Yapata wiki ya pili sasa kwa wale wauzaji king'amuzi cha Azam tv kimekuwa adimu kutokana na mzigo kutokuwepo makao makuu ya Azam,ingawaje taarifa zilizotoka ilikuwa jumatatu ya tarehe 8/2/2016 mzigo ungekuwa umeshafika na kuanza kuuzwa kwa mawakala na wateja pia ila hali imekuwa tofauti kutokana na sababu zilizo nje ya kampuni ingawaje jitihada za haraka zinaendelea kufanyika!
Hali hii imepelekea kwa wale mawakala/wafanya biashara tu wanaouza kwa kusua sua kipindi ambacho king'amuzi kina kuwa adimu wao bado wanavyo na matokeo yake wanauza bei juu tofauti na bei stahiki,hii ni kwa Dar na nje ya Dar pia!
Ninachoweza kuwasihi wateja wote wanaohotaji kujiunga na Azam tv waendelee kuwa na subira,mpaka jumatatu ya tarehe 15/2/2016 king'amuzi cha azam kitakuwa kinapatikana kwenye zile sehemu zinu zote,ingawaje juhudi zinazofanyika zikifanikiwa hata kabla ya jumatatu kitaanza kuuzwa! Wale waliopiga simu kama ambavyo wameahidiwa baada ya kuacha mawasiliano yao kwamba watafahamishwa pindi tu uuzwaji utakapoanza nasi tutafanya hivyo bila shaka na wale ambao bado wapo njia panda piga no.+255 789 476 655 kisha acha mawasiliano yako kisha utafahamishwa pindi tu uuzwaji utakapoanza! Kwa wale wa Dar es salaam unaweza kuletewa mpaka ulipo na kufungiwa kisha unalipia!
Kujua vifurushi vya Azam tv Bofya Hapa
0 Unasemaje..??:
Post a Comment