• KUEPUKA DISH LAKO LISIPATE KUTU

  Somo hili linawahusu wale wote ambao wanamiliki ving'amuzi vinavyotumia Dish, pia kwa wale wenzangu na mie Mafundi wa ving'amuzi ( Mafundi wanaofunga ving'amuzi )hususani kina #FundiKalipua, anafanya kama anategesha kwa ufungaji wake na akishaondoka king'amuzi alichofunga kinasumbua na mteja ukijaribu kumpigia kurudi inamuwia vigumu.
  Kikubwa kinachopaswa kuzingatiwa kila kilichomo kwenye seti ya dish kinatumika, kwa kutokutumia baadhi ya vilivyomo inasababisha madhara yasiyo ya lazima, mfano ulio hai ni dish kupata kutu.

 • JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI

  Moja kati ya naweza nikasema kero za watumiaji wa ving'amuzi karibia vyote Tanzania mnakumbwa na hili tatizo, wengi wenu mngetamani kuona utaratibu unakuwa tofauti na ulivyo sasa.
  Hii hapa list ya ving'amuzi na jinsi gani unaweza kuhama kifurushi mara baada ya kulipia either kifurushi cha juu zaidi ama cha chini zaidi. Ving'amuzi vilivyo kwenye list ni Azam tv | DStv | StarTimes | Zuku tv | kwa vilivyokosekana maboresho yanafanyika.

 • sHUKRANI KWA KUWA PAMOJA NASI

  Najua blog yangu hii imekuwa msaada mkubwa sana kwako kwa kila aliyepita hapa akiwa na shida yake yeyote inayohusu king'amuzi ama ulimwengu wa Digital tv huwa inamalizika kikamilifu. Hili ndio lengu langu hivyo sina budi kutoa shukrani za dhati kwako kwa kuwa na mimi mpaka leo hii, kuniamini na kuthamini kile nilichoamua kukifanya kwa mapenzi yangu yote.
  Hii ndio sehemu pekee ambayo inaweza ikazungumzia kuhusu ving'amuzi vyote..

Jan 7, 2018

HD kirefu chake ni High Definition - ni picha yenye ubora zaid ya SD kirefu chake ni Standard Definition kama kwa mfano unavyoonekana hapo chini!
 Ili uangalie katika mfumo wa HD ni lazima kama ni tv iwe ni HD pia na utumie cable maalum inayoitwa HDMI CABLE
HD imegawanyika katika ubora tofauti kutokana na Technology kuendelea kukua kila kukicha
 • HD - 720p ( 1280x720 )
 • Full HD - 1080p ( 1920x1080 )
 • ULTRA HD  4K- 2160p ( 3840x2160 )
 • ULTRA HD 8K- 4320p ( 7680x4320 )

Ukiwa una tv HD unapaswa pia uwe na vishiriki HD navyo, mfano uwe na King'amuzi ama Ving'amuzi DH na DVD pia iwe HD dhumuni la kukushauri utumie vishiriki HD navyo ili uweze kuona picha katika muonekano wa HD, kwanini!? ikiwa tv ni HD ukitumia king'amuzi ama DVD ambayo sio HD hautaona picha katika mfumo wa HD na hata kama utatumia king'amuzi ama DVD HD lakini ukatumia cable ya AV hautaona picha katika mfumo wa HD badala yake utaona picha katika mfumo wa SD ili uone katika mfumo wa HD ni lazima utumie cable ya HDMI CABLE

Ukiachilia hilo kuna baadhi ya picha zenyewe zipo katika mfumo wa HD na ndicho ambacho kinafanywa na wadau wengi wa mambo ya film Productions iwe kwenye vituo vya matangazo ama watengenezaji wa filamu..
Kwa Tanzania tunatumia sana HD na Full HD lakini kwenye Ultra HD nisiwe muongo bado sijakutana nazo ama aliyekutana nazo aniambia hapa..
1:10 AM   Posted by Mustapha Hanya with No comments
Soma zaidi

