Dec 6, 2015

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI DSTV


Wateja wengi wa DStv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue vifurushi vya Dstv kwa Kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha DStv Bomba  Tsh 23,500 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha DStv Compact  Tsh 84,500 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-

1 - Washa Decoder yako,kisha weka channel namba 200.
2 - Lipia Tsh 84,500 
3 - Piga nambari 0768988800 ( Atakayepokea mwambie kuwa unahitaji kubadili kifurushi toka DStv Bomba kwenda DStv Compact nae atafanya hivyo na itapokea ndani ya dk 5 tu )

Unaweza kubadili kifurushi kwa kufata utaratibu huu kwa kifurushi chochote kile na unaweza kufanya zoezi hili hata kabla kifurushi chako hakijaisha!

+255789476655
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

5 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Ikiwa nataka kuhama kifurushi kabla ya ambacho nimelipia nafanyaje?
Nipo hiki cha 51000 nataka kuhamia cha 84500 na toka nilipie hiki yapita kama wiki hivi msaada tafadhali mkuu

Anonymous said...

Nimelipia hivi karibun nataka kuhamia cha 84500 toka 23500 ipo vipi?

Danny Siriwa said...

Santeeeeeeh xn

kifuatz said...

msaada kaka nina dstv decoder nimepewa kina kifulushi cha dstv primium cha 175205 je niatawezaje kuhama kwenda dstv bomba cha tshs 23000? na datas zake sina mwenyewe yupo nje?

Anonymous said...

msaada kaka nina dstv decoder nimepewa kina kifulushi cha dstv primium cha 175205 je niatawezaje kuhama kwenda dstv bomba cha tshs 23000? na datas zake sina mwenyewe yupo nje?