Aug 4, 2011
 Swali ambalo nakumbana nalo kila kukicha ya kuwa channel gani na ngapi za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish na kwanini nyengine hazipatikani? huku wengine wakidhani channels zote za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish..!!
Zaidi ya yote kuna ambao mpaka leo hii wanaamini ya kuwa ukifunga S.Dish Antenna hata zile channel ambazo zinatumia Antenna zitakuwa hazina chenga kwa sababu karibu na Antenna hiyo kuna Dish...!!
Channels za Tanzania ambazo zinapatikana kwenye Dish ni zile tu zinazotumia Satellite kurusha matangazo yao mfano:-ITV,CAPITAL,EATV,AGAPE,CHANNEL 10,STAR TV na TBC1.
Pia hakuna ufundi wa kufanya nyengine zionekane kwenye Dish mpaka wahusika watakapoamua kujiunga na Satellite.
Uzuri wa kutumia Dish ni kwamba hata nje ya nchi channel husika inaonekana kwa kutumia dish lakini kama utatumia Transmetter kurusha matangazo itakuwa ni Tanzania tu tena wala si nchi nzima sehemu chache tu za nchi..!!
Hivyo kuna ulazima wa channel zote za Tanzania kujiunga na Satellite kurusha matangazo yao,hii ni kwa faida yao katika kujitangaza zaidi maana itakuwa inaonwa na watu wengi zaidi..!!
C2C,DTV,CTN,TV TUMAINI,CLOUDS.
Hizi hazipo kwenye Satellite hivyo hazipatikani kwenye Dish.
3:50 AM   Posted by Mustapha Hanya with 4 comments

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Ahsante kaka..!

Anonymous said...

Mimi nipo na DVD yangu lakini kama receiver ina channels kibao hivi naweza kuitumiaje..??

Anonymous said...

Channel 10 inazingua sana vipi ni tatizo la dosh langu au hali ya hewa tu kwasababu wakati mwengine inakuja na inatulia lakini sometimes hata kutokea ukiachilia kukata kata picha!!

iddi sharif said...

Nikitumia dish dogo la kawaid nawez kupat chanal ngap

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search