Call / WhatsApp +255673378129

Jul 5, 2013

BAHARI BEACH LODGE TENA!


Kumbu kumbu yangu ni siku kadhaa nyumba nilifanya ya kupendeza na ndo sababu iliyopelekea nikaitwa tena leo!
Kazi ilikuwa si kubwa sana ijapokuwa kwa asiyejua angemaliza hata mwaka na asingeambulia kitu!
Hapa DSTV ilikuwa time ya jioni inapoteza signal,ila wakati wa asubuhi na mchana mambo huwa shwari..
Tatizo ilikuwa lipo kwenye dish kwa maana nyengine signal ilikuwa imepungua hivyo kunapokuwa na upepo mkali hupotea kabisa!
so nikafanya nilichopaswa kufanya kisha nikashaa!!!
KAMA NAWE UNATATIZO KIUFUNDI ZAIDI USISITE KWENDA HEWANI:
+255659161111

 Ilipo Dish Setting zikiendelea!

 Bahari Beach Lodge Mapokezi

 Kupumzika imoo!!

 Hapa hakuna signal hivyo haiwezi kuscan!

 Baada signal kuingia!

 Hapa imeanza kuscan!
Share:

Jun 30, 2013

CNN!! ZAIDI YA CHANNEL 50 BURE!!

Matakwa ya mteja ndo wajibu wangu kila siku maana nipo kwa ajili ya kukufanya wewe upate furaha kwa unachokihitaji!!
Alinipigia simu na shida yake ilikuwa kupata CNN na BBC free kama inawezekana maana yeye hataki mambo ya kulipia lipia!
Nikamwambia inawezekana tena zaidi ya hizo anazozitaka yeye!
Nikatumia Dish ft 6 na LNB KU pale muda c muda channels zaidi ya 50 jamaa akabaki anacheka cheka tu!
Nikakinga nikakunja na kuachapa mwendo!
Maeneo ya msasani pale haya waungwana x nyngne tena!
Share:

Jun 29, 2013

TRANSIT MOTEL TENA!


TRANSIT MOTEL AIRPORT 

Nilianzia pale uwanja wa ndege na kisha nikaenda fanya ya kupendeza palee njiapanda ya sitakishari!
Kazi niifanyayo ndo inapelekea mwengine akosolewe maana huwa lazima mteja awe nae kama fundi penye tatizo namsomesha mpaka anaelewa n hata anapotoa pesa yake anajua inatoka kwa mahitaji gani!
Binafsi huwa najisikia furaha kuona namfanyia kazi mtu na mwisho wa siku yeye anapata kile alichokitegemea ama zaidi,kicheko chake mwanya mwengine kwangu!
Nikachukua vyangu na kuaga huku nikikaribishwa tena wakati mwengine!

TRANSIT MOTEL UKONGA
Share:

Jun 28, 2013

ARABSAT IMENIPELEKA MWANDEGE!

 HAPA NATAFUTA WAARABU
Sikuwahi kufika wala kutarajia kufika kabla ila kwasababu wewe ndo wa kufanya niende popote hivyo sina pingamizi na najivunia kazi yangu maana faida ya pili kuijua Tanzania kwa vitendo!
Kwa wenyeji wanasema Mwandege ni nje kidogo mwa mkoa wa Dar,hivyo sina la kupinga zaidi ya kulichukua na kutembea nalo kama hivi!

 HAPA NAUNGA UNGA

UNGA UNGA INAENDELEA
Hapa nilitakiwa kuwahamisha waarabu walipo na kuwaleta hapa,jambo hilo kwangu halikuwa gumu kihivyo... nami nikafanya fanya yangu kwa kuunga unga Dish na nikawavuta waarabu wakajaa tele!
Baada ya hapo nikachukua vilivyo vyangu na kuchapa mwendo!
0714973797 kiufundi zaidi!
Share:

Jan 6, 2013

CHANNEL ZA DIGITEK

Hii ni orodha ya baadhi ya channel zilizopo kwenye king'amuzi cha Digitek, ambacho hakina malipo ya mwezi unafurahia tu hizi channels:-

