Call / WhatsApp +255673378129

Oct 4, 2013

CHANNEL ZA BURE!!!!!!

Kuna kitu watu wengi wanashindwa kuelewa ni kwanini Aljazeera na Abudhab malipo yao ni rahisi pengine tofauti na Dstv hivi!! Ukweli ni kwamba hawa jamaa wana channel chache sana na ni za sport tu isipokuwa Satellite ambayo wanatumia kuna channel nyingi za bure hivyo humpumbaza mteja na kuona wanachannel nyingi malipo yao kidogo!!
 Ambacho nataka kukwambia ukitumia Receiver ya kwaida na ukaelekeza Dish yako NILESAT unakamata channel kibao za bure!!
Nilesat ama kwa waliozoea ukiwaambia Aljazeera,unaweza ukakamata kwa kutumia Dish zifuatazo:-

KU ft 4

KU ft4 ikitimizwa!

C band ft6 tayari kwa kuweka KU lnb

C band ft6 imekamilika

 Pia unaweza ukapata kwa kutumia C band ft8!!!

Share:

Oct 1, 2013

TRENET KWENYE DISH NAYO!!

Digital ndo habari ya sasa!
Sasa ile channel ya dini ya Trenet tv nayo kwenye Dish tena ikiwa bure!
Unaipata kutumia Dish ndogo,satellite husika Intelsat 17 nyuzi 66E,kama muelewa wa masuala ya madish tofauti nyuzi mbili na Emanuel tv kwenye dish ya KU!!!
Kwa mtazamo wangu wanaweza wakaja kuhama Satellite baadae maana hapa walipokaa wapo wenyewe tu kwa Tanzania hivyo wanaweza wakahamia zilipo nyengine ili kuwapa urahisi wapenzi wa channel hiyo ila kama wataendelea kuka hapo hapo inaweza ikawa mtihani kidogo kwa wadau!!
Share:

Sep 29, 2013

HATIMAE CLOUDS TV KWENYE DISH!!


Swali la wengi leo limepata jibu maana walikuwa wanauliza Clouds tv mbona haipo kwenye Dish,ukweli ni kwamba hili lilikuwa ni swala lililo ndani ya uwezo wa Clouds Media Group na sio mimi Mustapha Madish!!
wamefanya walichopaswa kufanya,ambapo kwangu imekuwa fulsa ndo hivi naitumia kuwaunganisha watu kuangalia clouds tv kupitia Dish,uzuri wake ni kwenye Dish ndogo pale pale zinapopatika zile za Local!!!
Hii inafanya idadi ya channel za Tanzania zinazopatikana kwenye Dish ndogo kuongezeka!!
Zaidi ya yote unapaswa utumie Receiver ya MPEG4 na si MPEG2!
Share:

Sep 13, 2013

KAZI NZURI KWA MACHO YAONEKANA!

Awali hapa fundi alipita na kutumia uwezo wake kufanya alichofanya na kuondoka,lakini haikupita muda kwa mujibu wa mwenyewe Dish ikazingua na fundi akipigiwa kimyaaaa!!
Wapi alipo MustaphaMadish baada ya kunipata solution ikapatikana!!
Kwanza labda nitoe angalizo kwa wateja na mafundi wote kama mimi Dish iliikae muda mwingi bila kusumbua ni lazima ikae sehemu ambayo unaweza kudril,vinginevyo itakuwa kila siku fundi hachezi mbali nawe!!
Hapa nilikuta Dish imewekewa mawe hivyo ikawa kila muda inacheza na kwa kuongezea mawe huchangia Dish kupata kutu maana mvua inaponyesha mawe hunyonya majina mpaka kukauka inachukua muda!

 Toboa toboa inaanza!

 Baada ya toboa!

 Somo linaeleweka!

Toboa inaendelea!

Wakujiita Kenya akikaza kaza!


+255789476655

Share:

Sep 3, 2013

TOKA AFRICANA KWENDA SALASALA

+255789476655/659161111/714973797
Ukija kwenye swala la kuhama toka nyumba moja mpaka nyengineni ni jambo la kawaida sana kuhama na Dish yako iwe ya DSTV ama ya kawaida yeyote ile unahama nayo na channel zako zile zile ama zinaweza kuzidi kama ulikuwa hujui!!!!
Ambacho wengi hawajui na kuona ni kitu cha kawaida tu kuifungua Dish iliyokwishafungwa then unatafuta fundi wakati wa kutaka kufunga ulihamia je unajua madhara ya kuifungua mwenyewe ikiwa haupo makini!!??
Kwanza unaweza ukaiharibu LNB!
Unaweza ukalipinda Dish na kumpa shida fundi wakati wa kufunga!
Hii inatokea kwenye ufunguaji na ubebaji pia toka ulipohama mpaka ulipohamia!
Lakini kama utaifungua kwa umakini inawezaekana kila kitu kikafika salama.
Hii ni DSTV ilikuwa naitoa Mbezi Africana na kwenda kuifunga Mbezi salasala kama ambavyo mwenyeji wangu alivyonituma!

