Oct 9, 2014


Tarehe 10 mwezi wa 10 miaka kadhaa nyuma..
Mustapha Hanya nikazaliwa kwa kichache nilichonacho Mustapha MaDish ukitiita hivyo inatosha..
Ah siwezi sema najua kila kitu ila nashukuru kwa umri wangu nimejua mengi sana..
Hakuna wa kumshukuru zaidi ya Allah muweza wa yote!
Kama leo nakumbuka siku yangu hii ya kuzaliwa sitakuwa sahihi kama sitawahusisha wazazi wangu wawili..
Daima ntaomba na sitaacha kuomba dua kwa Alla ampunguzie adhabu ya kaburi baba yangu mpendwa,huyu kwangu ndiye anakuwa shujaa,ndiye aliyenimezesha na kunifanya niishi popote na nisimame na yeyote na mwisho wa siku sirudi nyuma wala sinyoshi mikono juu..
Mungu ailaze roho ya marehemu baba mpendwa ISMAILY OMARY HANYA.
Shukurani za dhati pia zimuendee mama kipenzi FATUMA BAKARY wote kwa pa1 kufanya jitihada wawezavyo mpaka mimi leo nakuwa Mustapha MaDish maana yake wanastahili pongezi sijatoka nje ya mstari unaopaswa kijana kuwa ijapokuwa nna rafiki zangu kadhaa nilisoma nao na wengine kuishi nao mtaani kuwa nje ya mstari kwa kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ama kuwa watu wa matukio.
SHUKURANI KWENU WADAU..
Pia napenda kuwashukuru wadau wangu woote popote mlipo,nashukuru mpo sambamba na mimi kila kukicha napokea simu nyingi sana na zote zikionyesha ya kuwa mnanikubali na mnatembela haka ka blog chetu,nami nitajitahidi kadri niwezavyo maoni yenu kuyafanyia kazi!


4:30 PM   Posted by Mustapha Hanya with 5 comments

5 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hongera mkuu hivii mbona hampendi kuweka miaka!!

Anonymous said...

Hongera mkuu mungu akupe umri mreefu na mafanikio tele..

Anonymous said...

mungu akujaalie umri mrefu wenye baraka mingi mingu!

Anonymous said...

mbona hujatualika tukuletee vizawadi?
ila hongera sana kaka Mustapha

Anonymous said...

Happy born day Madiiiiish!!!
Upo juu sana n Mungu akuweke miaka miiiingi ili tuendelee kunufaika kupitia wewe big up mtu mzima n moyo wako iendelee hivyo hivyo upo peace sana

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search