Tv ya kijerumani ya mwaka 1956
Televisheni - TV au runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.
Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.
Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita).
Baada ya Vita Kuu ya II, mfumo bora wa utangazaji wa televisheni Black n White ulikuwa maarufu nchini Marekani na Uingereza, na seti za televisheni zilikuwa za kawaida katika nyumba, biashara na taasisi.Katika miaka ya 1950, televisheni ilikuwa katikati ya msingi kwa kushawishi maoni ya umma. Katikati ya miaka ya 1960, utangazaji wa rangi uliletwa nchini Marekani na nchi nyingi zilizoendelea.. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (widescreen).
Tangu mwaka 2010, kwa uvumbuzi wa smart television, internet television imeongeza upatikanaji wa programu za televisheni na sinema kupitia mtandao kupitia huduma za video za Streaming kama vile Netflix, Amazon Video, iPlayer, Hulu, Roku na Chromecast.
Aina za tv
Siku za usoni nitakuja kuzungumzia kwa kina kuhusu yaliyo hapa chini:
Broadcast Systems
- Terrestrial Television
- Cable Television
- Satellite Television
- Internet Television
- Disk
- CRT
- DLP
- Plasma
- LCD
- OLED
- LDTV
- SDTV
- HDTV
- UHDTV
Imeandikwa na Mustapha Hanya
Whatsapp+255784378129
1 Unasemaje..??:
Thank you for publishing this awesome post. I'm a long time reader however I've
never actually left a comment. I've bookmarked your site and shared this on my Facebook.
Thanks again for a great article!
Post a Comment