Always Connected
Kwa Maelezo zaidi
PIGA +255789476655
Share:

Jan 2, 2013

DSTV TANZANIA

Kujua bei ya sasa Bofya hapa
SO MUCH MORE..!
Kwa sasa kuna Offer ambapo kwa Tsh 149,000/= Full Installations
Unapata Dish ndogo,lnb,Decoder,Cable mt20 na Kufungiwa!
Baada ya hapo unachagua Package uipendayo kati ya zifuatazo:-
DStv Access Tsh 16,500 - $10
DStv Family Tsh 33,000 - $20
DStv Compact Tsh 53,000 - $32
DStv Compact Plus Tsh 85,000 - $52
DStv Premium Tsh 135,000 - $82
CHANNEL MAALUM
Portuguese-5 Channels
Asian-4 Channels
German-1 Channel
French-4 Channels
China-7 Channels
BEI MPYA YA VIFURUSHI Bofya Hapa
HUDUMA NYENGINE ZA DSTV:-
DStv Extra View
n.k.
Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu
Morogoro rd,Magomeni Mapipa opp DTB
Office: +255789476655
Mobile: +255659161111
Wakala wa DStv aliyeidhinishwa.
Tunafunga na kuuza vifaa vyote vinavyohusiana na DStv.
Pia tunauza na kufunga Dish aina zote.
Kwenye Hotel,Apartment,Office na Nyumbani.
Share:

Dec 5, 2012

FLAT SCREEN INAZIDI FANYA VIZURI!

 NISHAFANYA YANGU
Kiukweli ntaona ajabu sana kama unataka kununua TV na ukaenda kununua zile analogue badala ya flat screen kitu cha bapa!
Naanza kuzisahau TV za chogo maana kile niendapo nakutana na flat,jambo zuri na kupendeza maana hata ufungaji wake tv inakuwa self.
Ilikuwa ni kwenye Office moja hivi,nilifunga dish ya DSTV then nikafunga flat zipatazo mbili baada ya hapo wapi kilicho changu na kuchapa mwendo nikiwaacha watu wakicheka cheka tuu na office yao!!

YA KUPENDEZA
Share:

Oct 10, 2012

MAWASILIANO

East Africa,Tanzania.
Dar es salaam.
Magomeni.
Office: +255789476655
Cell: +255659161111/714973797
Email:mustaphamadish@gmail.com
Instagram
Facebook
Twitter

Share:

Sep 26, 2012

DSTV IMENIFANYA NIIJUE IKWIRIRI!!

DSTV bado inafanya vizuri na ukizingatia haina mipaka ndani ya Tanzania na ndo sababu ya kukufanya popote ulipo unaweza kufunga na ukaona kila ambacho unapaswa kuona kutokana na Package uliyoilipia!!
Kwa mantiki hiyo ikafanya watu watoke sehemu moja inaitwa IKWIRIRI na kutaka nikawafungie DSTV ili wacheck mipira na mengine ya kupendeza ila kubwa likiwa mipira,nami si nipo kwa ajili ya kufurahisha wengine huku mkono ukienda kinywani nikasababisha kama ambavyo unaona mwanaume hasifiwi sura!!





Hapa kazi tu!!
 Safari ilikuwa ni ya siku moja tu,nimetoka Dar mchana nikafika kule jioni nikapumzika kisha siku inayofuata asubuhi nikafanya kilichonipeleka nilipomaliza nikatembea tembea kidogo kuona IKWIRIRI ilivyo maana ndo mara ya kwanza kufika ila ambacho naweza kusema pazuri banaa nimepapenda kiasi kwamba hata kuweka kambi naweza kwasababu ni mjini na mji ndo unakua!!
Nnachofurahi kwangu safari moja huanzisha nyengine na ndo kilichotokea Mungu akipenda ntakuwepo tena next week,umuhimu wangu umeonekana hivyo nnahitajika kurudi!!
Share:

Sep 19, 2012

MBIO ZA ABUDHAB!!


