Mar 24, 2016


Ukiona neno NO SIGNAL ama kwa kukurahisishia ukiona hupati picha kwenye King'amuzi chako na unapata ujumbe ambao hauhusiani na malipo ujue kuna tatizo la Signal lakini utathibitisha vipi kujua kama ni kweli tatizo ni Signal.
> Kila King'amuzi kina channel ya/za bure ( hapa simaanishi Local channel ) ambapo hata ikiwa malipo yako ya mwezi yamekata utaendelea kuangalia tu huwa hazikati,hivyo yakupasa uzijue Channels hizo ili unapoona umepata ujumbe huuelewi jaribu kuweka channels hizo uone zitaonyesha!? Ikiwa zitaonyesha maana yake tatizo sio signal,tatizo litakuwa ni malipo na ikiwa hazitaonyesha jibu lake tatizo ni Signal.Nimejaribu kuwajuza njia hii ya kienyeji kutokana na wengiwetu hizi lugha zilizokuja na ndege ni mtihani nami nimegundua hilo hivyo sitawaacha nitaenda nanyi sambamba!

Cha kufanya ukishajiridhisha kuwa tatizo ni Signal:-
  • Angalia Signal Cable ( waya inayotoka kwenye Dish/Antenna ) ipo sawa?
> Hakuna sehemu iliyochunika/kukatika
> Imechomekwa sawa kwenye King'amuzi chako sehemu ya lnb in/Antenna
> Imechomekwa sawa kwenye Dish/Antenna ya hicho king'amuzi
> Signal Cable ( Coaxial Cable ) Ina nyaya mbili ndani ambazo hazipaswi kugusana ( Siku nitawaeleza kazi za hizo nyaya )

Ikiwa umeona kupo sawa huna budi kuwasiliana na fundi wako ikiwa unamkumbuka ama unaweza kuwasiliana na kampuni husika ya king'amuzi ukikosa msaada piga namba hii +255789476655.

Tatizo linaweza likawa ni nini baada ya hatua za awali kuzifata?
> Yaweza kuwa Dish ama Antenna imepoteza muelekeo wake
> Yaweza kuwa kama king'amuzi cha Dish lnb kufa
> Yaweza kuwa AC ya signal kwenye king'amuzi imekufa
Zaidi ya yote ili kupata uhakika wa nini tatizo ni fundi atakapofika sehemu ya tukio!

IKIWA UMEFANYA MALIPO NA HUPATI PICHA Bofya Hapa

mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
9:26 AM   Posted by Mustapha Hanya in , , , , , , , with 9 comments

9 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kwa somo hili nimeambulia kitu

Anonymous said...

Mimi nimekuwa muhanga kwa hili swala mara nyingi tu natumia king'amuzi cha zuku na kila inapotokea nataka kufanya malipo huwa napata usumbufu mkubwa mno hivyo naomba ufafanuzi ikiwezekana kumalizia hiyo link ya zuku tv nashukuru na pole na majukumu mkuu!

john sombi said...

Kiukweli maelezo haya yamenisaida kusolve tatizo langu

Unknown said...

Nimeelewa pia nimekuwa Mwalimu wa wengine ahsante sana

Unknown said...

Je sisi wenye vile ving'amuzi vya toleo la kwanza kabisa nafanyaje ili niweze kukitumia?

Unknown said...

SAWA MKUU

Unknown said...

Mimi sipat kabisa chanel mchana usiku ndio napata sijui nifanyaje naomben msaada

Unknown said...

Good

william francis said...

Ahsante sana kaka kwa elimu yako

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search