Call / WhatsApp +255755949413

Dec 18, 2010

AV selector

Kuna TV nyingi ambazo zina AV moja ama mbili na mtumiaji akawa ana vya kuchomeka zaidi ya viwili.
Mf: ana DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na Game labda,hapo hapo TV yako ina AV moja ama mbili hivyo itakuwa inakulazimu kuchomoa na kuchomeka kila muda ambao unataka kuangalia kimojawapo kati ya hivyo,ambapo itakuwa usumbufu licha ya hivyo pia ile kuchomoa chomoa kila wakati AV cable ni rahisi kukatika.
Napenda kukujuza ambacho labda ulikuwa hukijui....!!
kuna kitu kinaitwa AV selector kazi yake ni kuunganisha vyote kwa wakati mmoja,nikiwa na maana ya kuwa kama ni DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na hata Game na vyote ukaona bila kuchomoa chomoa...!!


Kazi yako itakuwa ni kubadili kwa kubonyeza AV selector yenyewe kwa namba husika kwani katika kuchomeka kwako kutakuwa na namba kwa kila ambacho utachomeka kama DVD no.1,Receiver no.2 na vilivyobakia kwa mtindo huo huo hivyo itakuwa ukibonyeza namba 1 itaonyesha DVD,namba 2 Receiver na vyote kulingana na jinsi utakavyobadili.
Kuna AV selector ambazo zinatumia remote na zisizotumia,kuna za umeme na zisizotumia umeme,kuna kuanzia njia tatu na kuendelea.

Share:

Segerea ilikuwa pangu pa kavu....!!

Offer bado inaendelea nami nazidi kusababisha watu wafurahie maisha,nilikuwa maeneo maeneo wanapaita segerea ambapo nyuma ya nyumba hizi ndipo ilipo gereza la segerea.....!!
Hapa tatizo kubwa lilikuwa ni pa kufunga dish maana nyumba ilikuwa imejengwa kiaina yake,kwa kawaida ili dish likae kwa uzuri na usimwite fundi kila baada ya muda ni lazima tudrill ukutani lakini sometimes inakuwa haina jinsi kama ilivyo hapa na ndio tukaamua tufunge kwenye mbao ili tu mwenye yake aweze kuona kama yalivyo matakwa yake......!!
 Tumeangalia ubora wa mbao kama kweli unaweza kubeba dish na ndipo tukafunga maana unaweza ukafunga ile unaondoka tu unapigiwa simu ya kwamba dish lipo chini....!!









Share:

Dec 17, 2010

IZUNGUKE DUNIA UKIWA NA TV YAKO NYUMBANI.......!!

Unaweza kuona channel ya taifa lolote ambayo ipo katika satellite katika ukanda huu wa Africa mashariki,tunakuwezesha kupata kujua na kuona kila kinachoendelea up to date kana kwamba upo nchi husika,tunakufanya usiichoke TV yako zaidi ya yote utamani kuibeba ba kutembea nayo popote uendapo...!!
Kuwa wa kwanza kupata habari kwa kuangalia vituo vya kimataifa vya habari na utaweza kuburudika na kujifunza zaidi kwa channel za ndani na za nje clear bila chenga....!!


Share:

Dec 13, 2010

Buriani DR REMMY..........!!!

Kiukweli kila kukicha tunapoteza wakongwe katika fani,inasikitisha ila mwisho wa yote inakuwa hatuna jinsi kwa7bu tumezaliwa ni lazima tutakufa isipokuwa tunachogopa ni kutangulia tu....!!
Kifo cha DR REMMY kamwe hakitasahaulika na hakuna wa kuziba pengo lake,kila mtu atakumbuka kwa style yake ila kwangu mimi ni zaidi ya ambavyo wengi wanadhani...!!
Mimi ni kati ya wale watanzania wachache waliopata bahati ya kuzaliwa mjini tena ni maeneo ya sinza pale nyuma ya shule ya Mashujaa kiasi kwamba ukitoka tu nje unakutana na kanisa....!!
Hivyo nikisema hivyo wale ambao wanakumbukumbu nzuri watakumbuka enzi hizo yaani nyumba za hapo kulikuwa na muingilianowa watoto sana yaani hakukuwa na mipaka kwa jinsi tulivyoishi enzi hizo so watoto wa DR REMMY walikuwa home hawapungui nasi kwao kama kawa...!!
Ila tulikuja kuhama sinza mwaka 1993 ambapo ndo ukawepo umbali,kiukweli nimesikitishwa sana poleni sana wana wa familia ya DR REMMY na wapenzi wote wa mkongwe huyu ambaye alikuwa JEMBE.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,Ameen.
Share:

Dec 12, 2010

c channel zote zinazopatikana kwenye Dish

Swali ambalo daily nakutana nalo kwa kila ninapoinstall Dish hasa kwenye makazi ya watu....!!
Unafunga dish ndogo channel za Emanuel gospel mtu anaulizia local zinapatikana ngapi...??
Unafunga futi sita local mtu asipoiona C2C anahoji kunani...??
Hivyo ni vema ukajua unachotaka na utakachopata kabla hujahudumiwa....!!
Nimegundua ya kuwa wateja design hii ni wale ambao wameenda nyumba ya fulani kaona channel fulani nae wakati anataka huduma anataja ile channel aliyoipenda na kuiona bila hata kujua zimefungwa dish ngapi nje,na ndo maana tunaamua kutoa darasa kabla ya kumuhudumia mteja nawe kuwa huru kuuliza...!!
Share:

Week end ndo inaishia hivyo...!!

