Aug 1, 2016


Wateja wengi wa Startimes wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi na utaondokana na ile adhabu ya kufanya malipio kwa lengo la kupata mwezi mzima matokeo yake unapata kuona kwa muda wa wiki 1 tu!
Kwanza vijue Vifurushi vya Startimes kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Smart Tsh 18,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Smart+SportPlus Tsh 32,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Kabla ya kufanya malipo chukua simu yako bonyeza *150*63# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu StarTimes
Chagua:
 1. Kiswahili <
 2. English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
 1. Kujua salio
 2. Kulipia kwa vocha
 3. Sajili dekoda yako mpya
 4. Q and A ( Swali na Jibu )
 5. Chagua kifurushi <
( Unachagua "chagua kifurush,una bofya OK" )

Ujumbe utakaoupata ni:-
 • 1.DTT ( Antenna )
 • 2.DTH ( Dish ) <
Chagua kulingana na king'amuzi unachotumia,hapa nitachagua cha Dish

Ujumbe utakaoupata ni:-
 • Tafadhali ingiza tarakimu 11 za smati kadi yako iliyochomekwa upande wa kulia wa dekoda yako (mfano 02139xxxxxx )
( Weka namba za Smartcard yako zenye tarakimu 11,kisha una bofya OK ) 

Ujumbe utakaoupata ni:-
 1. Smart-18k
 2. Smart+SportPlus-32k <
 3. Super-48k
( Unachagua unachotaka kulipia mfano tumechagua namba 2,una bofya OK ) 

Ujumbe utakaoupata ni:-
Asante.Utapokea majibu hivi punde.StarTimes

NB:Niwe tu mkweli nilichelewa kuiweka hii post kwakuwa maelekezo yake kampuni husika imeshindwa kuyakamilisha hivyo najua ambacho mtapata ni usumbufu kwa maana hiyo utakapokwama huna budi kupiga +255764700800 ili uhamishwe kifurushi.

1:20 PM   Posted by Mustapha Hanya in with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Unknown said...

nawezaje kuangalia channel za bure ata kama sijalipia please nisaidie usawa magu mgumu mpaka watu tuna shindwa kununua vifurush

Omary Aman said...

Tafadhali mutuwekee channel za bure jaman kama mulivyo tuahid awali....

Call +255789476655

 • Text +255759091445

Follow

Search