Jan 3, 2018


Biashara ushindani hivyo kuna maboresho kila kukicha kwenye swala la kukidhi haja za wateja na leo nakuletea list ya bei za ving'amuzi kwa mwaka 2017 na jinsi ya kununua kwa bei hii:-
 • Azam tv inauzwa Tsh 135,000/= Hii bila kifurushi wala Ufundi! Ila ina Offer katika malipo! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
 • Digitek inauzwa Tsh .......
 • DStv inauzwa Tsh 79,000/=  Hii bila Ufundi ila ina Offer ya kifurushi cha mwezi mmoja! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
 • Continental inauzwa Tsh .... ya Dish na Tsh 40,000/= ya Antenna. Hii bila ufundi ina Offer ya kifurushi cha miezi..! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
 • StarTimes inauzwa ya Dish Tsh 78,000/= na ya Antenna Tsh 34,000/= Hii bila ya Ufundi ina Offer ya kifurushi cha miezi...! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
 • Ting HD inauzwa ya Dish Tsh 100,000/= na ya Antenna Tsh 90,000 ina Offer ya kifurushi cha miezi..! Hii bila Ufundi Bofya Hapa
 • Zuku tv inauzwa Tsh 88,000/= Hii bila Ufundi ila ina Offer ya kifurushi cha miezi...! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
Zijue bei za vifurushi kwenye ving'amuzi kwa mwaka 2018 
Jinsi ya kuhama kifurushi
Kuepuka Dish lako kupata kutu
Kupata Mafundi Professional
10:07 PM   Posted by Mustapha Hanya in , , , , , with 5 comments
Soma zaidi

Jan 2, 2018


Tayari tumeshaingia ungwe nyengine nikiwa na maana tayari tumeachana na mwaka 2017 na sasa ni mwaka 2018 na ndio kwanza tunauanza.. Tuachane na ya mwaka 2017 sina maana hayapaswi kuangaliwa na kuyafanyia kazi laa nikiwa na maana kuna ambayo yapo mapya ambayo tunapaswa kueleka macho yetu huku..!!
Hii hapa orodha ya ving'amuzi na bei za vifurushi bila kusahau idadi ya channel zilizopo kwa vifurushi vyote kwenye ving'amuzi vyote Tanzania kwa mwaka mpya 2018..

Tumaini langu ni kwamba kwa uchache huu nimekurahisishia kitu, katika kutaka kujua bei mpya kwa mwaka 2018.. Kama una Swali, Maoni, Ushauri ama chochote niandikie kwenye ukurasa wa Comment, kama unahitaji private niandikie kwenye Email: mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
JUA ZAIDI...
 
