May 31, 2017

UFUNDI UNAHITAJI UMAKINI

Kwanza ukishakuwa Fundi moja kwa moja unaaminika kwa taaluma uliyonayo hivyo mteja ama jamii kwa ujumla wanajikuta wanaona unachofanya ama kusema ndicho sahihi kutokana na wadhifa wako hata kama ni cha uongo… Binafsi niwape angalizo wateja na mafundi kiujumla kwanza nianze na Wateja

Wateja – Nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wale wote wanaoheshimu na kuthamini uwepo wa Mafundi . Pia nichukue nafasi hii kuwapa angalizo wale wateja wote wenye Dharau kwa kuona Mafundi si chochote ama kudharau kile tufanyacho,Mfano mteja anahitaji fundi mnazungumza habari za gharama na mnakubaliana,fundi anafika kwako na anafanyakazi yake kwa muda mchache anamaliza kutengeneza..Mteja kwenye malipo unataka upunguziwe kwakuwa kazi yenyewe ndogo tu ,hii ndo dharau nisiyoipenda hata kuisikia.. sasa kama kazi ni ndogo tu kwanini hukufanya mwenyewe!? Hivi hujui kwanini imekuwa kazi ndogo tu!? Kwakuwa ni Fundi ( Ufundi ni taaluma ) si kila mtu ana taaluma na ndo maana ukahitaji Fundi.. Hivyo tumia lugha nyengine katika kutafuta unafuu wa malipo lakini si kudharau kazi za watu. Mpe uhuru fundi afanye kazi yake si kumbana hata anakosa kuwa comfortable maana fundi akiamua kukufanyia uhuni hata ukienda nae mguu kwa mguu ana nafasi 99% ya kukufanyia uhuni.

Mafundi – Lazima ujielewe kama si kuelewa thamani yako,ujue uwezo wako pia maana kuwa Fundi si kigezo cha kujua kila kitu ingawaje wapo mafundi kwa taaluma yake anajua kila kinachomuhusu.. hii maana yake kama umekutana na Technical issue ambayo kwako ni ngeni omba msaada kwa mafundi waliokuzidi ama ukikosa msaada mwambie mteja wako ukweli kwamba hilo tatizo huwezi kulisolve.. Kamwe usiseme uongo ili tu upate pesa.. Hakikisha unakuwa makini katika kazi yako,akili yako uiweke kwenye kazi uifanyayo wakati wa kazi ili isitokee ukafanya usahaulifu wowote maana utakuwa ni uzembe na matokeo yake itakucost ila zaidi itamcost mteja wako… mfano hii picha hapa chini


Kosa dogo alilofanya limesababisha huu mkono wa dish la DStv kuliwa na kutu kwakuwa hakuweka kifuniko ambacho kinazuia maji kuingia ndani ya mkono huu wa kushika Lnb..

 hili ni kosa dogo kimtazamo ila kiufundi ni kosa kubwa sana linaweza likawa limefanywa na fundi kwa bahati mbaya ama kwa makusudi kwa kudharau vile vifuniko vya kufunikia hii mikono.. Amedril vizuri na amefunga cable vizuri lakini kilichomshusha vyeo kuonekana ni fundi kalipua ni kosa moja tu…


Tuna Mafundi wataalamu wa kufunga

 •   Azam TV
 •   DStv
 •   Zuku Tv
 •   StarTimes
 •   Continental
 •   Ting
 •   Flat Screen
 •   Projector
 •   CCTV Cameras

Waliobobea kufunga kwenye:


 •       Hotel
 •       Apartment
 •       Bar
 •       Restaurant
 •       Office
 •     Majumbani

 Tunapatikana Dar es salaam, Magomeni Mapipa.. isipokuwa mkoa wowote Tanzania tunakuja.. inategemea unataka huduma gani toka kwetu!


Piga +255678476655
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: