Oct 16, 2014

Ijapokuwa imepita miezi ipatayo 10 ila hili ni moja kati ya niyakumbukayo na ya kujivunia pia na sababu napokea simu mpaka wakati mwengine naona imepitiliza ila kwakuwa ndo kazi yangu sinabudi kumaliza shida za wadau wangu...
Nakumbuka ni maeneo ya sinza pale kumekucha kwa mzee moja hivii wa kihindi nilifunga Azam tv,kama ilivyoada kulipua kwangu ni mwiko nikafanya yangu na kanuni zangu kisha nikakabidhi kazi kwa mteja wangu!
Mteja cha kwanza kuniambia "nimependa kazi yako,umechukua muda mfupi na kazi safi" kwa kulithibitisha hilo wakamtoka wekundu wekundu pale nje ya malipo ya king'amuzi,hii alitoa kama pongezi yake kwang,nami kwakuwa nimetumwa helaa aaah nikashukuru pale wekundu wangu mfukoni kisha nikachapa mwendo!
ilipita kama wiki mbili alipata tatizo la king'amuzi maana kulikuwa na fundi akaleta ufundi nyumbani kwake hivyo alitaka msaada wa fundi,ilimlazimu afike ofisini na kwa bahati mbaya sikuwepo..fundi aliyepo akachukua nafasi yake akaenda na mteja kuangalia tatizo...
Tatizo alilimaliza na mteja akaendelea pata burudani kama kawaida...
Ikapita kama siku kadhaa tu mbele akaja tena ofisini kwa kununua king'amuzi kingine ila kwasasa alitaka zuku lakini safari hii pia hakunikuta,alidai aondoke na vifaa vyake ila kufungiwa anataka afungiwe na Mustapha,nilijaribu kupigiwa simu nami nilisema ukweli ni kama baada ya siku nne ndipo nitakuwa na muda,kitu ambacho kila mmoja pale ofisini alishangaa kuona mteja anakubali kuningoja..
Haikuchukua siku nne bali yule mteja alingoja kama wiki na siku tatu ndipo nikapata muda wa kwenda kumfungia Zuku yake..
Na hapo ndipo nikapata malalamiko ya fundi aliyeenda kufanya repair baada ya kupita mimi..
Hakukuwa na maelewano mazuri,lugha ya biashara haikutumika hapa ila nilichofanya ni kumtaka radhi kisha nikampa burudani kama ilivyo ada!
Matokeo yake hataki fundi yeyote zaidi Mustapha.
Hapa tunazungumzia uwezo binafsi si kama najua saana,ijapokuwa najua vilivyo vingi ukanda wangu na hata aliyefanya hivyo ni mwanafunzi wangu kati ya wanafunzi wangu wengi tu ila alishindwa ama wanashindwa kufata ile misingi husika..
Mafanikio huja kwa kupenda unachofanya!
Ukipenda unachofanya,utakifanya kwa uwezo wako wote na hii lazima ufanikiwe..
Upo facebook Bofya hapa like page yangu kupata mapya ya ving'amuzi vyote Tanzania

8 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Heshima kwako mkuu!!
Ila pale ofisini kwako utaratibu uliopo sio mzuri kabisa tukija kukuulizia inakuwa mtihani sana hata kupewa no.zako ila kwa kuea hii blog tunakupata vema sema na jamaa zako...

Anonymous said...

Iweje ufanye vizuri na vijana wako walipue?
Ulipiga msasa vizuri hutalitafuta kosa mkuu.
All the best

Anonymous said...

Ndivyo inavyotakiwa iwe unawakumbusha kumbusha vijana wanaoharibu taaluma tupo nyuma yako kila hatua.
Mungu akubariki mkuu

Anonymous said...

Acha watu wakusifu, sio kujisifu mwenyewe kama wanamuziki wengi wa kibongo.

Anonymous said...

Hahaha kaka watu kama hao wasiokubali matokeo wapo kijiji tena wapo tokea enzi za mitume iwe kama changamoto huwezi fanana na bongo fleva Big up sisi ndio tunaojua umuhimu wako na hii blog piga kazi Mustapha madish mkaleee

Anonymous said...

Muda ambao unapoteza muda kuandika hii comment ya kudis mwenzako anaingiza mpunga nasi tunapata urahisi wa huduma tena huduma safi kwa bein tunayoimudu

mike said...

Trenet tv ya Efata mwenge unaipata kwa fr zipi mkuu , je ni lazima kutumia lnb ya ziada karibu na lnb ya 68.5deg East?

Anonymous said...

Mimi na wengine kama mimi bado tutakutakia mafanikio mema na kukupongeza kwa hili na kukusihi usiache kutupa elimu hii bure na huduma bora kwa urahisi

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search