10:07 AM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Jan 1, 2018

Kitendo cha kuendelea kupumua na kufanikiwa kuuona mwaka mpya 2018 unapaswa kushukuru, mshukuru Mungu bila kuangalia una hali gani ama yale uliyoyapa kuwa kwa mwaka 2017 hayajawa..
Binafsi nimeshashukuru na nachukua nafasi hii kukutakia kila la heri katika mwaka huu mpya wa 2018, ni wazi utakuwa mwaka wa kumalizia pale ulipoishia muda ambao mimi nalitazamia hilo kwako bila kuficha hicho ndicho nitakachokifanya kwangu/kwetu.. Yapo ambayo niliyapanga kwa mwaka 2017 yawe yametimia lakini kwa mapenzi ya mungu hayajatia hivyo imani na juhudi zetu mwaka huu yaweze kuwa....
Hii ni nafasi nzuri kwako kukushukuru wewe ambae kila leo unapita kwenye hii blog na kupatamawili matatu, nakushukuru sana kwakuwa bila wewe hata hii blog isingefika hapa, muda ambao wewe unapata faida kupitia hii blog kwa upande wangu pia nimepata faidi kupia hii blog.. 
Awali sikuwa najua kama naifikia idadi kubwa ya jamii ila pongezi na maoni nnayoyapa ndio yaliyopelekea niwe serious zaidi.. Kama ambavyo wengine wanaamini ya kuwa kwenye blog hii ndio sehemu pekee ambayo utapata kujua kiundani kuhusu ving'amuzi vyote, na ulimwengu mzima waDigital tv bila kuvutia biashara, nawe unapaswa kuamini hivyo lengo la blog hii ni kukupa wewe ELIMU, USHAURI,MSAADA, HUDUMA na HABARI kuhusu yote yanayohusu ulimwengu wa Digital tv, mlionufaika na blog hii mtakuwa mpo pamoja nami kwa msemo wangu huu.
Moja ambalo binafsi linaenda kunikwaza ni jinsi ya unavyohitaji msaada, wachache wenu hamzingatii muda, mimi sifanyi mazungumzo na mdau yeyote kwa saa 24 isipokuwa ni kuanzia saa 2 asubuhi mapaka saa 2 usiku kila siku na huwa sina utaratibu wa kuzima simu, kutokuwa na utaratibu wa kuzima simu imekuwa ndio fimbo ya kunipigia.. Nilishawahi kupokea simu alfajiri mdau ana shida.. saa 6 usiku.. saa 8 usiku... saa4 ama 5 usiku ndio nyingi sana..
Huwa napokea kwakuwa hii namba sio ya wadau wa humu tu hata wale watu wangu wengine ila nnapogundua ni wadau wangu nawaomba wapige muda wa kazi. Naomba nisisitize simu ya humu haifanyi kazi saa 24 hivyo kabla ya saa 2 asubuhi usipige na baada ya saa 2 usipige.
Mungu ibariki Tanzania!

5:46 AM   Posted by Mustapha Hanya with No comments
Soma zaidi

Dec 31, 2017

Kwenye Technology kuna vifaa ambavyo kuvitafutia lugha ya kiswahili moja kwa moja hakuna ila nitakachojitahidi kufanya ni kukupa urahisi ili uelewe pasi kutoka nje ya maana yenyewe.LNB ni nini?
LNB ama kwa kirefu chake ni Low Noise Block downconverter, ni kidubwana,kifaa kidogo kinachokaa kwenye dish ambacho kinapokea signal toka kwenye satellite na kupeleka kwenye satellite receiver ( King'amuzi kinachotumia dish ). Pia huitwa low-noise converter (LNC), au low-noise downconverter (LND), hiki kifaa wakati mwengine kinaitwa low-noise amplifier (LNA).

LNB ni mchanganyiko wa low-noise amplifier, frequency mixer, local oscillator na intermediate frequency (IF) amplifier. Inapokea microwave signal kutoka kwenye satellite iliyokusanywa na Dish, inaimarisha, na inachagua mzunguko wa mzunguko kwenye upeo wa chini wa mzunguko wa kati (IF). Hii downconversion inaruhusu signal kuletwa ndani kwenye Satellite receiver kwa kutumia Coaxial cable. ikiwa Signal ilibaki katika asili yake microwave frequency ingehitaji gharama kubwa na impractical waveguide line.

LNB kwa kawaida ni kisanduku kidogo kinachofungwa mbele ya uso wa dish kwa kutumia mfano wa fimbo ( kibomba/ vibomba ). Microwave signal kutoka kwenye dish inachukuliwa na  feedhorn kwenye LNB na hutolewa kwa sehemu ya waveguide.

LNB hufanyakazi kwa kutumia umeme ambao utatokea kwenye Satellite receiver kwa kutumia coaxial cable na huchomekwa sehemu iliyoandikwa LNB IN ikiwa imetumika pin katika kufanya coaxial cable kufunga kwenye Receiver na kwenye LNB pia.

AINA ZA LNB
 • Ku band 
 • Ka band
 • C band
Post hii itaendelea...
+255789476655

11:08 AM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Dec 21, 2017


Ving'amuzi vyote unavyovijua wewe iwe vya bure ama vya kulipia, nikiwa na maana vyenye kulipia malipo ya mwezi na visivyo na malipo ya mwezi, unaweza kutumia king'amuzi kimoja kwa tv zaidi ya moja, kwa kutumia king'amuzi kimoja unaweza kugawa picha kwa tv hata zikiwa 100.
Hii inawezekanaje!? kwanza unapaswa kujua ni king'amuzi gani ambacho unataka kugawa picha kwa tv zaidi ya moja,  chagua kwenye orodha hapo chini:-
 • Azam tv
 • Continental 
 • Digitek
 • DStv
 • StarTimes
 • Zuku tv
NB:Nitaweka link kwa kila king'amuzi ambayo itakupeleka mpaka kwenye post ambayo itakuwa na maelezo yote kwa kina.
Kwa Maelezo zaidi hii hapa +255789476655
3:52 AM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Dec 15, 2017

 Tv ya kijerumani ya mwaka 1956

Neno "televisheni" linatokana na maneno mawili: tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na visio (kutoka Kilatini: mwono; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza television lililotoholewa katika Kiswahili televisheni.
Televisheni - TV au runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.
Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.
Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita).
Baada ya Vita Kuu ya II, mfumo bora wa utangazaji wa televisheni Black n White ulikuwa maarufu nchini Marekani na Uingereza, na seti za televisheni zilikuwa za kawaida katika nyumba, biashara na taasisi.Katika miaka ya 1950, televisheni ilikuwa katikati ya msingi kwa kushawishi maoni ya umma.  Katikati ya miaka ya 1960, utangazaji wa rangi uliletwa nchini Marekani na nchi nyingi zilizoendelea.. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (widescreen).
Tangu mwaka 2010, kwa uvumbuzi wa smart television, internet television imeongeza upatikanaji wa programu za televisheni na sinema kupitia mtandao kupitia huduma za video za Streaming kama vile Netflix, Amazon Video, iPlayer, Hulu, Roku na Chromecast.
Aina za tv

Siku za usoni nitakuja kuzungumzia kwa kina kuhusu yaliyo hapa chini:
Broadcast Systems 
 • Terrestrial Television
 • Cable Television
 • Satellite Television
 • Internet Television
Display Technologies
 • Disk
 • CRT
 • DLP
 • Plasma
 • LCD
 • OLED
 • LDTV
 • SDTV
 • HDTV
 • UHDTV
 Imeandikwa na Mustapha Hanya
11:38 AM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Dec 14, 2017Leo ukiwapa nafasi wapenzi wa mpira ambao ni wateja wa king'amuzi cha Azam moja ya swali kuu ni kuhusu uonyeshwaji wa ligi ya uingereza kama ambavyo mmoja kati ya wapenzi hao wa kabumbu walivyomuuliza mkurugenzi mkuu wa Azam tv Bwana Tido Mhando alipowatembelea wananchi katika hatua ya kuwashukuru wateja wa azam tv.
 +255789476655

1:44 AM   Posted by Mustapha Hanya in with 1 comment
Soma zaidi

Dec 13, 2017


Hii inaweza kutokea kwenye ving'amuzi vyote na hutokea makosa ya mtandao ama kama kifurushi ulichopo sio sahihi hivyo hakiwezi kufika mwezi kwa baadhi ya ving'amuzi! Mara chache mno hutokea kwa ving'amuzi kama cha Azam tv,DStv,Zuku, n.k. na huwa mara zote ni kufail kwa system tu na unachopaswa kufanya ni kutoa taarifa ili uweze kusaidiwa kwa kurudishiwa huduma. Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa upande waking'amuzi cha Startimes na huwa tofauti na ving'amuzi vyengine ili kujua zaidi Bofya hapa
2:20 PM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Dec 2, 2017


Awali tulikuwa na ving'amuzi viwili ambavyo havikuwa na malipo ya mwezi, kulikuwa na Digitek na Continental, baadae Continental wakaanza mfumo wa kulipia na kuwa na Vifurushi pia kutaka kujua zaidi kuhusu Continental decoder bofya hapa, tukabaki na Digitek ambapo ni king'amuzi pekee ambacho hakina malipo ya mwezi. Kwa kutokuwa na malipo ya mwezi kwenye king'amuzi cha Digitek kumefanya kwenye zile Tv ambazo zinauwezo wa kupokea matangazo ya Digital pasi kutumia king'amuzi kuwezesha kupata channels za Tanzania bila malipo yeyote na bila kutumia king'amuzi cha nje kwakuwa ndani ya tv kwa lugha nyepesi tunasema ina king'amuzi.

Kwa maelezo zaidi +255789476655
5:21 AM   Posted by Mustapha Hanya in , with 1 comment
Soma zaidi

Nov 27, 2017

Tunaelekea katika kumaliza mwaka 2017 na tunategemea kuingia mwaka 2018, yapo mengi ambayo kupitia blog hii umefaidika kwa hali yeyote ile kama ndivyo tunashukuru kwakuwa ndio lengo letu, lakini pia nadhani yapo yaliyokukera kupitia blog hii kama ndivyo tunasikitika na kukuomba radhi pia maana sio lengo letu na ukizingatia hata kama itatokea unafanya jambo zuri vipi sio wote watakaopendezwa nalo kwa kuzingatia wapo ambao lengo lao ni kuharibu tu ama kutengeneza njia ya kufanya vibaya.. Zaidi ya yote shukrani kwa wale wote walio pamoja nasi kwa mwaka mzima na hata hapo miaka ya nyuma maana bila ninyi wala mimi na team yangu tusingefika hapa na isingezaliwa MADISH TECHNOLOGY.
Leo nawaletea orodha ya ving'amuzi vyenye offer katika msimu huu wa kumaliza mwaka 2017:-
 Bofya king'amuzi ambacho unataka kujua offer yake na utapata maelezo ya kina kuhusu offer hizo!
+255789476655 
12:30 AM   Posted by Mustapha Hanya in , , , , with 1 comment
Soma zaidi

Nov 23, 2017


Hotel - Tv system installation:- 
Hii ni hotel ina flow zipatazo tano ina zaidi ya room 50, ina ukumbi wa mikutano,sherehe, ina restaurant, ina bar na kuna sehemu ya Disco pia. Hapa tulichofanya ni kufunga tv ambazo ni zaidi ya 60 tv ambazo kila moja inapokea channels 18 na kila tv inajitegemea,nikiwa na maana mtumiaji anaweza akabadili channel bila kumuingilia mwengine ( tv nyengine ).
Mfumo uliotumika
  Baadhi ya Vifaa vilivyotumika:-
 • Dish ya FTA
 • Receiver kwa channel za Free
 • Dish ya DStv
 • Decoder za DStv
 • Dish ya Azam tv
 • Decoder za Azam tv
 • Signal Ampl.
 • Splitters
 • Multiswitch
 • Cable 
 • Connectors


Dish zimefungwa tatu, mbili zikiwa ni za kulipia na moja ikiwa ni ya channel za bure,Signal inayotoka kwenye Dish inaingia moja kwa moja kwenye chumba maalum, ambapo tunaita control room, sehemu ambayo decoder na receiver zote 18 zinafungwa hapo na sehemu kubwa ya mfumo mzima unafungwa hapo, kisha zinatoka cable ambazo zinakuwa zimebeba channel 18 na zote zinaishia kwenye tv ambazo zipo vyumbani na kwengineko kwenye jengo la hotel.

Hii ni Control Room sehemu ambayo ile connection muhimu yote tumeimaliza hapa

Kwa maelezo zaidi +255789476655
Face Book


10:44 AM   Posted by Mustapha Hanya in , with 2 comments
Soma zaidi

Nov 11, 2017

Mwaka unaishia yapo yaliyoenda sawa na yapo ambayo yamezidi kwenda kombo, hapa nazungumzia ulimwengu mzima wa Digital tv, ulimwengu ambao umekuja na fursa kwa namba kubwa kwetu sisi vijana lakini pia kuna changamoto ambhata ambazo zinawakabili wote wanaohusika na mulimwengu huu wa Digital tv... zipo zilizopata utatuzi na zipo ambazo zinaonekana zinaenda kutatuliwa na hapo hapo zipo ambazo hata dalili kama zitakuja kutatuliwa hakuna... Mimi na team yangu kila kukicha tunajitahidi kuwa tofauti na wengine, yaweza kuwa walitutangulia ama wametukuta.. tumelifanya hili kwa uchache ingawaje pongezi tunazozipata inaonyesha walionufaika ni wengi sana kupitia uwanja huu..
Panapo majaaliwa mwakani tutafanya makubwa zaidi na kuwafikia hata ambao hawana uwezo wa kufika humu sisi tutawafikia.!!


 #MustaphaMaDish na zao lake #FundiMakini
Hivi kweli Fundi unafanyaje kazi chafu kama hii!!?? kuna baadhi ya mafundi wengine wamepata ajira kabisa makampuni makubwa yenye kuendesha huduma hizi za Digital tv lakini wanafanya kazi chafu na wanafikia hatua ya kupiga picha na kuzipost kwenye mitandao... mimi ama sisi huwa tunawaita kina #FundiKalipua mbioni kuja na Signal Quality tv
 
Aliyefunga hapa ni #FundiKalipua sio #FundiMakini Toka #MaDishTechnology
4:32 AM   Posted by Mustapha Hanya in , with No comments
Soma zaidi
 Eneo ni Hotel ya Sea Cliff ndani ya mgahawa wa Karambezi, robo 3 ya wateja wa mgahawa huu ni ngozi nyeupe na lugha itumikayo kwa wengi wa wateja wa hapa ni kiingereza na hivyo hata mazingira huwa kama sio Tanzania hivi...
Kwa mwezi wa 10 imekuwa ni sehemu ambayo nimetembelea zaidi ya mara 12 kwa nyakati tofauti ingawaje ilikuwa tunakula na kunywa lakini kikubwa ilikuwa ni kwa mazungumzo maalumu ya kikazi zaidi isipokuwa kwa sura nyengine na siku ya 12 mtu wa mwisho kufanya nae mazungumzo alikuwa ni Gabo na Deo.
Naweza kusema kila jambo ama hatua upigayo shukuru Mungu kwakuwa yeye ndiye anayekuwezesha!
Alhamdullah!mustaphamadish@gmail.com

3:40 AM   Posted by Mustapha Hanya in with 1 comment
Soma zaidi

Nov 5, 2017


MFALME WA BURUDANI ZA FAMILIA
Offer hii inakupa unafuu kama ifatavyo:-
 • Kwa Tsh 78,000 StarTimes ya Dish - Unapata vifaa pamoja na kifurushi cha mwezi mmoja.
 • Kwa Tsh 34,000 Decoder ya Antenna.
 • Ufundi Tsh 30,000 Startimes ya Dish.
 • Ufundi Tsh 20,000 Startimes ya Antenna.
 • Vifurushi vya Startimes Bofya Hapa
King'amuzi cha Startimes kinafanya vizuri sana kwa Offer mara kwa mara hutoa offer na zawadi kem kem hii ni katika kufanya wateja na wanaotaka king'amuzi hiki kupata ahueni!
Kwa Maelezo zaidi +255789476655 
1:17 PM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment
Soma zaidi

Call +255789476655

 • Text +255759091445

Follow

Search