ya Local channels.
Pia unaweza ukapata za kenya kama KBC n.k. kwa kutumia KU lbn!!
Share:

Jan 3, 2012

FREE CHANNELS





Kwenye Dish ndogo kuna channels nyingi za bure,inategemea na wewe unahitaji channels za vipi!!
Lakini kwenye Dish ndogo hupati channels hata moja ya Tanzania.
Kwa maelezo zaidi usisite kuuliza!!
Share:

Oct 18, 2011

Dish thamani yake itabaki pale pale!!

Popote ulipo na popote utakapo unafunga.


Uzuri wa Satellite Dish Antenna ni popote ulipo ama utakapoamua kuweka makazi ukilifunga utakacho kuona utaona ikiwa clear bila chenga,Dish inakaa popote na Signal inaingia lakini lisikingwe ili kupata Satellite husika hii inamaana Dish huwezi kufunga chumbani!!
Kwa kuongeze ukifunga Dish huwezi muona mwanao wakati anaenda shule maana kuna maswali mengi tunakumbana nayo,huko mitaani watu wanadanganyana ya kuwa ukifunga Dish kama nyumba ya pili choo chao vile vya uswazi unaweza ukamuona!!

Jamani jamani sio kweli hiyo ni kazi ya CCTV Camera!!!
Share:

Aug 31, 2011

Savvanah Bar & Restaurant

In Quality centre Dar es salaam....!!!
Mpaka sasa najivunia kuwa na watu ambao wanaheshimu uwepo wangu,wanathamini mchango wangu na mengineyo mazuri kama hayo,hii imepelekea leo kupewa shavu palee kwenye jengo jipya kabisa la Quality centre lililop pugu road,hapa ndani pana kitu kipya pia kinaitwa Nivvanah bar & restaurant...!!
Hapa tenda ilikuwa ya wenzangu ambao walikuwa wanafunzi wangu na wao ndo waliosababisha mimi kuhitajika hapo kwenda kutoa ambacho nilistahili kukitoa na mwisho wa yoote ikawa kama ambavyo utapata fursa kutembelea na kujionea..!!
Kuna channels za Local na DSTV zaidi ya yote kumepambwa na flat screen ni hayo tu kwa leooo...!!!
Share:

Aug 8, 2011

DSTV offer imeisha..!!

Ilikuwa kama utani na kuacha watu wakajiuliza hee DSTV kunani tena ama ndo wameishiwa,ama wameteteleka kwa sababu ya STAR TIMES...!!!??
Baada ya kutoa bonge la offer kwa 89000/= uliweza kupata full installations..!!
Watu wakajisahau na wengine wakiamini wataendelea kushuka ndipo wao watakapofunga ila mambo yakawa ndivyo sivyo,offer imeisha na wengine wakiitamani hata ile bei ya 89000/= ambayo muda wake umeshaisha..!!
Jamani labda kama itakuwa mmepoteza umakini ni kwamba Multichoice ni kampuni kubwa na ipo serious na kazi zaidi ya yote wanajua wakifanyacho na hata burudani zao za ukweli na ndio maana hata wateja zao ni watu makini na ambao wapo up to date..!!

Share:

Aug 4, 2011

CHANNELS ZA TANZANIA KWENYE DISH..!!




 Swali ambalo nakumbana nalo kila kukicha ya kuwa channel gani na ngapi za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish na kwanini nyengine hazipatikani? huku wengine wakidhani channels zote za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish..!!
Zaidi ya yote kuna ambao mpaka leo hii wanaamini ya kuwa ukifunga S.Dish Antenna hata zile channel ambazo zinatumia Antenna zitakuwa hazina chenga kwa sababu karibu na Antenna hiyo kuna Dish...!!
Channels za Tanzania ambazo zinapatikana kwenye Dish ni zile tu zinazotumia Satellite kurusha matangazo yao mfano:-ITV,CAPITAL,EATV,AGAPE,CHANNEL 10,STAR TV na TBC1.
Pia hakuna ufundi wa kufanya nyengine zionekane kwenye Dish mpaka wahusika watakapoamua kujiunga na Satellite.
Uzuri wa kutumia Dish ni kwamba hata nje ya nchi channel husika inaonekana kwa kutumia dish lakini kama utatumia Transmetter kurusha matangazo itakuwa ni Tanzania tu tena wala si nchi nzima sehemu chache tu za nchi..!!
Hivyo kuna ulazima wa channel zote za Tanzania kujiunga na Satellite kurusha matangazo yao,hii ni kwa faida yao katika kujitangaza zaidi maana itakuwa inaonwa na watu wengi zaidi..!!
C2C,DTV,CTN,TV TUMAINI,CLOUDS.
Hizi hazipo kwenye Satellite hivyo hazipatikani kwenye Dish.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita