Call / WhatsApp +255673378129

Showing posts with label Digital tv. Show all posts
Showing posts with label Digital tv. Show all posts

Mar 24, 2016

NINI UFANYE KING'AMUZI CHAKO KIKIPOTEZA SIGNAL!!


Ukiona neno NO SIGNAL ama kwa kukurahisishia ukiona hupati picha kwenye King'amuzi chako na unapata ujumbe ambao hauhusiani na malipo ujue kuna tatizo la Signal lakini utathibitisha vipi kujua kama ni kweli tatizo ni Signal.
> Kila King'amuzi kina channel ya/za bure ( hapa simaanishi Local channel ) ambapo hata ikiwa malipo yako ya mwezi yamekata utaendelea kuangalia tu huwa hazikati,hivyo yakupasa uzijue Channels hizo ili unapoona umepata ujumbe huuelewi jaribu kuweka channels hizo uone zitaonyesha!? Ikiwa zitaonyesha maana yake tatizo sio signal,tatizo litakuwa ni malipo na ikiwa hazitaonyesha jibu lake tatizo ni Signal.Nimejaribu kuwajuza njia hii ya kienyeji kutokana na wengiwetu hizi lugha zilizokuja na ndege ni mtihani nami nimegundua hilo hivyo sitawaacha nitaenda nanyi sambamba!

Cha kufanya ukishajiridhisha kuwa tatizo ni Signal:-
  • Angalia Signal Cable ( waya inayotoka kwenye Dish/Antenna ) ipo sawa?
> Hakuna sehemu iliyochunika/kukatika
> Imechomekwa sawa kwenye King'amuzi chako sehemu ya lnb in/Antenna
> Imechomekwa sawa kwenye Dish/Antenna ya hicho king'amuzi
> Signal Cable ( Coaxial Cable ) Ina nyaya mbili ndani ambazo hazipaswi kugusana ( Siku nitawaeleza kazi za hizo nyaya )

Ikiwa umeona kupo sawa huna budi kuwasiliana na fundi wako ikiwa unamkumbuka ama unaweza kuwasiliana na kampuni husika ya king'amuzi ukikosa msaada piga namba hii +255789476655.

Tatizo linaweza likawa ni nini baada ya hatua za awali kuzifata?
> Yaweza kuwa Dish ama Antenna imepoteza muelekeo wake
> Yaweza kuwa kama king'amuzi cha Dish lnb kufa
> Yaweza kuwa AC ya signal kwenye king'amuzi imekufa
Zaidi ya yote ili kupata uhakika wa nini tatizo ni fundi atakapofika sehemu ya tukio!

IKIWA UMEFANYA MALIPO NA HUPATI PICHA Bofya Hapa

mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
Share:

Dec 6, 2014

AIRTEL DIGITAL TV | KING'AMUZI CHA AIRTEL


La kwanza ambalo utajiuliza  mitandao ya simu nayo inachangamkia fursa!?
Ikumbukwe ya kuwa mwaka ndio mwaka wa mwisho kutumia Analogue,ifikapo tarehe 31 mwezi huu,saa 23:59 tunachotakiwa labda kuizungumzia Analogue tu lakini si kudeal nayo...
Lakini ambapo tunaelekea kuisahau kabisa Analogue leo hii mtu ukimuuliza ni nini maana ya Digital hajui na mwengine anajua ni King'amuzi tu kamaliza...
Kuingia mfumo wa Digital pekee bila kuhusisha Analogue ndipo imetulazimu kutumia Ving'amuzi na sababu hii ndio iliyopelekea kukawa na ving'amuzi kibao vipya achilia mbali vile vikongwe..
Airtel Digital Tv..
Hiki nacho ni king'amuzi kama ilivyo ving'amuzi vyengine vya kulipia..
Inatumia Satellite ya SES-7  Nyuzi 108.2E
Ina channels 383 ambapo za HD ni 25
Decoder yake inauwezo wa kurekodi masaa 150
Ijapokuwa mtandao wa Airtel upo hapa kwetu Tanzania lakini king'amuzi hiki kinatumia India tu kwa sasa,sina lolote la kuzungumza kama je na Tanzania kitakuja king'amuzi hiki..
Kwa maelezo zaidi kuhusu king'amuzi hiki Bofya Hapa


+255789476655 | MUSTAPHA MADISH
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita