Dec 1, 2015


Wateja wengi wa Azam tv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue Vifurushi vya Azam tv kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Azam Pure Tsh 15,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Azam Plus Tsh 23,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Lipia kwanza Tsh 23,000 kisha chukua simu yako bonyeza *150*50*5# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu Azam tv
Chagua
 1. Kiswahili <
 2. English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
 1. Angalia salio
 2. Badili kifurushi <
 3. Sajili Huduma Mpya
 4. Endeleza Kifurushi Cha Nyongeza
( Unachagua Badili kifurush,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata nia:-
 • Tafadhali ingiza namba ya Smartcard
( Weka namba za Smartcard yako,kisha una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
 1. Pure 15,000
 2. Plus 23,000 <
 3. Play 28,000
 4. Kihindi Pekee 16,000
( Unachagua namba 2,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
 1. Badili sasa hivi <
 2. Badili baada ya kifurushi kuisha
( Unachagua namba 1,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-

Asante. Ombi lako linashughulikiwa. Utapata ujumbe muda si mrefu.AZAM TV

Kisha utapokea ujumbe mfupi kwenye simu yako unaotoa maelezo kama ombi lako limefanikiwa ama laa!!
Hii ni jinsi ya kuhama toka kifurushi cha Azam Pure kwenda kifushi cha Azam Plus.Utaratibu wa kuhama kifurushi ni huu kwa vifurushi vyote na ikitokea umelipia Tsh 23,000 na haujahama kifurushi itafunguka kifurushi kile kile cha Tsh 15,000 na kubaki kwenye a/c yako Tsha 5,000.Unaweza ukabadili kifurushi ndani ya masaa 72 kwa lugha nyepesi siku tatu na ikitokea imezidi hapo huna budi kupiga simu ili wakusaidie zaidi!
Zoezi hili uhakikishe king'amuzi chako umekiwasha kisha ndipo unafanya zoezi hili na inachukua dk 5 mpaka 20 kubadilika kifurushi na ukitaka kujua zoezi lako limefanikiwa baada ya muda Angalio Salio kwa kutumia utaratibu wa hapo juu!
Kwa uchache huu nadhani nimekusaidia kitu!

+255 789 476 655
2:26 AM   Posted by Mustapha Hanya in with 7 comments

7 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Ikiwa mimi nimelipia 23000 kabla mwezi haujaisha nataka kuhama kifurushi nafanyaje hapo mkuu?

Unknown said...

Acheni kutubadilishia bei za kifurushi kila ikiingia channel mpya tu mnabadiri bei cc wenye hali ya chini kimaisha mnatupa wakati mgumu sana.

James Joseph said...

Jana nilipia kifurushi cha 15,000 leo nataka kuhamia cha 23,000 nifanyeje!???

Unknown said...

Ikiwa nimelipia kifurushi kwa ajenti na hajaniunga nifanyeje

Salum Salum said...

Jaman kuna chanal gani ukitoa TBC1 na UBC ambayo inaonesha world cup

Unknown said...

Jinsi ya kujiunga kifurushi cha Azam lite

nassoromwanga10@gmail.com said...

nimejiunga cha 10000 jana ila leo nataka nihamie cha pure 18000 kwa kujazia 8000 inawezekan!?

Call +255789476655

 • Text +255759091445

Follow

Search