Dec 3, 2015

 Lawama zimekuwa ni nyingi kuhusu Ving'amuzi kusumbua,ambapo Ving'amuzi vinavyolalamikiwa wala havina usumbufu huo,katika kuchunguza nimegundua ya kuwa mafundi husababisha Ving'amuzi vionekane vinasumbua hata kama havina sifa hiyo ijapokuwa kweli kuna Baadhi ya Ving'amuzi vinasumbua ukiachilia uwezo wa fundi..
Baadhi ya Dish nilizowahi kukutana nazo na nikabahatisha kupiga picha ni hizi hapa chini:-

 Dish ya ZUKU tv
Badala ya fundi kutoboa na Drill yeye alichofanya ni kutafuta mawe na mbao na kufanya alichofanya kama ambavyo macho yenu yanaona hapo,matokeo yake kila baada ya muda mfupi picha itakuwa inakata kata ama hata kupotea na matokeo yake fundi hakauki kwako mwisho wa siku king'amuzi hiki kinasumbua!
 Hizi ni Dish za Azam tv
Nilikutana nazo pale Ubungo National Housing,hii ya mbele ndio mpya kwa muonekano na ya kule mwisho ya siku za nyuma kidogo,kilichofanyika hapa ni kile kile uzembe wa fundi wa kutokutoboa na Drill!

Alichofanya fundi ni kutafuta misumari ya zege na kugonga mpaka nadhani alijibonda midole kwa maana zege hili sio la kitoto..

 Baada ya kukata misumari kadhaa maana ulishindwa kuingia wote akaonelea atafute vitu vya kuweka ili kuweza kukaza kwakuwa msumari hauwezi kuingia wote,juu ya kichwa cha msumari kumewekwa bolt kwa ili pia kuweka mkaze ambao haijasaidia chochote..

 .....!!

 Kwakuwa kazi yote aliyoifanya haijasaidia kitu fundi huyu akaonelea atafute na kamjiti ili kuizuia Dish hii isishuke na kupoteza signal..

 Fundi wetu huyu akamalizia kwenye kuchomeka cable kwenye lnb,ukiachilia uchafu alioufanya hapo pia kuna kitu hajakifunga hapo ambacho kazi yake ni kufunika kabisa hayo maungio ya hiyo cable,je unayajua madhara ya ufundi huu..!!??

 Kazi ya fundi hiyoo...!!!

 Yametafutwa mawe yalipo yakapangwa kwa uchungu ili kuhakikisha signal zinapatikana na hazipotei..
Ah jamani kweli hii hata hujisikii vibaya bwana fundi..!!??

 Ile ya zege ikagongwa hapa kwa mbwembwe balaa..

 Hivi mteja wako unayemfungia ameona kazi hii?

Hii ni maeneo ya Kimara ila hii cha ajabu ni kwamba ilipofungwa mteja anaona kila kitu jinsi ilivyo sasa ambacho nimeshindwa kuelewa ameridhika na uchafu huu ama vepe!
 Hii ni Dish ya DStv

 Macho yako yameona nini hapo...!?

 Ni wazi kuwa ukuta huo haufai kubeba hii dish ila alichofanya bwana fundi akatumia ufundi wake kuonyesha yakuwa hata kama ukuta haufai yeye anauwezo wa kufanya ukafaa..

 Fundi na ufundi wao..!

 Hapa uhakika wa signal hakuna kabisa...

 Hii nadhani inatokea kwa mafundi dish wa Tanzania tu!


Hapa utalaumu King'amuzi unachotumia ama fundi aliyekufungia?
Nnachoweza kukusihi angalia sana kazi anayokufanyia fundi wako zinafanana na hizi?
JE UNAHITAJI FUNDI KWENYE KAZI SAFI TOFAUTI NA UCHAFU HUU KWA AJILI YA KING'AMUZI CHOCHOTE UNACHOKIJUA WEWE?
PIGA +255 789 4766 552:38 AM   Posted by Mustapha Hanya with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kaka huu kweli ni uchafu ubarikiwe sana na mungu akuweke miaka mingi ili uendelee kutupa mautaalamu

Anonymous said...

Wengine Ni shida mi nilikua mtaalam WA kufunga madishi lakini baada ya kuona taaluma imeingiliwa na wanaofanya uchafu kama huo nimebadili fani wanachafua wataalam,

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search