Call / WhatsApp +255755949413

Dec 25, 2010

Near at Bondeni Hotel Magomeni mapipa

Hapa ufundi ukiendelea
Mcheza kwao hutunzwa na ndivyo ilivyo kila siku ziendazo kwa mungu,hapa ni Magomeni mapipa yaani ni mitaa ya nyumbani wenyewe wanasema mitaa ya kujidai ni karibu na Bondeni hotel ambayo inaonekana kwa mbele kule yenye rangi nyeupe kwa wenye macho....!!
Hapa banaa ilikuwa tatizo local channel hii dish ilifungwa kitambo isipokuwa ilihama tu kidogo kwenye position yake,hivyo nikafanya nilichokifanya ikawa heee watu wanaona wabongo na wazungu wazungu,nami nikachukua vyangu nikachapa mwendo kujiandaa kula chakutoka cha x-mass....!!
Share:

Dec 24, 2010

Tuanaendeleza mbio kama kawaida....!!

Unaambiwa kimbia kipindi wenzio wanatembea....!!
Ila mbio ukimbiazo isije ikawa upo nje ya mstari kiasi kwamba unachoka kabla ya kufika utakapo...!!
Mda huo yule aliyekuwa ananyata anakupita kama anamsukuma mlevi vile...!!
Nashukuru mpaka kufikia hapa ila kiukweli nipo bize sana wale walionitumia email then sijarepply si kwamba nimewapotezea laa hasha ubize ndo unao7bisha na ambacho naweza kusema tupo pa1 daima zaidi ya yote nawatakia sikukuu njema...!!
Share:

Dec 21, 2010

Nawatakia x-mass njema wadau...!!

2010 inaishia na sikukuu nazo ndivyo hivyo zinamalizika malizika kwa mwaka huu...!!
Kila mtu,kila nyumba,maofisi nk. watu wana mishe mishe za sikukuu ya x-mass na mwaka mpya,si mbaya nami nikawatakia maandalizi mema mpaka kufikia sikukuu wadau wote popote mlipo...!!
La msingi nawasihi msherehekee kwa amani na utulivu,huku mkijiuliza je mwaka unaishia huu lipi ambalo ulipanga kufanya limefanikiwa na kwa kiasi gani? ili mwaka unaoanza 2011 uanze na kila ulichokiacha,tufanye hivyo ili tufanikishe ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.
Share:

MAFUNDI WA DSTV NA DISH NYENGINE ZA BURE!!

 Je umewahi kukutana na usumbufu wa Mafundi wenye uwezo mdogo ama usumbfu wowote!!??
Je unahitaji kufunga DSTV mpya kwa bei halali bila kuongeza cha juu!!??
Je unahitaji kufunga Dish yenye channel za bure na ukaondokana na usumbufu wa kila siku kuita ita fundi!!?
 
 Fund dish akifunga Dish ya channel za bure
 
 Umeionaje hapa
 
Kwa Mafundi wa Dish Antenna aina zote na bei nafuu hapa ndipo mahala pake!!
Uzoefu usiokipimo na utapata ushauri bureee!!
Ufunge popote pale iwe Hotelini,Ofisini,Nyumbani na popote upendapo ndani ya Tanzania!!
Kuwa miongoni mwa walionufaika na huduma bora!!
0659161111
Share:

Dec 20, 2010

Zijue channel za nyumbani zinazopatikana kwenye Dish..!!








Hizi ndizo channel za Tanzania zinazopatikana kwenye Satellite Dish,ambayo inaanzia ft6 na kuendelea kwa kutumia C band lnb 1.
Unaweza ukajiuliza inakuwaje mtu anafunga dish kwa channel hizo tu,ila ambacho kitakuongezea ni channel za nje zikiwemo habari,movie na mengineyo...!!
Idadi ya channel inakuwa nyingi ama chache kutokana na idadi ya lnb na ukubwa wa dish pia lakini dish inayoanzia ft6 unaweza ukaona channel zaidi ya 60 zikiwepo na hizo hapo juu za channel Tanzania.
Share:

Dec 19, 2010

Dish hii haina uwezo....!!

Dish ndogo ( ku satellite dish ) haina uwezo wa kukamata channel zilizopo cband kama kwa mfano channel za Tanzania,pia haina uwezo wa kuondoa chenga zilizopo kwenye Antenna uliyofunga kwa ajili ya local kwani haina muingiliano wowote na channel zilizopo kwenye transmetter zaidi ya yote inatumia lnb ndogo tu.
Kwa kuongezea ukifunga Dish huwezi kumuona jirani yako akiwa anafanya mambo yake,maana wapo wanaoamini na kutoa soga za kwamba ukifunga dish ndo kila kitu hata mwizi wako unamuona jamani jamani si hivyo hayo mambo ni ya CCTV camera,nadhani nimesomeka......!!

Share:

Watu wanavyotafuta pesa......!!!

