Jul 7, 2014

Sababu iliyonileta hapa

  Baba yake na Fetty

Moja kati ya wanafunzi wangu wa kwanza kwanza kuwapa ujuzi huu ni huyu ambaye anaitwa Dullah kwa sasa amekula ajira pale Multichoice Tanzania ( DSTV ).
Kutoka ku moyo najisikia faraja sana kuona nasababisha mtu au watu fulani hasa vijana wenzangu kupiga hatua moja juu ikiwa kwenye kutengeneza maisha yake na familia yake kwa ujumla!
Nashukuru hakuna aliyenisahau ijapokuwa si wote kati ya wanafunzi wang ambao tunawasiliana mara kwa mara,najua ubize unaweza ukawa umechukua nafasi yake ama mambo ya hapa na pale.
Kwanini nimemzungumzia Dullah kwasababu hii kazi ya leo ilikuwa yake,mteja alimpigia mara kadhaa kwa siku tatu lakini muda wa Dullah ulikuwa mdogo hivyo kutokana na ushirika mzuri ndipo akaileta mezani kwangu ili tumalize tatizo la huyu mteja!
C band hii si ile iliyozoeleka na mafundi wengi ft6 ama ft8 hii ni ft12.
Nami nilienda nikijua ni ft6 kama ambavyo Dullah alidhani,hata spana ilinilazimu kurudi tena ofisini kuchukua kwa maana zile nilizobeba hazikuwa na uwezo wowote wa c kufungua hata kufunga tu.
Hapa angeenda ndugu yangu lazima angehitaji twende sote kwa maana Dish hizi zinahitaji uwezo wa ziada!
Kwanini naitwa MUSTAPHA MADISH ndipo nikadumisha umwamba wangu kisha tukachapa mwendo!
1:00 AM   Posted by Mustapha Hanya with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Umetisha sana kiongozi haya dhihirisha umwamba wako!

Anonymous said...

Fanya yako kaka upo juu sana mpaka naogopa kukutafuta kwa huduma bei zk c zitakuwa juu sana!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search