ABUDHAB INSTALLATIONS!!
Napata maswali yenu mengi sana  kwamba mnataka kujua mnawezaje kupata Decoder za Abudhab!?,kiukweli kwa Tanzania sijui sehemu maalum ya wakala wa hawa jamaa na kama wapo tunaweza kufanya mawasiliano ili kwa wanaotaka niwaelekeze kwao kwasababu mimi ambacho nafanya ni Installations pamoja na vifaa vyengine kasoro Decoder tu.
Ugumu wa kupata Decoder ni jinsi ya kuagiza kutokana na ukweli kwamba hawa jamaa wapo Arabuni,hivyo hakuna jinsi zaidi ya kuagiza kwa kumtumia mtu ama kuagiza mwenyewe!
Unaweza ukanunua then ambacho mimi nitakusaidia ni kuhusu vifaa vyengine kama dish,cable na Installations ila kwa kuongezea tu unaponunua ni vizuri ukanunua card mbili,namaanisha na ya Aljazeera!!














Hapa nikiwa katika kufanikisha watu waone channels zilizomo baada ya kununua Decoder waliponunua then wakanitafuta nikawapelekea Dish na vifaa vyote vilivyohitajika na kuwafungia kisha nikachapa mwendo maana wengine pia walikuwa wananihitaji!!!
Share:

Sep 1, 2012

UZURI WA FLAT SCREEN KWA UKUTA!!

Kwanza inapendeza asikwambie mtu,ipo salama pia na haichukui nafasi kubwa,zaidi ya yote unakuwa wa kisasa zaidi na ambaye unakwenda na wakati,kama bado upo nyuma huyu ameshakuacha!!
Si kama nauza TV flat laa ila ambacho nafanya ni kufunga tu kama hivi,hii ni office ila nilianzia nyumbani kwa moja ya wafanyakazi wa hii Office baada ya kufanya vizuri ndipo nikatakiwa nifanye Installations ya Office nami ndo nikafanya haya ya kupendeza!!

Hapa ni kudrill mwanzo mwisho!

Ili niweze kufunga kishika TV!!

..........

 Nikiweka TV baada ya kfunga tv bracket!!!

 Inapendezaje!!

 Hapa nje nikiset Dish ya DSTV!

 Lazima umalize hivi kuweka muonekano mzuri na kazi saafi!!!!
Hapa nimefanya Installations ya DSTV na Local Channels.
Share:

Aug 23, 2012

MWENDO NDO ULE ULE!!

Wenye kujua wataendelea kujua na wasiojua sitaacha kuwajuza!
Hiki ni chumba cha kulala,matakwa ya mteja ndivyo nilivyoyatimia!
Kwa kufunga Flat screen hapo ilipo na DSTV!!
 Unaonaje kulivyopendeza!!
 Mimi je!!
 Ng'aa!!
Nikachukua kilicho changu na kuchapa mwendo!!
Share:

Aug 11, 2012

OFFER KWA WATEJA WANGU WOTE!!

Kwa wale wateja wapya na wa zamani nafasi yako hii!!
DISH MPYA YA LOCAL CHANNELS Tsh 280,000/=!!
Inajumuisha vifaa vyote pamoja na ufungaji!!
Unapata channel za Tanzania na nyenginezo za nje,ambapo inajumuisha zaidi ya Channels zaidi ya 50 bure!!
Share:

Jul 29, 2012

INSTALLATIONS YA TV ZAIDI YA 1!!

Hakuna sababu ya kufunga Dish zaidi ya moja ya aina moja kwa nyumba moja kwasababu tu una TV zaidi ya moja na unahitaji channels zipatikane kwa TV zote!
Hii inatumika kama kwenye Hotel au Lodge lakini pia inaweza ikatumika hata maofisini ama hata nyumba binafsi!!
Ambacho unapaswa kufanya ni kujua channel gani unataka na je ni za bure ama za kulipia kisha unapata mchanganua kutokana na matakwa yako na utakapoafiki kazi inaanza ilihali unalolikusudia ndilo utakalo liona ontime!!
Huduma hii inawezaekana kwa channel aina zote za bure na kulipia!!
Share:

Jul 28, 2012

CHANNELS ZA BURE!!


