Dstv ni wakongwe hii haina ubishi,ila ukongwe wa dstv haina maana kuwa hakuna king'amuzi ambacho kinaweza kuja na kufanya vizuri zaidi yake,hii inatokana na kwanza kujua mahitaji ya watazamaji kwa ujumla na kuwatimizia kile wanachokihitaji,unafuu wa bei ukizingatiwa.
Azam tv ni king'amuzi kipya kati ya vyote unavyoviona ila ndio king'amuzi kinachokimbizana na wakongwe,kwanini? kwasababu wameangalia watazamaji wanataka nini na kwa unafuu pia..Ingawaje Azam tv haijakidhi mahitaji wa wadau kwa 100% lakini alau wameweza kwa ukubwa.
Wadau wengi ni wapenzi wa mpira hivyo Azam tv wamefanikiwa kwa mpira wa Tanzania na Dstv bado anang'ang'ania ukongwe wake kwa mpira wa nje.
Ving'amuzi hivi vina mapungufu yake na kinachowakera wengi ni haya hapa:-
-Kubwa linalolalamikiwa na watanzania wengi ni bei kuwa juu,nikimaanisha malipo ya mwezi na hii inachangia na mtindo unaotumika wa kutumia $ badala ya Tsh.
Madhara ya kuwa bei juu kumefanya wadau watafute kila aina ya njia kuona wanapata uhondo wa dstv ila kwa njia isiyo rasmi,na hii inapelekea kupunguza walipaji halali wa malipo ya mwezi.
-Wana local channel,lakini malipo ya mwezi yanapokata hawaziachi zikawa bure.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Dstv.
MAPUNGUFU YA AZAM TV
-System wanayotumia kushindwa kutambua malipo ya mwezi wanayolipia wateja na kufunguka badala yake ukilipia kifurushi ukipendacho mpaka upige simu,hii imekuwa kero kwa wateja wengi wa azam tv,mteja anakaa mpaka wiki mbili na ikitokea hapigi simu unapita mwezi pasi kuona kile kifurushi alicholipia.
-Mawakala na wauzaji wengine wasio mawakala kuuza bei tofauti na bei sahihi.Hii sio tu mikoani ijapokuwa mikoani lawama hizi ni kubwa lakini hata hapa Dar es salaam wapo wanaouza bei juu tofauti na matangazo yalivyo.
-Picha kupotea kipindi cha mvua,king'amuzi ambacho kinaongoza kwa kupotea signal wakati wa mvua ndogo tu,hii ni kero nyengine kubwa kwa wateja wa Azam tv,kitaalamu hii inatokana na signal kuwa chini hivyo ni jukumu la Azam tv kuongeza signal badala ya 60 zifike alau 80 lakini kinachotakiwa mfikishe 100.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Azam tv.
TOFAUTI KUBWA KATI YA DSTV & AZAM TV
Dstv ana huduma zaidi ya moja kama:-
Extra view-Inakuwezesha kuona channel mbili tofauti kwa tv mbili tofauti kwa a/c moja.
Explora-Inakupa fulsa ya kurecodi saa 150 na mengineyo.
Umiliki na utofauti wa channel.
Dstv inaonyesha mpira wa nje na Azam tv mpira wa ndani.
MUSTAPHA MADISH | +255789476655 | mustaphamadish@gmail.com
1 Unasemaje..??:
Azam walianza vizuri sana kwa kusema kweli lakini wanachotufanyia sasa ni dhahiri kwamba wanatushawishi tuendelee na ving'amuzi vyengine,dstv nayo inautamu wake hasa kipindi cha mpira ,katika kumalizi vyote vinaubora katika huduma zake isipokuwa swala la kila leo kupanda bei za vifurushi vya azam mnatuchosha...
Post a Comment