Nov 19, 2015Yapo mengi ambayo siwezi kuyamaliza kwa siku moja na pia siwezi kuyamaliza ikiwa sijajua ambacho wewe ungependa kujua kuhusu ulimwengu huu wa Digital tv na hata ukihitaji kujua yale ya Analogue tv nipo tayari kukujuza kwa kina kabisa!
Ni nini ambacho ungependa kukijua yawezekana kuhusu king'amuzi chochote kati ya vilivyopo Tanzania ama vinavyotumika Tanzania ingawaje ninauzwa nje ya nchi.Hata kama swali halihusiani na ving'amuzi ila tu linahusiana na ulimwengu huu wa Digital tv nnachoweza kusema karibu alau tuwekane sawa.

NIULIZE:
  • Chochote ambacho ungependa kujua ikiwa kutokea kule tulikotoka Analogue tv ama hapa tulipo Digital tv.
  • Jambo lolote la kiufundi ambalo linakutatiza katika ving'amuzi vyote vilivyopo.

Ili na wengine wanufaike na majibu ya maswali yatakayoulizwa naomba muulize kwenye sehemu ya ku comment nami nitajibia hapo ili maswali yasijirudie!
11:20 PM   Posted by Mustapha Hanya with 17 comments

17 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Nini maana ya fta?

Anonymous said...

Free to air channel

Anonymous said...

Baada ya setelite ya contnental kupotea kwa takriban wiki sasa. Tunasikia kwamba wamejiunga na setelite nyingine. Je naweza kupata frequency zake mpy?

Mustapha MaDish said...

Nini maana ya FTA?
-Maana yake kuna mdau amejaribu kunisaidia hapo kuwa ni Free to Air channel ila kwa lugha nyepesi ni channel za bure,hizi channel zipo nyingi kwenye Satellite nyingi tu huko angani ila kupitia ving'amuzi vyetu channel hizi wamezilenga zile channel za nyumbani ambazo ni za bure ijapokuwa si ving'amuzi vyote wanazoziachia kuwa za bure,kwa maana malipo unayolipia kupitia kifurushi ulichochagua yakiisha nazo zinakata hivyo hii haileti maana ya FTA.
Ili upate FTA ni lazima utumie Satellite Dish Antenna ili kulenga Satellite fulani kwa ajili ya kupata FTA zile ambazo unazihitaji huwa hazina malipo kabisa.

Mustapha MaDish said...

Continental Decoder wanashida ni kweli na kusema kwamba wamehama sio sahihi ila kwa tatizo linalowakabili kuhama ni lazima ijapokuwa mpaka sasa bado haijajulikana watahamia wapi ijapokuwa mtazamo wangu...
Tatizo lililowapata Continental limewapa pia Ting kwa maana tatizo limetokea kwenye Satellite ya Amos 5,Satellite ambayo inatumiwa na makampuni mengi tu sio hapa Tanzania pekee Duniani kote wanaotumia Satellite hii hili limewakumba.
Satellite ya Amos 5 haipo tena kwasasa imepotea.
Nafasi hii toka kwangu nawapa pole wadau wote wa Amos 5.

Mike Mshanga said...

Vipi kiongozi umeshawahi kufunga lnb 4 za c band ktk 1 la ft 6 ? Nataka mtu wa kunifungia kwa ajili ya kunasa sate hizi ...intelsat20,17,906,na NSS 12. VERY SOON.

Anonymous said...

Yale madish makubwa hayafanyikazi kwasasa?

sharifu rajabu said...

Vipi kaka menunu digital TV LG 42lb6520-TB.
Nimeiconnect na antenna ya star times hizi za yagiuda antennae
Nikisearch channel napata kama 100. inayo ni moja to ya ST guide

sharifu rajabu said...

Chanel nyingine kama tbc tv1 clouds nkiselect inanpa message kua ni invalid service. Na chanel ambazoambazipo nje ya nchi naambiwa scrambled. Msaada jaman nipo arusha.

sharifu rajabu said...

Menununua digital tv lakin napata chanel moja to ta st guide

Anonymous said...

Vip kk

Anonymous said...

Unapatikana mkoa upi?

Erick Kalaliche said...

Nimesetiwa ting ila napata chanali za nje tu sipati za ndani,nipo Arusha

Erick Kalaliche said...

Nimefungiwa dishi la ting ila sipati chanali za home shida ni mini?

Erick Kalaliche said...

Nimefungiwa dishi la ting ila sipati chanali za home shida ni mini?

Erick Kalaliche said...

Nimesetiwa ting ila napata chanali za nje tu sipati za ndani,nipo Arusha

hudsson75 said...

Habari.mimi nina LG smart tv ambayo ina uwezo wa kurecord na kuriwind live tv lakini ikiwa imekonektiwa kwenye RF PORT.Je kuna namna yoyote ya kuconnect kutoka kwenye king'amuzi kwenda kwenye RF PORT ya TV?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search