Call / WhatsApp +255673378129

Oct 7, 2010

HOTEL INSTALLATIONS

Tunachofanya ni kukubaliana na muhusika channel zipi anahitaji kutokana na mapenzi ya wateja,nikimaanisha channel pendwa,baada ya hapo tunainstall channel idadi iliyotakiwa then tunatengeneza master chumba maalumu,tukiwezesha vyumba vyote vya hotel kuingia channel zote zilizohitajika na kufanya kila mteja aliye chumba alichopanga kujibadilishia channel apendavyo kwa kutumia remote ya TV chumbani kwake,huku channel zikiwa na quality ya digital pasipo chembe ya chenga.
Share:

APARTMENT INSTALLATIONS

Wengi wanapenda kufunga DSTV huku local na channel nyengine zikiachwa kwa wapangaji wenyewe kama wanahitaji kutokana na ukweli kwamba wapangaji wengi wa Apartment si wenyeji wa Tanzania hivyo hawaoni umuhimu wa kuangalia channel za nyumbani wakiamini TBC inawatosha ambayo inapatikana kwenye DSTV.Ambacho kinafanyika tunainstall Dish 1 ama 2 mbili kwa apartment nzima,nikimaanisha nyumba zote za wapangaji wa humo kutakuwa na connection ya DSTV ambacho yeye anafanya ni kukunua DSTV decoder tu ambayo hata akihama anaweza kuhama nayo.Hii pia inafanya mazingira ya apartment husika kuwa nadhifu na muonekano mzuri kwa kupunguza wingi wa madish,njia hii inawezekana kwa channel za local ama nyengine pia inategemea na wapangaji husika ama mmiliki wa apartment.
Share:

C BAND SINGLE SOLUTION CABLE

Hiki ni kifaa ambacho kinauwezo wa kukabiliana na interfierence sehemu zilizo na minara mitambo mitambo nk.Pia kuna channel ambazo hazipatikani mpaka utumie Single solution cable c band LNB haijarishi kama kuna interfierence ama laa.
Share:

TOFAUTI YA RECEIVER NA DECODER

Decoder ni kifaa kinachopokea Channel ambazo zipo fixed kwa mfano DSTV,ni lazima ziwe zinalipiwa na kampuni husika,hii inamaana huwezi kupata bure labda wenyewe waamue hivyo ama upite wizi.
 Receiver ni kifaa kinachopokea channel zote zilizopo kwenye satellite,haijarishi kama ni fixed ama zipo zipo tu,ila hii inategemea na muelekeo na setting husika ikizingatiwa freequence.Haina maana kwamba hata zile za kulipia utazipata bure,zipo ambazo utazipata kutokana na ukubwa wa dish na muelekeo na huwa sio zote.
Pia kuna Receiver zinazotumia smart card hivyo unaweza ukapata channel zote za kulipia mf: channel za DSTV unaweza ukapata bila kutumia decoder zao,kitakachokulazimu ni kununua smart card yao.
Share:

Baada kufa GTV...!!

Ni wazi kwamba ni watanzania wengi wameathirika na uyeyukaji wa GTV wamejikuta wamebakia na Decoder wasijue wazifanyie nini huku wengine wakijipa imani ya kuwa ipo siku watarejea....!!
Decoder ya GTV unaweza ukaitumia kwa kutumia dish lake lile lile unaweza ukaona channel zipatazo 13 FREE,ambazo ndani yake kuna kama MBC1,2,3 ambazo zinonyesha movie sometimes mpira ambao unakuwa live ila si mechi zote,wala ligi maalumu inakuwa wenyewe tu wakijisikia kufanya hivyo wanafanya.Ukiacha njia hiyo kuna jamaa yangu mmoja ambaye nakili kusema ya kuwa amenizidi ung'amuzi kiasi kwamba amefanikiwa kuflash GTV decoder na ikawa receiver ambayo inapokea channel yeyote kutokana na matakwa yako...!!
Dish la GTV pia unaweza ukatumia kwa DSTV ama channel za Gospel ama nyengine kwa sababu Dish haichagui Receiver ama Decoder ni ufundi wa fundi tu.
Share:

JUA USICHOKIJUA..........!!!

Kwa channel za nyumbani Tanzania si zote ambazo zinapatikana kwenye Satellite Dish Antenna,kwa sababu TV station nyengine wanatumia Transmeter kurusha matangazo yao hivyo channel yeyote ambayo inatumia Transmeter haipatikani kwenye Dish,nikiwa na maana ya kuwa itakulazimu utumie Antenna ya kawaida.
Zijue channel ambazo zinapatikana kwenye Satellite Dish Antenna:-
*ITV,EATV,CAPITAL
*STAR TV
*ATN
*TBC
*CHANNEL 10
NB:Hii ni kuanzia Satellite Dish Antenna inayoanzia futi 6 na kuendelea na LNB itumikayo ni C band.
Share:

Sep 15, 2010

ARABSAT


Hii inajumuisha Dish kubwa cband,Receiver,LNB,Cable na Installations!
Unapata kama channels 29!

KUHAMISHA Tsh 50,000/=

KUFANYA REPAIRING Tsh 30,000/=

KUFANYA INSTALLATIONS Tsh 50,000/=
Share:

DSTV INSTALLATIONS



DSTV SINGLE VIEW
Kwa sasa offer imeisha kwa Tsha 169,000/= unapata vifaa pamoja na Installations ya single view!!
Then unachagua package uipendayo na kuilipia kwa utaratibu uliowekwa kama ifuatavyo:-
Access $10 - Channels 40. Kama Tsh 16,000.
Family $20 - Channels 55. Kama Tsh 32,000.
Compact $30 - Channels 60. Kama Tsh 48,000.
Compact plus $50 - Channels 70. Kama Tsh 80,000.
Premiur $80 - Channels 100. Kama Tsh 128,000.
Unaweza ukapanda na kushuka kutokana na chaguo lako!
BEI MPYA YA VIFURUSHI Bofya Hapa

 DSTV EXTRA VIEW
 
Hii inatumia Decoder mbili na unapata channels 2 tofauti kwa A/c moja kinachozidi ni $10 kwa mwezi kwa package utakayoichagua!


DSTV HD DECODER
Ina uwezo wa kupeleka mbele,kurudisha nyuma,kusimamisha hata kama kipindi ni cha moja kwa moja,pia ina uwezo wa kurekodi saa 150!
Zaidi ya yote inaonyesha vizuri zaidi kuliko decoder za kawaida.
Hiiinajumuisha Dish ndogo,lnb ya njia 4,cable mt 100.Kwenye malipo ya mwezi inazidi $10 kutokana na kuongezeka channels kwenye HD DECODER unapata zaidi ya channels zile zanazopatikana kwenye SINGLE VIEW DECODER!
Pia unaweza ukawa na HD DECODER na ukafanya EXTRA VIEW kwa kuongeza DECODER nyengine ya SINGLE VIEW lakini pia itazidi $10 kwenye malipo ya mwezi!
Pia unaweza ukawa na HD na ukaongeza HD kwa EXTRA VIEW

KUHAMISHA DISH
Inategemea DSTV gani:Single view,Extra view,HD!!

KUFANYA REPAIRING
Inategemea DSTV gani:Single view,Extra view,HD!!

KUFUNGA MPYA
 Inategemea DSTV gani:Single view,Extra view,HD!! 

Pata huduma fasta na inakufuata mpaka ulipo!!
Piga +255 789476655
Offer ni mpaka kuisha kwa bidhaa!!
Share:

Sep 14, 2010

Abudhab TV


Hii ni ya waarabu na ili upate lazima ununue Arabuni,bei inategemea na jinsi utakavyopata namaanisha zile njia za kuagiza!!
Hii inakuwa ni Decoder inakuwa na air time ya miezi 12!!
Itakapoisha itakulazimu kulipia tena kwa mwaka kwa utaratibu utakaopewa!
Sisi ambacho tunafanya ukishakuwa na Decoder tutakusaidia kupata Dish.lnb,Cable pamoja na Installations.
 KUHAMISHA Tsh 50,000/=

KUFANYA REPAIRING Tsh 30,000/=

KUFANYA INSTALLATIONS Tsh 50,000/=

Share:

Mar 16, 2010

Kazi za Diseqc switch

 Inaitwa Diseqc switch ni switch mojawapo katika mfumo wa satellite dish antenna.
Kazi yake ni kuunganisha LNB zaidi ya moja,ama unaweza kusema Dish zaidi ya moja kwa wakati mmoja na channel zote kuingia kwenye receiver moja na kuweza kuona hata channel zaidi ya 200 ambazo zipo kwenye dish zote ambazo zimeunganishwa kwenye diseqc switch.
Kuna aina kadhaa za Diseqc:
  • Njia 2-inauwezo wa kuunganisha lbn 2 kwa wakati mmoja.
  • Njia 3-inauwezo wa kuunganisha lnb3 kwa wakati mmoja.
  • Njia 4-inauwezo wa kuunganisha lnb 4 kwa wakati mmoja.
  • Njia 6-inauwezo wa kuunganisha lnb 6 kwa wakati mmoja.
  • n.k
 Our service's more than your payments.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita