Lipia kifurushi cha Azam Play Tsh 28,000/= kwa miezi 12 ( Mwaka mmoja ) ambapo ni Tsh , utapata Vifaa na Kufungiwa bureee!!!
Hii itakufanya uokoe Tsh 165,000/=
Offer hii iawahusu wateja wapya tu!
Kujua vifurushi na channels zilizopo kwenye Azam Tv Bofya Hapa
Kupata mafundi wa Azam TV Bofya Hapa
Kununua King'amuzi cha Azam Tv Bofya Hapa
Ile kununua kwa Tsh 79,000/= bado inaendelea ingawaje kwa sasa hakuna ile kupata na kifurushi cha Compact badala yake kuanzia Tarehe 1/11/2016 Vifurushi vyote vya DStv vitapungua bei..
Wateja wengi wa Startimes wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi na utaondokana na ile adhabu ya kufanya malipio kwa lengo la kupata mwezi mzima matokeo yake unapata kuona kwa muda wa wiki 1 tu! Kwanza vijue Vifurushi vya Startimes kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Smart Tsh 18,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Smart+SportPlus Tsh 32,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Kabla ya kufanya malipo chukua simu yako bonyeza *150*63# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu StarTimes Chagua:
Kiswahili <
English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
Kujua salio
Kulipia kwa vocha
Sajili dekoda yako mpya
Q and A ( Swali na Jibu )
Chagua kifurushi <
( Unachagua "chagua kifurush,una bofya OK" )
Ujumbe utakaoupata ni:-
1.DTT ( Antenna )
2.DTH ( Dish ) <
Chagua kulingana na king'amuzi unachotumia,hapa nitachagua cha Dish
Ujumbe utakaoupata ni:-
Tafadhali ingiza tarakimu 11 za smati kadi yako iliyochomekwa upande wa kulia wa dekoda yako (mfano 02139xxxxxx )
( Weka namba za Smartcard yako zenye tarakimu 11,kisha una bofya OK )
Ujumbe utakaoupata ni:-
Smart-18k
Smart+SportPlus-32k <
Super-48k
( Unachagua unachotaka kulipia mfano tumechagua namba 2,una bofya OK )
Ujumbe utakaoupata ni:- Asante.Utapokea majibu hivi punde.StarTimes
NB:Niwe tu mkweli nilichelewa kuiweka hii post kwakuwa maelekezo yake kampuni husika imeshindwa kuyakamilisha hivyo najua ambacho mtapata ni usumbufu kwa maana hiyo utakapokwama huna budi kupiga +255764700800 ili uhamishwe kifurushi.
Kifurushi cha Smart Plus kimeongezeka huku beo zikiwa pungufu kwa baadhi ya vifurushi pia,mabadiliko hayo ni kama ifatavyo:-
1-ZUKU SMART PACK
Ina channel 30 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 8,999 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
2-SMART PLUS
Ina channel 40 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 13,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki! 3-ZUKU CLASSIC
Ina channel 69 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 18,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
4-ZUKU PREMIUM
Ina channel 98 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 25,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
5-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 26 safi.
Malipo ni Tsh 24,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Kununua Zuku tv Tsh 88,000 bila ufundi! Ufundi ni Tsh 30,000! Piga +255 789 476 655
Niwe mkweli katika hili usipopata fundi makini uwezekano wa kuepuka hili ni mdogo sana vinginevyo muhusika uwe makini sana na Fundi wako ingawaje mara nyingi muhusika inakuwia vigumu kuona jinsi fundi wako alivyofunga Dish huko juu ya paa!!
Sababu zinazopelekea Dish kupata kutu kwa haraka:-
Sababu zisizoepukika:-
> Ikiwa Dish inafungwa ufukweni.
> Ikiwa Dish ni FAKE.
Sababu zinazoepukika:-
> Kutokuweka vinavyozuia maji kuingia.
Tuone madhara ya kutotumia vinavyozuia maji kuingia ndani na kukosa pa kutokea!
1
Hii ni Stendi ya kubeba Dish,hiki ni kikalio ( Chini ) ambapo kwa kutokufunika juu,imesababisha maji yameingia na kwakuwa hakuna sehemu maalumu ya kutokea maji yanapoingia,yenyewe yakatafuta njia kwa kutafuna kidogo kidogo mpaka kupata njia kama muonavyo!
2
Huu ni mkono wa kushika LNB,upo mfano wa V,mkono huu ni bomba maana yake kati lipo wazi,upande wa mbele inafungwa LNB ambapo inazima maji kuingia na upande wa nyuma kuna ya kukipachika ili kuzuia maji yasiingie kama ilivyoonyeshwa picha namba ( 5 ) kwakuwa yakiingia kinachotokea pale kwenye mkunjo ndipo maji yatajitengenezea njia kama muonavyo hapo juu!
3
Matokeo yake ile V inageuka vipande viwili baada ya kuliwa na kutu!
4
Ufungwaji Dish wa namna hii ndio unaopelekea madhara tuliyoyaona hapo juu kwenye picha ( 1 - 3 ) jinsi maji yalivyosababisha kutu,ambapo kama fundi angetumia vifaa vyote ipasavyo yasingetokea madhara hayo yaliyotokea!
5
Hivi ndivyo unavyopaswa kufunga Dish yako kwa kutumia Plastic cover ili kuzuia maji yasiingia kwenye bomba ya Stend na mkono wa kushika LNB!
Nadhani kwa uchache umeambulia kidogo kwa maelezo zaidi
Kwakuwa karibu Ving'amuzi vyote Tanzania vinatumia Dish ndogo leo niwape kasomo haka alau mwenye kujaribu na ajaribu atakapopata wasaa!!
Fanya haya ili uweze kufunga Dish ndogo:-
1.Dish Antenna Assembly:
- Unganisha kifaa kimoja kimoja kama karatasi ya maelekezi inavyoonyesha ili kulikamilisha dish lako bila kuacha hata kimoja kwakuwa kila kimoja kina kazi na umuhimu pia.
2.Unganisha stendi yako ya kubeba dish.
3.Angalia sehemu nzuri ya kufunga Dish ili uanze kufunga stendi yako:
- Hakikisha sehemu unayoifunga mbele hakuna miti itakayozuia kupokea signal.
- Sehemu imara itakayoweza kukaa Dish bila kucheza.
- Unashauriwa kuifunga juu ya usawa wa nyuma/jengo ili isipate kuguswa guswa.
4. Funga stendi yako ya dish sehemu ulipoona panafaa.
5. Funga Dish lako kwenye stendi kwa kulielekezea Satellite uliyoikusudia ( Muelekeo wa king'amuzi husika )
6. Unganisha Coaxial cable ( Signal cable ) kwenye king'amuzi chako kwa nyuma sehemu iliyoandikwa LNB IN kisha unganisha kwenye either kwenye Dish sehemu ya LNB ama kama utakuwa na kitafuta signal (Signal Finder ),kama utatumia Finder lazima uwe na Test cable ( Kipande cha cable ambacho utachomeka toka kwenye finder mpaka kwenye dish ( LNB ) - Nimetoa mfano wa Finder hii kwakuwa ni rahisi kupatikana na hata bei yake ni ya kawaida ila kuna finder nyengine hazihitaji Test cale.
7. Upo tayari kwa kuanza kutafuta signal. Jinsi ya kutafuta signal ntawaletea somo hilo katika post nyengine!
Wadau/Wateja wa ving'amuzi wakubwa ni wapenzi wa mpira hii ilikuwa hata kabla Tanzania haijaingia katika makubaliano ya kati ya zile nchi zilizoachana na mfumo wa Analogue tv na kuingia katika mfumo wa Digital tv..Hii inatokana na wapenzi wa mpira kutaka kupata mpira kwa njia yeyote ile,hivyo imekuwa kama ndo biashara ikiwa ni mdau wa ving'amuzi ili ufanye mauzo mazuri ni lazima ujue namna ya kupata kuonyesha mpira hii imepelekea kina sisi kuchangamkia fulsa kwanza kutafuta njia za kupatikana kwa channels zinazoonyesha mpira bure/kwa bei nafuu kwa udi na uvumba ili kuweza kuuza kwa wahitaji ukiachilia kampuni iliyo na idhini ya kuonyesha mpira Multichoice ( DStv ) ambayo hakuna mdau yeyote wa mpira ambaye halalamikii bei za DStv hususani Packeges za Sports,hii inapelekea kila kukicha kubuniwa njia za kuibia channels za DStv!
Pata msaada wa haraka na updates za Visimbuzi instagram @mustaphamadish
Hili ni moja kati ya yale ambayo ni kero kwa watumiaji wa ving'amuzi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha na kukosa sehemu ya kupata maelezo ya kina kama hapa!
Swali la kwanza unatumia king'amuzi gani!?
Ving'amuzi vyote vyenye vifurushi ukilipa kifurushi ambacho si kile ulicholipia mwezi uliopita kama pesa pungufu hakuna picha utakayoiona na ikiwa pesa ni nyingi utaendelea kuona kifurushi kilichoisha,hivyo ili uone kifurushi ambacho umekusudia kutokana na pesa uliyolipa unapaswa kubadili kifurushi kwa kufata mtindo niliouelekeza hapa!
Chagua king'amuzi chako hapo chini ili kupata maelezo ya kina:-
Azam tv Bofya Hapa kujua kuhusu jinsi ya kuhama kifurushi!