Call / WhatsApp +255673378129

Dec 31, 2013

TUNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WADAU!!!


Mwaka ndo unaishia hivyo leo ikiwa Tarehe 31/12/2013 dah! yaani hata siamini wallah!!
La msingi nashukuru Mungu kwa kunijalia pumzi mimi,timu yangu nawe mdau wetu kama u bu kheri wa afya kama ilivyo sisi!!
Wapo wengi waliotamani kufika leo ila kwa mapenzi yake mungu hatunao tena,tuwakumbuke kwa kuwaombea dua na kuwatolea sadaka kwa ajili yao kama kweli tunamapenzi nao!
Mwaka ikiwa unaishia tunapenda kuomba radhi kwa wale wote tuliowakosea maana hakuna aliyekamili chini ya jua,mimi binafsi na kwa niaba ya Mustapha MaDish Crew tunawatakia heri ya mwaka mpya!!
Msherehekee kwa amani na utulivu!!
Katika kazi kuna changamoto nyingi sana na ukizingatia sisi tunafanyakazi na watu wa aina tofauti,sehemu tofauti kiukweli wakati mwengine changamoto zinakuwa za kiwango kikubwa mno lakini cha kushukuru tunafanikiwa kukabiliana nazo zaidi ya yote tukumbushane hii ni kazi kama zilivyo kazi nyengine la msingi ni kuheshimiana ili lengo litimie!
Zaidi ya yote yale maoni yenu yote tunayafanyia kazi ili mwaka unapoanza uanze tukiwa wapya hasa!!
MALIZA MWAKA FUNGUA MWAKA UKIJUA!!
Kuwa hapa ndipo nyumba ya ving'amuzi vyote unavyovijua wewe Tanzania!
Tunauza na kufunga kwenye nyumba hadi nyumba,maofisini,kwenye Hotel!
Mafundi wana uzoefu unaomaliza mwaka wa 7 mpaka sasa!!
Namba yetu ni ile ile +255789476655 Office.
+255659161111 Technical support.
Share:

Dec 27, 2013

POPOTE ULIPO TUPO NA WEWE
























Mwaka tunaumaliza vema na tukisisitiza ya kuwa popote ulipo tupo nawe,king'amuzi chako kinakuweka karibu nasi huku ukiwa unaizunguka dunia ukiwa na tv yako!
USIHOFU ULIPO NI WEWE TU KUWA TAYARI KUPOKEA HUDUMA ZETU KWA KUPIGA NO.
+255789476655/714973797/659161111

Share:

Dec 24, 2013

BONDENI HOTEL TUKIFUNGA AZAM TV

+255789476655 AU +255627985436 HUDUMA HII INAKUFIKIA
 Kuelekea funga mwaka na Azam tv ikiwa inaendelea kufanya vizuri,nasi tukiendelea kutekeleza wajibu wetu kama kawa kama dawa!
Ndani ya Bondeni Hotel ya Magomeni Mapipa Morogoro rd.
Hapa Azam tv nayo ilionekana umuhimu wake!



Dumee akiwa na Mustapha MaDish baada ya kumaliza kufanya yetu!
Share:

Dec 21, 2013

AZAM TV MTEJA WA KWANZA KUFUNGA MKULANGA!

 Njiani kuelekea .......................!!!


Kuelekea funga mwaka kwetu ni mbio tu!!
Leo kazi ya kwanza tumeamkia mkoa Pwani wanapaita Mkulanga,hii mimi ni mara ya pili narejea kufunga Dish ila safari hii Azam tv ikiwa ndo imenirejesha nikiwa na mtaalamu mwenyewe Herman!!
Kiukweli haikuwa tabu na mara nyingi ndivyo inavyokuwa,site ambazo nje ya mji ama mikoani tofauti na Dar es salaam ukifunga Dish katika pisition husika haisumbui kupata signal ila katikati ya jiji ukifunga dish kama si mzoefu lazima itakutafuna!
Hapa Mkulanga ni karibu kabisa na shule ya msingi ya mkulanga,tulitumia saa 1 tu kufunga azam tv na kugeuza mkoa wetu wenye kila aina ya majambo!
Ilikuwa tuingie pale Mbagala ila kwa bahati mbaya mteja wetu wa azam tv alisema anaenda kuangalia mpira hivyo tufanye kesho!
Ratiba haikuishia hapo tukapandisha mpaka mbezi kwa Msuguli hapa tukafanya ya kupendeza then tukachapa mwendo mpaka Mbezi Maramba mawili azam tv ikiwa inaonyesha kuwa watanzania wameielewa!
Baada kuuza kama kawa ratiba ilisema twende kunduchi mtongani lakini kutokana na muda hatuna budi kukubaliana na mipango ya Mungu,hivyo wajibu wetu kupumzika na Inshallah kesho ratiba itaendelea tukianza na vilivyolala!!!
Niwatakie maandalizi mema ya X mass na mwaka mpya wadau huku nikiwashukuru kwa kila hatua ambayo tulikuwa sambamba zaidi ya yote usisahau kuwa hii ni nyumba ya ving'amuzi!
Uliza,Sema,Nunua ama chochote kuhusu kinga'amuzi chochote ukijuacho ama unachokisikia!
Share:

Dec 20, 2013

BAADHI YA CARD ZA ALJAZEERA ZIMEFAIL!

Kuna baadhi ya wateja wa Aljazeera sports wanalia sasa kama si kuhaha na kudhani pengine ndo imeshakula kwao maana wanakosa jibu la uhakika kuhusu card zao! Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya card zimefail na tatizo ni la kwao wenyewe na kwa mujibu wao wanalifanyia kazi! Je wewe ni miongoni mwao ama!!?
Share:

Dec 15, 2013

LOCAL CHANNEL ZINAZOPATIKANA DSTV

Awali ilikuwa TBC1 pekee,ambapo baadae ikaongezeka na STAR TV na hivi karibuni CHANNEL 10 nayo imeongeza idadi na kuwa channel 3 za Tanzania zinazopatikana DStv



Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita