Ukiona neno NO SIGNAL ama kwa kukurahisishia ukiona hupati picha kwenye King'amuzi chako na unapata ujumbe ambao hauhusiani na malipo ujue kuna tatizo la Signal lakini utathibitisha vipi kujua kama ni kweli tatizo ni Signal.
> Kila King'amuzi kina channel ya/za bure ( hapa simaanishi Local channel ) ambapo hata ikiwa malipo yako ya mwezi yamekata utaendelea kuangalia tu huwa hazikati,hivyo yakupasa uzijue Channels hizo ili unapoona umepata ujumbe huuelewi jaribu kuweka channels hizo uone zitaonyesha!? Ikiwa zitaonyesha maana yake tatizo sio signal,tatizo litakuwa ni malipo na ikiwa hazitaonyesha jibu lake tatizo ni Signal.Nimejaribu kuwajuza njia hii ya kienyeji kutokana na wengiwetu hizi lugha zilizokuja na ndege ni mtihani nami nimegundua hilo hivyo sitawaacha nitaenda nanyi sambamba!
Cha kufanya ukishajiridhisha kuwa tatizo ni Signal:-
- Angalia Signal Cable ( waya inayotoka kwenye Dish/Antenna ) ipo sawa?
> Imechomekwa sawa kwenye King'amuzi chako sehemu ya lnb in/Antenna
> Imechomekwa sawa kwenye Dish/Antenna ya hicho king'amuzi
> Signal Cable ( Coaxial Cable ) Ina nyaya mbili ndani ambazo hazipaswi kugusana ( Siku nitawaeleza kazi za hizo nyaya )
Ikiwa umeona kupo sawa huna budi kuwasiliana na fundi wako ikiwa unamkumbuka ama unaweza kuwasiliana na kampuni husika ya king'amuzi ukikosa msaada piga namba hii +255789476655.
Tatizo linaweza likawa ni nini baada ya hatua za awali kuzifata?
> Yaweza kuwa Dish ama Antenna imepoteza muelekeo wake
> Yaweza kuwa kama king'amuzi cha Dish lnb kufa
> Yaweza kuwa AC ya signal kwenye king'amuzi imekufa
Zaidi ya yote ili kupata uhakika wa nini tatizo ni fundi atakapofika sehemu ya tukio!
IKIWA UMEFANYA MALIPO NA HUPATI PICHA Bofya Hapa
mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
+255789476655