Imenipelekea kuandika post hii kutokana na simu niliyoipokea hivi karibuni kutoka Dodoma,lakini kabla ya simu hiyo kuwaelewesha wadau wangu kuhusu HDMI CABLE ni kawaida tu ila kwenye hii blog yetu leo wacha nitoe kile kidogo nilichonacho kwa wadau wangu!
Unapozungumzi HD
lazima ushirikishe cable inayoitwa HDMI CABLE,kwasababu ili uone picha katika mfumo wa HD ( Ubora wa picha wa hali ya juu ) ni lazima utumie HDMI CABLE,cable ambayo inatoa picha kutoka kwenye inaweza kuwa DVD/Receiver/King'amuzi ama chochote chenye uwezo wa kutoa HD na kupeleka kwenye tv ambayo nayo ikiwa ina uwezo wa kupokea HD.
Hii cable inachomekwa kwenye tundu lililoandikwa HDMI.
Ili kujua kama tv/DVD ama king'amuzi chako ni HD unapaswa kuangalia kwa umakini je kuna tundu lililoandikwa HDMI,kama lipo hilo jua kifaa chako hicho ni HD.
Je unavijua ving'amuzi vilivyo kwenye mfumo wa HD hapa Tanzania..??
Una swali piga +255789476655