Nov 8, 2014


Hapa nazungumzia wale ambao wapo kitambo na ambao wamejiunga hivi karibuni ama hata kama unataka kuingia ukanda huu kwa mikono miwili nakukaribisha na hii post inakuhusu sana zaidi ya yote ukiyachukua yangu na kuyafanyia kazi majibu utanirejeshea!
Ufungaji wa Dish ya Azam tv..
Hivi karibuni nilikuwa pale Tandika Flat,katika ile huduma piga simu tunakufata ulipo..
Ilihitajika Azam tv nasi tukatekeleza,tulipofika kazi ikaanza kwa kuangalia pa kufungia Dish kwanza haikuwa tabu kwakuwa tayari dish nyengine tena zikiwemo Azam tv zimeshafungwa, na ndipo nikapata hii post..


Hii ni kazi ya Fundi ambaye anapewa dhamana kama ambavyo napewa mimi na wateja ila matokeo yake kinachofanyika ni kulipua kama hivi ili tu picha ipatikane ndani biashara imeisha!
Nikaona nifunge hapo hapo ili hata kama naye ni mpitiaji humu aone alichofanya alau nafsi itamsuta na kuona alivyoitendea taaluma ndivyo sivyo na mteja wake pia huku wengine mkijifunza msije kuwa kama mafundi hawa!

Ona kazi ya Mustapha MaDish...


 Tofauti hata kwa macho inaonekana!

 Ugumu upo wapi kufanya hivi..

 Angalia na uyafanyie kazi..

 Tofauti ya kazi zangu na wengine..

 Sababu ya kuitwa Mustapha MaDish..


 Setting zikiendelea..

Baada ya kudrill..

Nikiwa nimeachana na hiyo issue ya Azam tv,nikakumbuka kituko kingine nilikutana nacho Kimara,nikiwa katika huduma yangu ile ile ya PIGA SIMU TUKUFATE ULIPO..
Safari hii sio Azam tv tena...
Ufungaji wa Dish ya DStv...
Kwakweli hii ni kituko,hivi nawe mteja kabisa unakubali kazi ya fundi wako hivi!!??
Ambacho kilichofanya mpaka nianze kumshangaa mteja kwakuwa ndipo mlango wake ulipo maana yake ili aingia nyumbani kwake lazima apitie lilipo hilo dish,jibu lake ameridhika ama!?
Kiukweli kama ningemkuta wala nisingevumilia ningeongea nae mawili matatu kuhusu hilo dish...

Ona kazi ya Mustapha MaDish..


Ustadh nae...

Wale mafundi nonihino wado waliendelea kunishangaza...
Ufungaji wa Dish ya Zuku...
Palee Flat za Ubungo ndipo nilipokutana na ufundi huu..
ukipiga upepo kweli jamani hii Dish haiondoki kweli!!??
Bahati mbaya ama bahati nzuri ukifanyakazi katika hizi flat mara nyingi unapewa mwenyeji wa kuwa nae unapokuwa juu,swali je mwenyeji wa huyu fundi aliifurahia hii kazi!!??

KAZI SAFI | MAFUNDI WAZOEFU | DISH AINA ZOTE | PIGA 0789476655

7 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kaka tunakosa huduma zako huku mikoani,fanya uwe unatembea tembea ili kuwaonyesha mfano mafundi wetu huku.

Anonymous said...

Ni moja ya sababu inayonifanya nisiache kupita angalau kwa siku mara moja hii blog kwangu ni CHUO

Anonymous said...

NAHITAJI SANA HUDUMA ZAKO ILA SIJUI KAMA NITAMUDU COST ZAKO!

Anonymous said...

SHIKAMOO MWALIMU

Anonymous said...

Naomba niwe mwanafunzi wako!

Anonymous said...

Napenda unachokifanya umekuwa msaada mkubwa sana kwangu ,awali sikuwa nategemea kama ungeweza kunisadia kwakuwa nilishakosa msaada kwa wahusika wakuu mungu akubariki sana mkuu.

Unknown said...

Kaka hii imeenea hadi huku mkoan niliko nikikutumia picha utashangaa,mm nifundi pia lkn wateja nao pia wanachangia kaz kuwa mbaya wanatafuta fundi wa bei ndogo, lkn mara zote nagombana na baadhi ya mafundi wenzangu kwann ukubali kufanya kazi ya bei ndogo huku mwingine akiitwa wa gali?huoni kuitwa wew kwa bei ndogo nikwamba kiwango chako cha kazi sio?zidi kupaza sauti kaka huku tumechoka!!!!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search