Call / WhatsApp +255673378129

Jun 21, 2012

DSTV KWENYE RECEIVER IMEKUFA!!


 Hii ni Receiver
Zamani ilikuwa unaweza ukanunua Receiver yeyote ambayo inasoma card then unaenda DSTV wanakuuzia smart card kisha wanalink baada ya hapo unakuwa mteja bila kununua Decoder hii ilikuwa inamfanya mteja kuweza kupata Channels za DSTV na zile za bure kama Local kiasi kwamba hata usipolipia DSTV utaendelea kuona zile za bure!!
Lakini huduma hii kwa sasa wamesitisha ili kupata huduma za DSTV ni lazima upate Decoder za DSTV!!
Hii inakuwa huduma ya pili kufungwa ya kwanza ikiwa ile ya kupata DSTV kwa kutumia C BAND na wale wenye Decoder za zamani kwa sasa pia hazifanyi kazi
 Decoder hii ya zamani

 Hii nayo ya zamani lakini unapata DSTV

 Zifuatazo ndizo mpya single view Decoder:







Share:

Jun 6, 2012

KARIBUNI WAPENDWA!!

Tarehe 10.06.2012 jumapili,40 ya baba yangu marehemu ESMAILY O.HANYA hivyo kama utapata chance karibu sana,inafanyika nyumbani kwake Magomeni Mapipa,Idrisa street no.27,karibu na delux bar/chipolopolo bar/kwezi dispensary,itakuwa saa 7 mchana!!
Nawakaribisha wote ndugu jamaa na marafiki wa ukweli!
Share:

May 19, 2012

NITANUNUA VING'AMUZI VINGAPI!!??

Tarehe 31.12.2012 saa 23:59 itakuwa mwisho wa Local channel kupitia c band na Antenna pia na ili upate Local itakulazimu ununue king'amuzi ama ving'amuzi kutokana na channel za Tanzania utakazo!!
Mawazo yangu binafsi kulikuwa na mapungufu mengi sana kwenye mchakato huu na mwisho wa siku inaonyesha dhahili wakuu walikurupuka hawakufikiri kwa kina kabla ya kuweka mwisho mwaka huu!!
Tuangalie hali za watanzania wengi wao ni duni then tuangalie bei za ving'amuzi na channels zinazopatikana kwa kila king'amuzi,kuna kampuni moja tu ambayo binafsi naipa pongezi za kutosha EASY TV unapata Local channels karibu zote na bei yao ni 9000 tu kwa mwezi lakini zooote tupa kule!!
Nawaangalia wale wa vijijini ina maana hawastahili tunachokipata!!?? maana ilikuwa mtu anajipinda anafunga Dish ya Local anasahau,haina malipo ya mwezi wala nini zaidi ni kurekebisha tu litakaposumbua!!
Au ndo wazo la mtu mmoja tu alienda nje ya nchi akaona watu wapo UP TO DATE then akaja Tanzania kuwashawishi viongozi wakalipitisha,je mnajua hao ambao wanakwenda na wakati walianzia wapi!!??
Wananchi wengi watakosa haki yao ya msingi ya kupata habari kwa kukosa pesa ya kulipia ili aone/asikie hiyo taarifa ya habari.
IJAPOKUWA HATA NKISEMA WALIOLIPITISHA LIMEPITA,HAKUNA JINSI ILA UJUMBE SI MBAYA UKAWAFIKIA NA MKAONA MLIVYOVURUNDA HAPA!!
Ina meengi sana ila wacha niishie hapa nisije nikanyimwa hata hizo tenda maofisini mwao maana ndo hao hao wateja zangu!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita