Apr 12, 2016


Leo nimeonelea niongelee hili jambo kwakuwa ukiachilia kuliona sehemu mbali mbali pia nimekuwa nikulizwa kama kuna umuhimu wa wenye ving'amuzi vya madish kuweka makopo?
 Jambo la awali la kuzingatia king'amuzi kiwe cha Dish ama Antenna kina namna ya ufungaji wake kwa kutumia vifaa vyote vilivyomo kwenye set ya king'amuzi hicho,ikitokea kimojawapo umekiacha ndipo unajikuta nafasi ya kile ulichokiacha inachukuliwa na KOPO!
Kutumia KOPO kunatokana na sababu hizi:-
  • Tuanze kiufundi
- Fundi hupaswi kuacha kutumia kitu chochote kati ya ulivyovikuta kwenye set ya Dish kwakuwa vyote vina kazi yake na ni muhimu sana.

Hapa unamshawishi mteja atafute kopo lilipo ili aweze kufunika akiamini atasaidia angalau kuepusha gharama za kuita ita fundi.

Ukifunga hivi ni kipi ambacho kitamshawishi mteja aongezee ufundi wake wa kuweka kopo?
Fikra za watanzania wengi wanaamini wakifunika na kopo husaidia:-
  • Huzuia kunguru kufanya uharibifu
  • Husaidia picha kutokupotea wakati wa mvua
Niseme tu ukweli KOPO halisaidii chochoteikiwa fundi amefanyakazi safi.
Kupotea kwa Picha kwa dish ndogo kipindi cha mvua ni kawaida kutokana na uwezo mdogo ili kuepuka hili inakulazimu kutumia Dish kubwa ama lnb maalum na kuhusu kunguru fundi akifanyakazi yake vema kunguru hata abembee vipi hawezi kufanya uharibifu!
mustaphamadish@gmail.com

3 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hili somo nimelipenda kwakweli nashukuru mkuu endelea kutuletea hii elimu!

Anonymous said...

Mkuu naomba unifahamishe amc channel za free napata kwenye sat ipi?

Anonymous said...

JE KUNA UWEZEKANO WA KINGAMUZI KIMOJA KUTUMIKA KWENYE ZAIDI YA VYUMA VITATU NA KILA CHUMBA KIKAWA FREE KUCHAGUA CHANELI WANAZOTAKA KUANGALIA TOFAUTI NA VYUMBA VINGINE? KAMA NDIO INAWEZEKANAJE?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search