 Hapa nafanya setting zangu

Hapa tayari signal za kumwaga  ila haijalipiwa
Share:

Sep 1, 2013

CHANNEL ZA TANZANIA KWENYE DISH NDOGO


Awali ilikuwa huwezi kupata Local channel mpaka ufunge dish ya c band yaani dish kubwa,lakini sasa mambo ni tofauti kwani unaweza kupata Local channel kwa kutumia kadish kadogo (KU) na lnb ya ku,isipokuwa Receiver ni lazima utumie ya MPEG4 tofauti na upatikanaji wa kwenye c band ambapo hata kwa MPEG2 unapata Local channel!
Channel za Tanzania zainazopatikana kwenye Dish ndogo:-
  1. TBC
  2. CAPITAL
  3. EATV
  4. ITV
  5. CHANNEL 10
  6. ATN
  7. STAR TV 
na nyenginezo za nje ikiwemo Emanuel tv kwa wale wapenzi wa Gospel!
+255789476655/714973797
Share:

Aug 22, 2013

TOKA KINYELEZI MPAKA K'KOO!!!

 Hivi ndivyo masaa yanavyokatika tukiwa tunawajibika kama ilivyoada ili mkono uende kinywani!
Kutoka Kinyelezi ilipokuwa Dish ya DSTV na kutakiwa ihamishiwe Kariakoo ili maisha yaendelee kama kawa watu wakila burudani zao wakiwa na tv tuu!!
 
Hapa tayari kwa kufunga Dish!
 
 Imeshika kwa ukuta!
 
 Imetokeza kwa bati

Hapa setting zikiendelea

 Hapa kitu mwake!
Ila katika site ambazo kama si ubunifu wa fundi itakuchukua muda mrefu ama kutokupata signal kabisa hii ni mojawapo site pasua ila kwakuwa ndo hivyo tena Mustapha MaDish nikadish dish hapo kisha nikachukua vyangu nikachapa mwendo kama kawaida!
Share:

Aug 16, 2013

HUYU KATI YA WENGI WALIONIPATA KUPITIA MTANDAO!

+255789476655
Hapa ilikuwa hakuna kitu kinaitwa signal,na sababu kubwa inayofanya natembelea vijumba ama office za watu ikiwa Dish imeshafungwa signal kupotea mi fasta nakurejeshea!!!!
Hapa ni Mwenge,mitaa flani hivi imetuliaaa!!

 Kuonekana imooo!!

 Tayari kwa kuanza kazi

Unga unga ya Mustapha MaDish

 Signal zimeanza kuingia

 Single solution lnb

 Hapa Dish signal za kutosha

 Nikarejesha ndani kila kitu safii!!!
Ila hapa ilinichukua siku mbili coz siku ya kwanza kuangalia kazi na kama kuna cha kuhitajika then nilipokuja kama dish namjua aliyelitengeneza,maelezo niliyotoa ndicho mteja alichoona! 

Share:

Aug 10, 2013

Karibu na ubarozi wa Ufaransa!

+255789476655
Muda ambao vijana wenzangu wanatumia mtandao kupiga soga na kupotoshana mi kwangu ipo tofauti sana tena sana maana kila kukicha naongeza idadi ya marafiki si kupiga piga soga zisizo na maana bali kufanya haya ya kupendeza na hapa nimefika kutokea mtandaoni umenisomaaa!!!!!














Share:

Aug 8, 2013

ALJAZEERA SPORTS

Maswali yamekuwa mengi mkiniuliza mnawezaje kupata Decoder za Aljazeera sports ila jibu huwa nalitoa moja tu kama ilivyo kwa Abudhab Sport pale awali...!!
Hii kampuni haina wakala hapa bongo na kama yupo mi simfahamu maana kila ninyemfungia anakuwa anaagiza mwenyewe ama nafanya muunganiko then nawaacha wakubaliane jinsi ya kuagiza kutoka kwa waarabu!!
Hii pia mwendo ule ule jamaa katoka nayo mwenyewe mimi nilichofanya kutafuta dish inayofaa na kuleta ufundi wangu na mwisho wa siku yakawa yaliyokuwa!!

Hapa naangalia cha kuchukua ili nisababishe!

Hapa nafunga stend baada ya kudril!

Hapa nafunga Dish kwenye stend!

Hapa tayari imekaa still!

 Hapa tayari kwa kuanza kufanya setting!

 Hii ndio Decoder ya Aljazeera Sports

 Hapa vipi!!??
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita