Jul 8, 2014

NILIYONAYO KWAKO...

 Baba na Mwana
Nawasikitikia sana wale wanaopiga mechi za kikubwa kisha wanakimbiana,sababu zikiwa nyingi zisizo hesabika huku mwanamke akibaki mjamzito,ujauzito ambao mwisho wake unakuwa sio mzuri sana kwa maana wapo ambao wanaamua kutoa..hapa kwenye kutoa wapo waliofanikiwa kuchota dhambi kwa wingi na wapo waliopoteza maisha wakiwa katika kutimiza hilo!
Pia wapo waliamua kwa dhati kujifungua huku akijua yeye ndiye atakayekuwa baba na yeye ndiye atakayekuwa mama..
Kwa hili wapo waliofanikiwa wachache sana ila wengi wamefail kwa kukimbilia kutoa ama kuzaa na kushindwa kumuangalia mtoto kwakuwa yupo pekee yake..
Matokeo yake idadi ya watoto wa mitaani inaongezeka...
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa angalizo wanawake na waschana wote kwa ujumla Mwanaume,
mimi ikiwa mmojawapo niliyeandika post hii,tuna salio la uongo la kutosha lisilopungua kukudanganya wewe ili tu niingie panapofanya wewe ukaitwa mwanamke..
Bahati mbaya hata muambiwe vipi uelewa wenu wengi wenu ni tatizo,tena tatizo kuwa..
Ila alau hata kwa mwezi mara tatu ama mbili si vibaya tukazungumza alau kukumbushana tu kwa yale machache niliyonayo kwenu wapendwa!
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

upo sahihi sana kiongozi

Anonymous said...

Ukiwajali pengine inaweza ikasaidia japo kwa uchache!
Hongera

Anonymous said...

Mwanamke ni mtu wa ajabu sana na sijui kwanini wnashindwa kujielewa ni rahisi kudanganywa na hata ukimtakia mema ye anajua unambania tu so sijui tunawasaidiaje!

Anonymous said...

Mbna umechelewa waache tu cz ndo wamejiamulia..