LNB ni nini?
LNB ama kwa kirefu chake ni Low Noise Block downconverter, ni kidubwana,kifaa kidogo kinachokaa kwenye dish ambacho kinapokea signal toka kwenye satellite na kupeleka kwenye satellite receiver ( King'amuzi kinachotumia dish ). Pia huitwa low-noise converter (LNC), au low-noise downconverter (LND), hiki kifaa wakati mwengine kinaitwa low-noise amplifier (LNA).
LNB ni mchanganyiko wa low-noise amplifier, frequency mixer, local oscillator na intermediate frequency (IF) amplifier. Inapokea microwave signal kutoka kwenye satellite iliyokusanywa na Dish, inaimarisha, na inachagua mzunguko wa mzunguko kwenye upeo wa chini wa mzunguko wa kati (IF). Hii downconversion inaruhusu signal kuletwa ndani kwenye Satellite receiver kwa kutumia Coaxial cable. ikiwa Signal ilibaki katika asili yake microwave frequency ingehitaji gharama kubwa na impractical waveguide line.
LNB kwa kawaida ni kisanduku kidogo kinachofungwa mbele ya uso wa dish kwa kutumia mfano wa fimbo ( kibomba/ vibomba ). Microwave signal kutoka kwenye dish inachukuliwa na feedhorn kwenye LNB na hutolewa kwa sehemu ya waveguide.
LNB hufanyakazi kwa kutumia umeme ambao utatokea kwenye Satellite receiver kwa kutumia coaxial cable na huchomekwa sehemu iliyoandikwa LNB IN ikiwa imetumika pin katika kufanya coaxial cable kufunga kwenye Receiver na kwenye LNB pia.
AINA ZA LNB
- Ku band
- Ka band
- C band
+255789476655
Whatsapp +255784378129
2 Unasemaje..??:
Naomba utupe somo kwanini LNB zinakufa na je kufunika kopo kunasaidia kuilinda LNB?
Ni kwasababu kisiweze kuharibiwa na ndege pamoja na mvua!! Ndo maana kinawekwa kopo
Post a Comment