Ili mkono uende kinywani na hata ukikosa kicheko basi likutoke tabasamu ni lazima pesa zikutembelee,hata zikiwa za msimu na kwa kulijua hilo ndo maana watu wanaamka asubuhi wanajituma sana ilihali ankala ipatikane na maisha yaweze kwenda as usually banaa....!!
Kipindi wewe unaumia kutafuta pesa mwengine anaumia jinsi gani atakavyokuchukulia kiulaini na kuondoka nazo,akikuacha kwenye majuto ya ningejua ningenunua hata nanii... ila inakuwa ushachelewa wenye kazi zao washachukua mahela yao...!!
Kiukweli nilichogundua tunapenda sana shortcut ya maisha ila tunasahau misemo ya wazungu yenye maana kubwa sana,NO PAIN NO HONEY au NO GANE WITHOUT PAIN sasa iweje tupende vizuri bila kutaabika...??
Maisha ni magumu sana tena na bila kujituma kamwe hauwezi kutoka na kupenda shorcut madhara yake ni makubwa sana,pesa bila kufanya kazi ni sawa na kulipwa kabla ya kazi maana kazi utakuja ifanya tu siku za usoni,tena inaweza ikawa ni ngumu kuliko malipo ambayo ulikwishapokea,kuwa makini especially vijana wenzangu..!!
 Hii ni picha tu ambayo najua itakuwa imewatamanisha wengi na kudhani nina zaidi ya hizo kwenye akiba yangu kumbe ni picha tu wanaharakati wenzangu....!!
Nimeandika hii kutokana na jamaa fulani ambao waliwahi kunipigia simu kitambo kidogo,wakidai kunifahamu sana na kudai kuna wazungu wamefikia hotel hapa dar na walitaka kufanya biashara hivyo hawana mwenyeji,jamaa mmojawapo katika mtandao huo ambaye alijifanya yupo mkoa na ndiye ananijua mimi kwa maelezo yake,akaomba mimi niwe mwenyeji na kuna madawa ya mazao ama kitu kama mifugo ambayo yanapatikana s.group hivyo niwe kama mtu wa kati then nitapata % fulani....!!
Kusema kweli alivyokuwa ameanza huyo jamaa ndipo alipokosea na nikagudua hanijui bali alipata contact zangu kutoka mtandaoni ama kwa mtu hivyo hata dili yenyewe ilikuwa ya uongo kama jinsi alivyoanza nami nikawapotezea.....!!
Baada ya muda jamaa yangu mmoja nae akanihadithia kama ambavyo mimi nilikumbana nayo ila yeye ikawa wamefika kwenye suala la kutakiwa kutoa pesa kidogo ili apate kingi....!!
Kama ni watanzania ama wageni tunaenda wapi....???
Umakini katika pesa iwe wa hali ya juu otherwise mtalia jamani.....!!
Share:

EURO MIND Antenna

Si wanainchi wote ambao wana uwezo wa kufunga Dish ama king'amuzi kutokana na hali ya maisha jinsi ilivyo na kwa upande wa pili pia si channel zote za nyumbani zinazopatikana kwenye Satellite Dish ama hata penye king'amuzi pia,hivyo swala la Antenna linabaki pale pale kwamba ni la muhimu si uwezo ijapokuwa linahusika pia.
Kwa wapatao tabu kuhusu Antenna ipi inaweza ikawasaidia kuona picha clear kutokana na eneo waishilo,jibu ni moja tu EURO MIND Antenna na ikitokea haishiki basi ujue eneo lako halistahili Antenna.
Kwa wale wenzangu na mimi wa uswazi kuna zile tube ambazo unazifanyia mambo na kuwa bonge la Antenna.
Share:

KU na minara dam dam....!!

 Lau ingelikuwa nainstall C band hakika ningekesha bila kuwa na single solution cable kwa kuwa kungekuwa na kitu kinaitwa interference maana uwapo mnara either wa simu ama mitambo mitambo Satellite Dish hasa C band linakuwa kama linakingwa hivi ama kupungua uwezo wake wa kukamata sawia satellite husika,baada ya wataalamu kulijua hilo wakatutengenezea kifaa ambacho kinaweza kuimili mikiki hiyo nayo ni SINGLE SOLUTION CABLE hii ni kwa Dish kubwa tu...!!
Kwa dish ndogo ni nadra sana kutokea interference hata kama kuna mnara mbele kama nilivyoinstall hiyo DSTV maeneo ya Afri center na mambo yakawa swaafiii...!!!
Ukienda mbali zaidi zipo lnb za dish ndogo ambazo nazo kazi yake ni kukabiliana na interference....!!
Share:

DSTV OFFER IMEFANYA USIKU KUWA MCHANA...!!

Hapa ni maeneo ya sinza karibu na shule ya msingi GRACE,nyumbani kwa mdada mmoja hivi anafanyia kazi pale tigo mliman city,kutokana na ratiba kuwa ngumu katika kipindi cha offer ikatufanya tufike saa 12 jioni na kutulazimu tusababishe ili watu waone walicholipia na usiku ukatukutia hapo.......!!
Lakini pamoja na hayo mpaka kwenye saa mbili kasoro ikawa wanaume tunachapa mwendo na siku ikawa bulubulu kama zege halikulala maana ingeharibu ratiba ya kesho.....!! 

 Kutoboa matundu na drill ili kufunga stend ya Dish ya DSTV

 Hapa kutafuta signal ya DSTV

 Stend imekaa inavyotakiwa

 
 Hapa signal ya kutosha picha inaonekana


Finder inafanya kazi nyakati zote kutokana na mazingira nikiwa na maana ya kuwa hata usiku pasipokutumia taa yenyewe ina taa ambayo inaweza kujiteemea hata kwenye giza totoloo....!!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA WHATSAPP +255755949413

Post zilizokupita