Muda huu ndo week end inaishia kwangu mimi ila najua kwa wengine ndo kwanza wanaamka sasa na kutafuta pa kwenda,ila kiukweli kila mtu na starehe yake............!!!
Leo nilikuwa sehemu 1 wanapaita mbezi salasala nika7babisha watu waone DSTV then nikajirejesha home na ndo nipo mpaka sasa natuma post hii....
maana yake sina mpango wa kutoka tena kwenda popote najiandaa kuianza Monday.....!!

Share:

Dec 10, 2010

ROYAL PUB....!!

Kiukweli mimi sio mpenzi wa mpira ila afanyae vizuri stahili zake pongezi,leo nilikuwa hapa Royal pub ambapo nilifunga DSTV pamoja na projecter si leo ni muda sasa ila leo nilikuwa hapa kuhakikisha mpira wa leo unaonekana vema pasipo kutokea tatizo lolote na ndicho kilichotokea watanzania wameangalia vema jinsi time ya Tanzania iilivyoichakaza Uganda....!!
Bao lilopatikana kwa njia ya penati,ambapo Juma kaseja ameweza kudaka penati 1 huku kipa wa timu ya uganda kutoambulia hata penati 1...
Share:

Hali ya hewa c shwari dar.....!!!

Kiukweli ikiwa kijijini wanaomba mvua mjini tunaichukia mvua kwa kuona ya kuwa haina faida yeyote kwetu kutokana na ukweli kwamba shughuli nyingi zinasimama ama kuchelewa kutokana na hali ya mvua ila mwisho wa siku inakuwa haina jinsi sababu ndio kudra ya m'mungu analopanga binadamu hawezi pangua....!!!
Kwa upande wa DSTV usishangae upo ndani unaangalia huku mvua kubwa unanyesha unaona inakatakata mfano wa CD iliyochunika,ukataka kumwita fundi wala usisumbuke kwani ndo kawaida ila ikikata mvua nayo inatulia kama kawaida,ila kwa madish ya free haina kukata huendelea kuonyesha vizuri muda wote...!!!
Kipindi hiki ndo kipindi cha kujua ubovu wa Dish lako kwako kama pembe la ng'ombe halifichiki....!!!
Share:

Dec 9, 2010

UHURU DAY ilivyokuwa......!!

Tarehe kama ya leo ila miaka 49 iliyopita hayati mwalimu J.K.Nyerere na viongozi wengine walisababisha siku hii iwe tunaikumbuka kila mwaka na kuifanya siku ya kihistoria,kwanini kwasababu ndo siku tulyopata uhuru toka kwa watawala wetu ambao ni wakoloni,ulikuwa uhuru wa Tanganyika ambayo sasa inajulikana kama Tanzania.
Leo ni mapumziko na kila mtu anaifurahia kwa mtindo wake,ambapo kitaifa ilifanyika uwanja wa taifa wenye nafasi walienda lakini mimi nilikuwa kazini kama kawa na haya ndo niliyoya7babisha leo uhuru day.....!!!












 Unaweza ukashangaa vipi Dish la DSTV lakini kuna Reciveiver ya Media com badala ya Decoder ya DSTV,hapa bana nimeinstall channel za Gospel ambazo ni free zipo 30,hazina uhusiano wowote na DSTV ila kwasababu dish zinaingiliana ndo maana tukatumia hilo.....!!!
Share:

Dec 3, 2010

Mfumuko wa VING'AMUZI Tanzania....!!

Watanzia tulizoea ili picha ya TV ionekane clear na uweze kupata channel za nyumbani na za nje kwa kutumia Decoder/Receiver sambamba na Satellite Dish Antenna,ila sasa ni tofauti maana unaweza ukatumia Decoder na Antenna ukapata channel clear kabisa.
Ilianza EASY TV ijapokuwa hawajajitangaza vema ila kiukweli wamekuja vizuri na bado wanafanya vizuri maana unapata local channel karibu zote yaani zile zilizo kwenye transmeter na zilizo kwenye satellite,pia unapata channel nyengine za mataifa ya nje yakiwemo habari.( hawa ni wachina )
Hata mwaka bado toka tutamburishwe STAR TIMES nayo ina channel za local ambazo hazifiki hata tano,pia channel za mataifa ya nje yakiwemo habari.( hawa ni wachina na TBC )
Tena imekuja ATN nao wana vinga'amuzi vyao ambao wapo sana kidini.
Hii inaonyesha kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ongezeko la ving'amuzi linakuwa kubwa kutahamaki ukitaka TBC ununue king'amuzi,ATN ununue king'amuzi,STAR TV ununue king'amuzi,ITV ununue king'amuzi na nyenginezo......!!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA WHATSAPP +255755949413

Post zilizokupita