 Wengi wanapenda kupata channel ambazo hazina malipo ya mwezi,ambazo ukifunga inakuwa ndo umefunga labda iharibike dish na ahitajike fundi afanye ufundi wake!!
Channels zipo nyingi sana ambazo hazina malipo ya mwezi ila ambacho huwezi zile channels zilizo hotest za kulipia ukazipata bure ijapokuwa baadhi zipo bureee!!
Kupitia Dish ndigi kwa kubwa kuna channels nyingi za bure ila yategemea na wewe mapenzi yako wapendelea channels za namna gani!!
Unaweza kuuliza wala usisite na ukapata ufafanuzi ulio sahihi kabla ya kufunga channels utakazo!!
Channels hizo unaweza ukafunga nyumbani,Hotelini,Ofisini,n.k!!
+255 716 899 155
Share:

Jul 20, 2012

Dish yako inasumbua!!??


 
Dish c Antenna za tube ukasema ikileta mushkeri ushike bomba na kuzungusha!!
Dish inahitaji ufundi na mafundi wake kama sisi!!
Swali je dish yako inasumbua!!??
Kama kupoteza signal!
Picha kukata kata!
Unataka kuhama!
Umenunua uliponunua lakini huna mafundi wa kukufunga!
Na mengineyo kama hayo kwa msaada kiufundi zaidi unaweza wasiliana nasi:
Iwe unatatizo nyumbani kwako,Hotelini kwa wale wamiliki hotel,iwe bar,kwenye lodge,kwa office n.k.
Huduma ni zaidi ya malipo ulipayo!!
Share:

Jul 1, 2012

DSTV OFFER!!!!149,000/=


Kwa Tsha 149,000/= unapata vifaa pamoja na Installations ya single view!!
Then unachagua package uipendayo na kuilipia kwa utaratibu uliowekwa kama ifuatavyo:-
Access $10 - Channels 40. Kama Tsh 16,000.Kwa offer unalipia 4 miezi.
Family $20 - Channels 55. Kama Tsh 32,000.Kwa offer unalipia 3 miezi.
Compact $30 - Channels 60. Kama Tsh 48,000.Kwa offer unalipia 2 miezi.
Compact plus $50 - Channels 70. Kama Tsh 80,000.Utakavyo.
Premiur $80 - Channels 100. Kama Tsh 128,000.Utakavyo.
Unaweza ukapanda na kushuka kutokana na chaguo lako ila kwa offer ni lazima ilipwe kwa utaratibu huu!
Pata huduma fasta na inakufuata mpaka ulipo!!
Piga +255 789476655
Offer ni mpaka kuisha kwa bidhaa!!
KUPATA BEI MPYA YA VIFURUSHI Bofya Hapa

Share:

Jun 21, 2012

DSTV KWENYE RECEIVER IMEKUFA!!


 Hii ni Receiver
Zamani ilikuwa unaweza ukanunua Receiver yeyote ambayo inasoma card then unaenda DSTV wanakuuzia smart card kisha wanalink baada ya hapo unakuwa mteja bila kununua Decoder hii ilikuwa inamfanya mteja kuweza kupata Channels za DSTV na zile za bure kama Local kiasi kwamba hata usipolipia DSTV utaendelea kuona zile za bure!!
Lakini huduma hii kwa sasa wamesitisha ili kupata huduma za DSTV ni lazima upate Decoder za DSTV!!
Hii inakuwa huduma ya pili kufungwa ya kwanza ikiwa ile ya kupata DSTV kwa kutumia C BAND na wale wenye Decoder za zamani kwa sasa pia hazifanyi kazi
 Decoder hii ya zamani

 Hii nayo ya zamani lakini unapata DSTV

 Zifuatazo ndizo mpya single view Decoder:







Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita