Swali la wengi kwasasa ni hili kutokana na ukweli kwamba uondoshwaji wa local channels kwa baadhi ya Visimbuzi imekuwa kama janga hivi.. Sasa niwape namna ya kujua jinsi gani ya kupata local channels kupitia tv ikiwa ina kisimbuzi ndani, inaweza ukatumia Antenna ama Dish inategemea na uwezo wa tv:-
Utajuaje kama tv yako ina kisimbuzi ndani?
- Ingia kwenye INPUTs inategemea na brand, zipo ambazo zinatumia SOURCE, INPUT n.k unabonyeza na itakuletea orodha ya input zote mfano:-
HDMI1
VGA
USB
ATV
DTV
Ukiona ina DTV ujue ina kisimbuzi.
- Njia nyengine unachukua remote yako unabonyesha kwenye SETTING unaenda kwenye SEARCH hii nayo inategemea na tv, tv nyengine hutumia tune n.k hapa unaweza ukaweka AUTO SEARCH itakuletea Analogue tv na Digital tv ikikuletea hizo chaguo ujue tv yako ina kisimbuzi ila kama itakuletea Analogue tv pekee ujue haina kisimuzi..
Kuna DVB T1/ T2 hii ni kwa ajili ya antenna.
Kuna DVB S1/ S2 hii kwa ajili ya dish.
Insta @mustaphamadish
Whatsapp+255784378129
Whatsapp+255784378129
1 Unasemaje..??:
Mbona huku kwetu hamjapita nasi tuna maswali yetu tunataka mkurugenzi atujibu.. kwanini hamtoi offer mwisho wa mwaka kwa wateja kama ilivyo ving'amuzi vyengine
Post a Comment