Nimejaribu kufatilia kwa ukaribu sana utaratibu wa kufanya malipo ya king'amuzi kati ya watumiaji wageni nikimaanisha wenzetu rangi nyeupe na sisi ngozi nyeusi ijapokuwa si wote isipokuwa wengi wetu tuna utaratibu mmbovu sana wa kufanya malipo ya ving'amuzi tunavyotumia...!!
Mfano ukute mzungu/ama muhindi utaratibu wake wa kulipia, mfano amelipia king'amuzi anachotumia tarehe 10 mwezi wa 11, atalipia tena siku mbili ama tatu nyuma kwa mwezi unaofata, anaweza akalipia terehe 7 ama 8 ama 9 mwezi wa 12 ambapo hukuti anapata usumbufu kuhusu malipo na uzuri zaidi ving'amuzi karibu vyote vina utaratibu wa kukutumia ujumbe tena kwenye king'amuzi chako ya kwamba kifurushi chako karibu kinaisha hivyo ufanye malipo mapema!
Wengi wetu sie kina ngozi nyeusi kama nimelipia tarehe 10 mwezi wa 11, sitafanya malipo mpaka kifurushi kitakapokata kabisa matokeo yake unatokea usumbufu wa hali ya juu.. wakati mwengine inaweza ikawa kipato hilo ni sawa siwezi lipinga ila hupaswi kungoja mpaka siku ya mpira ndipo ufanye malipo kwa maana mara zote siku za mipira sio Azam sio DStv huwa system zao zina elemewa na matokeo yake unapata maudhi usiyoyategema ambapo ungelipia siku moja ama mbili kabla ya mpira unaotaka kuangalia usingepata usumbufu hata kidogo!
Tujitahidi kubadilika wadau wa ulimwengu huu wa Digital tv... Kwa hili naomba niwe mkweli ikiwa utalipia siku ya mpira na ukatafuta msaada umekosa hata mimi na managment yangu hatutakuwa na msaada ila kama utalipia siku 2 ama 1 kabla ya mpira msaada utaupata toka kwetu kwa king'amuzi chochote kile.
Kwa maelezo zaidi.....
- Umelipia na bado hupati picha bofya hapa
- Unataka kuhama kifurushi bofya hapa
- Una tatizo la kiufundi bofya hapa
+255789476655
Whatsapp+255784378129
2 Unasemaje..??:
Mkuu simu haipokelewi!
Mbona hawa azam tv simu zao ukipiga zinakata tu hakuna mkuita hakuna msaada wowote!
Post a Comment